Msaada jinsi ya kusafisha ukungu kwenye taa za gari

Sijui kama umesha solve tatizo lako. Ila kama bado nenda kwa hawa jamaa Autovision wako Sinza Mapambano.

Nimepoteza namba yao ila Instagram wanatumia autovisiontz

Wana gharama kidogo kusafisha taa Tsh 70,000 ila haichukui dakika 10 taa zote mbili.

Ila zinarudi kwenye hali yake ya dukani. Sijajua kama ni permanent au ni kwa miaka/miezi kadhaa ila wako vizuri.
 
Tumia majivu, ( weka majivu kwenye kitaulo safi anza kusugua taratibu mpaka uhakikshe taa imeanza kuteleza, mwagia maji safi umemaliza) ila make sure unayachambua kutoa vimkaa ili usikwangue taa...halafu lete mrejesho
Ngoja nijaribu hii
 
Nenda Lumumba pale vijana watakuchangamkia kukusafishia!Au nunua kabisa wewe mwenywe dawa yake inauzwa elfu 8 unakuwa wallau kila wiki unasugua na kitambaa saana baada ya kupaka hiyo dawa!Then taa ina ng’aa
 
Back
Top Bottom