The dream
JF-Expert Member
- May 10, 2015
- 999
- 997
Habari za mida hii wana jamvi??
Nahitahitaji msaada wa haraka wa kimawazo juu ya jambo hili!!
Mdogo wangu wa kike anasoma chuo cha Sokoine (SUA) -Morogoro na jana mida ya saa 1 jioni wakati anatoka kwenye vipindi pale pale chuoni akiwa anatembea na mabinti wenzie ghafla ilipita boda boda na kumukwapua mkoba wake uliokua na simu zake 2,card za benki 2,vitambulisho vyake, notisi za chuo na kiasi cha fedha taslimu kisha yule boda boda aligeuka na kuanza kuwachekea na kisha akaongeza mwendo na kutokomea na vitu hivyo ila kwa bahati nzuri alifanikiwa kunukuu plate number zake.
Ameenda polisi kapewa RB.
Naomba msaada wa jinsi ya kuipata hii boda boda kwa kutumia plate number zake ili arudishe vitu vya mdogo wangu.
==============
Kilichotokea baada ya kufuata ushauri wenu
Kheri ya mwaka mpya iwe kwenu wakuu.
Nashukuru kwa mchango wenu wa kimawazo maana simu ilipatikana.
Dogo alienda polisi, akapewa RB na polisi wakafanya kwenda TRA na mpaka mhusika akapatikana.
Ila kama mjuavyo tena jeshi letu lilivyo, alivyoitwa kwenda kuchukua vitu aliishia kupewa simu moja tu na akaambiwa vitu vingine havijaonekana na akaombwa na hela ya soda.
Cha muhimu nashukuru kwa ushauri wenu sana.