Msaada:Jinsi ya kuipata hii Boda Boda

Msaada:Jinsi ya kuipata hii Boda Boda

Kheri ya mwaka mpya iwe kwenu wakuu.
Nashukuru kwa mchango wenu wa kimawazo maana simu ilipatikana.

Dogo alienda polisi, akapewa RB na polisi wakafanya kwenda TRA na mpaka mhusika akapatikana.

Ila kama mjuavyo tena jeshi letu lilivyo, alivyoitwa kwenda kuchukua vitu aliishia kupewa simu moja tu na akaambiwa vitu vingine havijaonekana na akaombwa na hela ya soda.

Cha muhimu nashukuru kwa ushauri wenu sana.
Duhhh......[emoji47] [emoji47]
Hatari sana

Nenda TRA kufatilia mmiliki wa hiyo bodaboda kupitia utaratibu wake Wa kulipa kodi huenda ukamfahamu.

Hizo plate number unazificha za nini?

Pole sana Kiongozi. Bila shaka itakuwa ni maeneo ya njiani kutokea Main campus kuja New Hostel. Maeneo hayo huwa ni kichocheo cha vijana vibaka kama hivyo.

Mdogo wetu akishatuliza akili mshauri haya yafuatayo.

1) Si vizuri kila wakati kutembea na ATM Cards, tena ATM zote mbili at once.? Atembee nazo pale tu anapohitaji kutoa pesa ATM. Otherwise iwe anasafiri.

2) Si vizuri sana kutembea na kiasi kikubwa cha pesa kisichokuwa na matumizi kwa wakati huo.

3) Fuata ushauri hapo juu, Post # 3.

Nenda na rb ya police TRA

Ova
 
Asante mkuu, dogo alipata simu yake ila vitu vingine naona polisi wamesaidia kujilipa posho.

Kheri ya mwaka mpya
Si ana RB mkuu au haitasaidia.

Bodaboda wenzangu wamekuwa wajinga sana wanafanya tunakuwa hatuaminiwi.
 
Wamiliki wengi wa bodaboda maranyingi huwa hawabadilishi majina ya umiliki pindi wazinunuapo toka kwa wauzaji. Na hufanya hivyo kwa kuogopa gharama zinazohitajika TRA ili kubadili umiliki. Sasa basi anaweza kwenda TRA lakini asifanikiwe kupata information kamili za mmiliki bali atapata info za kampuni iliyoagiza pikipiki hiyo kutoka china. Kuna uwezekano mkubwa sana wa kupoteza hivyo vitu kwa huyu mdogo wetu mpendwa.
Ni kweli, kama hiyo namba ya pikipiki hiyo si fake TRA wataifahamu kampuni iliyoagiza hiyo mashine na wenye kampuni watamjua muuzaji na muuzaji atamjua mnunuzi kama wote walitunza vizuri nyaraka za kumbukumbu.
 
Mkuu TRA watakubali kutoa information za mtu bila ridhaa yake?
Hata ukizipata hizo details itasaidia nn kuna mamilioni ya pikipiki nchi hiI. Hata hao TRA watakushangaa. Wao wanahangaika na kuongeza mapato ww unaleta utani wa demu wako kuporwa kipochi na Atm card za NMB. Potezea na ugharamie simu mpya Acha kukwepa majukumu ndugu
 
Asante mkuu, dogo alipata simu yake ila vitu vingine naona polisi wamesaidia kujilipa posho.

Kheri ya mwaka mpya
Ndiyo tatizo la polisi wetu. Wao wako busy na upinzani. Ndiyo maana hawaaminiki. Mm siwezi amini polisi 100%
 
Back
Top Bottom