jinsi ya kuroot simu ya Vodafone VFD 301
1. unahitaji mafaili ya simu ya vodafone vfd 301
unaweza kuyapata hapa (kama unayo tayari usidownload)
2. TWRP recovery ya vodafone vfd 301 (nimeiport kutoka kwa stock recovery)
unaweza kuidownload hapa
3. Root manager app. Tutumie Supersu, ambayo
inapatikana hapa
4. SP Flash tool,
unaweza kuipakua hapa
Tuanze sasa
na assume tayari umesha install driver za usb za simu yako kwenye kompyuta yako, kama huna basi install hizi
a.) MTK USB DRIVER ambayo unaweza
download hapa, na
b.) CDC Driver ambayo
utaidownload hapa (maelezo jinsi ya kuinstall yako
hapa)
1. Nenda kwenye folda lako lenye mafaili ya simu yako na badili file lilioandikwa recovery.img na hili nililoliweka hapo namba mbili.
2. Fungua SPFlash tool (as admin) kisha load scatter file kutoka kwenye folder la simu, likiload hakikisha umechagua recovery pekeake halafu bonyeza download
3. Hakikisha simu imezimwa na una waya wa usb upo tayari kwenye pc, chomeka waya wako, SP flash tool itaanza kusoma, ndani ya sekunde mbili tatu itakuwa ishamaliza na itaweka tick. chomoa simu yako kisha bonyeza volume up na power (kwa pamoja) kwa sekunde kadhaa uone kama tumefanikiwa kuflash TWRP recovery
4. Washa simu yako kisha copy file tulilodownload namba 3 kule juu. halafu zima simu kisha ipeleke kwenye recovery(power+vol.up)
Twrp ikifunguka bofya install, kisha litafute file ulilocopy kwenye simu, libonyeze kisha swipe to confirm flash.
Mpaka hapo tayari simu yako itakuwa imekuwa rooted. unaweza sasa kuirestart, mara ya kwanza itachukua muda kidogo kuwaka. ikishawaka angalia kama kuna app ya supersu. ili kujiridhisha unaweza kuinstall root checker uone kama imekuwa rooted
Hapo unaweza ondoa app ambazo zimewekwa na voda na makorokoro mengine ambayo huyahitaji, unaweza kuondoa ads, simu iwe nyepesi..
Jinsi ya ku unlock simu ya vodafone VFD 301 iweze kutumia mitandao yote
Credit:
ashomile kwa kutoa mwangaza kwenye post za awali
hapa tunahitaji Cracked version ya NCK MTK ANDROID FULL NO HWID ambayo
nimekuwekea hapa
1. extract file ulilodownload hapo kwa kutumia winrar. (Hakikisha antivirus yako imezimwa kwa muda maana uwa inafuta crack files)
2. ukisha extract, run file hili ---> Nck Mtk Dongle 2.5.6.2 Loader By Gsm_X_Team.exe "as administrator" likishafunguka inakuwa inaonekana hivi. a.) chagua tab ya unlocking b.) hakikisha inasoma 0 by CPU na MT6580 kisha bofya direct unlock.
3. ukishabonyeza itakupa maelekezo ya kufanya, hakikisha simu yako iwe imezimwa kabla hujaichomeka, lakini betri usiitoe, chomeka usb cable yako kisha tulia ianze kazi. Baada ya sekunde kadhaa itamaliza na itaonekana hivi
4. Restart simu yako ukiwa umeweka line za mitandao tofauti ili uendelee kufurahia kasimu haka kadogo
Mafaili yote niliyoyatumia
nimeyaweka hapa kama utayahitaji yote
ANGALIZO: SITAHUSIKA KWA KUHARIBIKA KWA SIMU YA MTU YOYOTE, UNAPOAMUA KUFUATA HAYA MAELEKEZO, YAFUATE KWA KUPENDA KWAKO