Msaada: Jinsi ya kupunguza au kutokuwa na hasira

mwayungi

JF-Expert Member
May 9, 2017
1,814
3,079
Wapendwa wa JF habarini, poleni na majukumu.

Kama kichwa cha habari kilivyo,

Naomba ushauri ili niweze kupunguza au kuondoa kabisa hasira katika maisha yangu.

Wakuu ninatabia ya kupandwa hasira hata kwa jambo dogo mimi ni mtu wa kukasirika sana, nikitofautiana tu na mtu kwa jambo lolote lazima nikasirike. Hasira hizi zimenifanya baadhi ya ndugu na marafiki wapungue nimeshindwa kujitawala.

Nahitaji ushauri wenu nifanye nini ili nisiwe mtu wa hasira hasira.
 
Wapendwa wa jf habarini poleni na majukumu.Kama kichwa cha habari kilivyo naomba ushauri ili niweze kupunguza au kuondoa kabisa hasira katika maisha yangu.Wakuu ninatabia ya kupandwa hasira hata kwa jambo dogo mimi ni mtu wa kukasirika sana,nikitofautiana tu na mtu kwa jambo lolote lazma nikasirike.Hasira hizi zimenifanya baadhi ya ndugu na marafik wapungue nimeshindwa kujitawala nahtaj ushaur wenu nifanye nn ili nisiwe mtu wa hasira hasira
Penda kusoma neno LA Mungu na kuhudhulia katika nyumba za ibada kwa ushauri zaidi usisite kurudi tena.
 
Kaombewe hilo in pepo la kufisha na kuteketza. Yupo Mchungaji mmoja wa kkkt anayaweza hayo. Tuwasiliane private nikuambie anapatikanaje
 
Hasira ni sehemu ya ukichaa (failure to control your temperament), zipo dawa za kutuliza huo ukichaa, wahi haraka sana unywe faster usije ukadhuru watu wengine.
 
Yasome hayo maandiko ya Mungu na kuyatafakari kwa kina pia jaribu kukutana na watu wa kiroho kwa maombezi, wakati mwingine ni shetani,mapepo na hata tabia fulani za kurithi umefungamana nazo kwahiyo bila maombi ni kazi bure.
 
Pole Sana kwa hilo maana mara nyingi hali kama hiyo inakupa majuto sana baada ya kujikuta umemkasirikia mtu kwa sababu isiyo ya msingi.
Ila kwa wewe kujua ni tatizo tayar ni nusu ya jibu. Mm pia kuna wakati nilipitia hali kama ya kwako nilijitahidi kuacha nikashindwa,ilibidi nimwombe Mungu sana na kujilazimisha kuacha hasira hatimaye nilifanikiwa kupunguza sana hasira. Jitahidi kuwa mtu wa ibada na kumwomba Mungu au kuwashirikisha wengine wakuombee nina hakika utafanikiwa. All the best
 
Back
Top Bottom