Jinsi ya kubadili ROM (android version)

Hackerz

JF-Expert Member
Apr 25, 2016
352
235
JINSI YA KU UPDATE ANDROID KITKAT
KWENDA LOLLIPOP
No Computer needed…..
Utangulizi:
Bado Teknologia inakua kila sekunde.. Yapo
Maboresho kila Nyanja hasa katika Mawasiliano kwa ujumla. Kompyuta na Simu za Mikononi
zimechukua nafasi kubwa katika Nyanja nzima
ya Mawasiliano.
Kampuni mbalimbali zakutengeneza simu nazo
kila nyakati zinajitahidi kutoa Matoleo mapya na
yalioboreshwa. Ipo mifumo (Operating Systems) mitatu inayofanya kazi katika Simu za
kisasa zijulikanazo kama ‘Smartphones’. Mifumo
ni Android, iOS na Windows phone. Upo
ushindani mkubwa kwa Watengenezaji wake
hali inayosababisha Uboreshaji kwa kila mfumo.
Binafsi napenda mifumo yote lakini mfumo wa Android ndio unatumika na watu wengi duniani
kwa sababu kuu zifuatazo;
(i) Simu zinazotumia mfumo huu zinauzwa kwa
Grarama ndogo zikilinganishwa na zinazotumia iOS na Windows phone.
(ii) Kuna zaidi ya Program 1.6 million
zinazofanya kazi kwenye mfumo huu amabazo
mtumiaji anaweza kuzitumia kwenye simu yake
kuendana na Mahitaji yake.
(iii) Ni rahisi sana ku root Simu za Android. Rooting ni kitendo cha kukupa uwezo wa
kutumia na kuifurahia simu yako kwa asilimia
mia moja. Ukisha root simu yako unakua na
uwezo wa ku UPDATE mfumo wa simu yako
(Mfano kutoka Kitkat kwenda Lollipop), kuweka
Program zilizozuiwa na Android Developers (Mfano program maalum za Kutunza Chaji, ku
‘boost’ simu yako, kukuongezea RAM, program
za kukuwezesha kuipata simu yako hata pale
mwizi anapoi flash), kutoa ‘System applications’
ambazo huna kazi nazo, kuufanya mfumo wa
simu UWE KAMA UTAKAVYO wewe, nk… Kwa waliobahatika kuisoma Makala yangu ya
JINSI YA KU ROOT SIMU YAKO YA ANDROID,
nafikiri wananielewa zaidi hapa.
Kama hujaiona Tembelea ukurasa wangu wa
Facebook au wasiliana nasi 0757 413 078.
Waweza pia kui search google kwani iliwekwa kwenye tovuti ya JamiiForums.
(iv) Zipo Program/ Applications nyingi na za
kisasa ambazo bado watumiaji wa iOS na
Windows phone hawajazipata.
Mfumo huu wa Android una Matoleo yafuatayo
hadi Makala hii inapoandikwa ambayo ni: 1. Cupcake (1.5)
2. Donut (1.6) 3. Éclair (2.0 – 2.1)
4. Froyo (2.2 – 2.2.3)
5. Gingerread (2.3 – 2.3.7)
6. Honeycomb (3.0 – 3.2.6)
7. Ice Cream Sandwich (4.0 – 4.0.4) 8. Jelly Bean (4.1 – 4.3.1) 9. KitKat (4.4 –
4.4.4)
10. Lollipop (5.0 – 5.1.1)
11. Marshmallow (6.0 --- )
Matoleo haya yanaboreshwa kila yajapo Mapya
na Mpaka ninapoandika Makata hii Simu nyingi za Android zinazotumiwa na wengi zinatumia
Andriod 4.4 – 4.4.4 (Kitkat). Mfumo wa mwisho
(Marshmallow) umewekwa kwenye simu
zilizotolewa hivi karibuni kama vile Nexus 6P,
Nexus 5X nk... Kujua toleo lako nenda
Settings˃About phone˃Android version. Kama upo Kitkat, huu ni Muda sahihi wa
kufurahia Lollipop Experience. Binafsi Simu
yangu ni Tecno H6 na nilishawishika kutoka
KitKat kwenda Lollipop kwa sababu zifuatazo:
(i) Mfumo wa Lollipop uko ‘stable’ na fasta kuliko
KitKat (ii) Unatunza chaji kuliko Kitkat kwani ‘bugs’
nyingi zimekua fixed na pia ‘Power saving
feature’ imeboreshwa
(iii) Una mwanga zaidi (More brighter) na pia
una Visual effects nzuri na za kuvutia
(iv) Rahisi sana ku root (v) Una uwezo wa ku manage app nyingi bila
ujumbe wa ‘program not responding’ au
‘Unfortunately, program has stopped’ JINSI YA KU UPDATE KITKAT KWENDA
LOLLIPOP;
Vinavyohitajika ; - Muda - Simu ya Android iliokua ROOTED tayari (ipo
Makala jinsi ya kuroot, kwa atakaehitaji)
- Memory Card isiyo na tatizo ( angalao 8GB)
- Kifurushi cha Internet angalao GB 1 (kwa ajili
ya ku download ROM na ku install program zako
muhimu baada ya kufanikisha zoezi zima) Zoezi hili ni LA HATARI SANA KWA
ATAKESHINDWA kufuata hatua zifuatazo kwa
MAKINI kwani Simu yako HAITAWAKA tena
ukikosea! Kinachotakiwa ni UMAKINI na Uhakika
wa USAHIHI kwa kila unachokifanya! Ndio
maana nimetangulia kusema andaa MUDA maalum unapoanza—usiwe na kazi nyingine. Binafsi nilisha update SIMU ZAIDI YA 40 sasa
bila kuua hata moja!
Kwa kuanza, naamini simu yako tayari umeshai
root, na sasa tuanze kupitia hatua moja baada
ya nyingine kufanikisha zoezi zima.
1. Hakikisha simu yako ina Chaji ya kutosha. Inashauriwa wakati wa ku update iwe kwenye
chaji.
2. Wezesha ‘’Developer Options” kwenye simu
yako. Nenda Settings>About phone>Build
number. Baadhi ya simu (LG na HTC) nenda
Settings>About phone>Software information>Bui ld number. Ukishafika kwenye Build number gusa hapo mara saba
(tap 7 times)…mpaka uambiwe “You are now a
Developer” Sasa nenda Settings>Develo per options>USB debugging. Weka tiki hapo (kama
haipo). Hatua hii kwa wengi hua ni tayari kwani
hufanywa wakati wa ku root.
3. Nenda settings>Securi ty>Unknown Sources. Weka tiki hapo (Kama haipo).
4. Nenda Playstore install program inayoitwa
[ROOT] Rashr – Flash Tool. Usiifungue baada
ya kui Install.
5. Hatua hii ni ya Muhimu sana. Kabla
hatujaiangalia tunapaswa kujua Mambo machache.
(i) Recovery – Hiki ni kipengele cha Mfumo wa
simu au hata Computer ambacho
kimetenganishwa na Mfumo wa kawaida wa simu. Hiki husaidia tunapo flash/ku update
simu.
(ii) Bootloader ni sehemu ya Mfumo wa simu na
hata Computer ambacho ndicho huamua Simu
au Computer kuwakia kwenye Recovery au
iwake kawaida. Kwa wale wanao Install Windows OS kwenye Computer zao
wananielewa zaidi hapa. Unapoweka DVD ya
Windows files na kuwasha PC yako na
Kubonyeza F11 KEY. Hapo ni kwamba unai
Instruct PC yako iwake kwenda kwenye
Recovery. Ndicho tunachokifanya tunapo Install Android Lollipop ROM.
(iii) ROM (Operating System Image) – ni Flash
files ambazo ndizo huwekwa kwenya Read Only
Memory (ROM) ili simu iweze kuwaka.
(iv) Android Custom Recovery. Watengenezaji
wa Simu za Android wame lock Bootloader ili watumiaji wake wasiweze ku Install ROMs
mbalimbali kwenye simu hizo. Wameweka
Recovery ambayo hairuhusu kuflash chochote.
Sasa hapa ndipo hatua ya tano ilipo, Ku Unlock
Bootloader ili tuweze ku flash ROM yoyote
kwenye simu ya Android. Kufanikisha hatua hii tuna flash Android Custom
Recovery nyingine itakayoturuhusu kuflashia ROM mpya Kwenda kwenya Mfumo wa simu.
Zipo Android Custom Recovery mbili (2) ambazo
hutumika sana tunapo flash Android Devices
ambazo ni ClockworkMod Recovery (CWM) na
Team Win Recovery Project (TWRP). Hapa
nashauri twrp kwani ni rahisi kutumia, inaeleweka zaidi na ina Option nyingi.
Hatua za ku Install twrp;
- Kwa kutumia simu yako au PC, nenda google
kisha search tmrp ya Simu yako. Mfano kama
unatumia Tecno H6, search ‘twrp image for
Tecno H6’ au ‘Team Work Recovery Project image for Tecno H6’ kisha i download.
- Ukishai download iweke kwenye Memory Card
ya simu unayotaka kuiflash.
- Fungua Rashr (rejea hatua ya nne hapo juu)
kisha gusa ‘Recovery from Storage’. Hapo
chagua twrp ulioi download. Gusa ‘Yes’ utakachoulizwa. Kama itakua imefanikiwa Utaona ‘ Partition flashed. Reboot
into Recovery now?’ Gusa ‘NO’ Kisha nenda
hatua ya 6.
6. Hatua hii ni ya KU DOWNLOAD Lollipop ROM
kwa ajili ya SIMU YAKO. Ziko ROMs nyingi
kutoka kwa Developers tofauti. Binafsi nilishakutana nazo nyingi na asilimia
kubwa zilikubali lakini nyingine hua zinakataa!!
Nenda Google kisha search ROM ya Simu
yako…Mfano kama unatumia Tecno H6; search
‘Lollipop ROM for Tecno H6’ Nyingi hua ni zaidi
ya MB 200. Tahadhari; Kabla ya ku download ROM utakayoiona soma
kwanza COMMENTS za walioitumia ili uweze
kujua kama ilikubali kwao. Baadhi ya ROMs hua
zilishakua infected na Virus na ukizi Install hua
zinakataa!! Na zikikataa hua nia HATARI kubwa
kwani simu haitawaka tena! Baada ya kui download iweke kwenye Memory
Card ya Simu unayotaka kui flash/update.
7. Hatua hii ndio kiini cha Zoezi zima! Nunua
kikombe cha Kahawa weka pembeni, mwombe
Mungu kisha ENDELEA…. Fungua tena Rashr
kisha gusa ‘Reboot Recovery’. Sasa simu yako itawakia kwenye
Recovery ( Team Win Recovery Project) kama
inavyoonekana pichani.
Kuona picha omba pdf Doc (0757413078)
Kama tulivyokwishaon a, zoezi la Kuflash linaweza ku fail..na ikitokea SIMU HAITAWAKA
TENA!
Ni mpaka Computer na USB vitumike KUFUFUA
simu hio! Sasa kuepuka hili, hua tunahifadhi
mfumo uliopo ili likitokea tatizo tuurudishe simu
iwake.. Ili kuuhifadhi mfumo uliopo, gusa ‘Backup’ , weka alama kwenye Boot, Unboot,
nvram, System,
na Cache,,, gusa Storage na uweke alama
kwenye sd card kisha ‘Swipe to Back Up’
Ikishamaliza ku back up rudi nyuma kisha gusa
‘wipe’ ˃ ‘Advanced wipe’ kisha weka alama kwenye Dalvic Cache, System, Cache na Data
kisha ‘Swipe to Wipe’ Kumbuka ku format
System ndicho kinachofanya Simu isiwake tena
kwani OS haipo tena mpaka hatua hii. Kwa hio
hakikisha Backing Up Process ilikamilika kabla ya
ku format/wipe Simu. 8. Baada ya ku back up na ku wipe, rudi
nyuma, gusha ‘Install’, chagua ile ROM ya Simu
yako uliokwishai download kisha
‘Swipe to Confirm Flash’. Ni ndani ya Dakika
zisizozidi 10, utakua tayari una Android Lollipop
experience kwenye simu yako!!! Gusa Reboot ˃ System
Angalizo; Kuna baadhi ya Lollipop ROMs
ambazo System apps hazijawa included. Uwe
makini hapo, kama hio ROM haina apps, lazima
kuna maelekezo ya ziada ulipoipatia hio ROM.
9. (Hatua hii ni endapo Flashing process ili fail…) Gusa Restore, chagua Package yenye
tarehe sahihi kisha Swipe to Restore.
Hapo ule Mfumo uliopo utarudishwa na simu
yako ITAWAKA kama kawaida. Kama bado
utakua na nia Tafuta ROM nyingine tofauti
kisha jaribu tena. Hitimisho: Mwandishi wa Makala hii hatahusika kwa
Uharibifu wowote utakaofanywa na baadhi ya
Watu watakaokosa Umakini wakati wa Kuflash
Simu zao. Hatua zote zilizoelezewa hapa ni
SAHIHI na alieziandika hua anazitumia na
kufanikiwa. Waweza pata Msaada kutoka kwa Mwandishi
wa Makala hii kama vile;
- Kupata ROM sahihi kwa ajili ya simu yako
(ndani ya saa 24). Hua nina ROM za simu
ambazo ni popular na zilikubali kwenye Simu
hizo. Ukihitaji utatumiwa ‘download link’ ili ui download kwenye simu yako.
- Kua na mawasiliano ya moja kwa moja na
Mtaalam pale unapoanza zoezi hili… hapa
utakua unatoa taarifa kwa kila hatua ambayo
utakua huelewi au kama kuna tatizo. - Kuuliza
swali lolote kuhusu Makala hii. Nikutakie kila la Kheri wewe utakaeamua
kuchukua hatua za kufurahia Maisha MAPYA na
Android Lollipop Experience…
 
Asante kwa makala hii.. kabla ya cupcake kulikuwa na version mbili ambazo hizo hazikutumia majina ya vyakula...
 
umenichanya physics nilikuwa zero
Aaah mkuu sidhani kama physiccs inahitajika hapa. You just follow the instructions dot by dot thereafter you shall be a super user of your phone into lollpop version. Nakutakia umnuda mwema wa kufanya hiki kitu
 
Nipo magomen dar (inabid kam ujaelew nipgie 065460769 ntakuelkez
 
Jamaa nimekukubali. .ila simu yangu nikiwasha wi-fi huwa inaniletea kabisa ili nianze ku download OS lollipop. Vipiii naweza ìruhusu haiwezi leta madhara?
 
Yaani nikiwasha wi-fi network huwa simu inaniletea option direct ya kuanza ku download operating system..yaani inatokea msg ambayo ina details zoote za lollipop operating system yaani iko ready to start downloading. Ila huwa mala nyingi naogopaga ku confirm. Sasa swali langu ni hili mkuu, niki download bila ku pitia settings yaani shortcut kama inavyoni direct sitoharibu? ??
 
Hizo ni Google ads huw zinazingua tu -....... (hazina ukweli wiwote)
 
Nipo magomen dar (inabid kam ujaelew nipgie 065460769 ntakuelkez
Nikikua nina huawei,
Ghafla tu siki hio

Ilianza kuleta errors


"Unfortunately playstore has stopped working"

Kila app nikigusa napata hio message.

Simu ikaanza kuji restart yenyewe.

Ikawa inajirestart tu

Nikaamua kuizima, like two hours kuja kuiwasha

Sasa hio error ndio ikawa kila sekunde, ikafikia hatua, app zote zikagoma kabisa.

Na kuji restart

Mara ikazima kabisa. Haikuwaka wala haikuingiza charge.

Hio itakua ni nini?
 
Yaani nikiwasha wi-fi network huwa simu inaniletea option direct ya kuanza ku download operating system..yaani inatokea msg ambayo ina details zoote za lollipop operating system yaani iko ready to start downloading. Ila huwa mala nyingi naogopaga ku confirm. Sasa swali langu ni hili mkuu, niki download bila ku pitia settings yaani shortcut kama inavyoni direct sitoharibu? ??
Mkuu hiyo ndo rahisi sana ku update maana developer wa kampuni ya simu unayitumia wame release OS kwaajili ya simu ya aina yako....hapo cha kufanya ni kuweka internet bando la kutosha kisha nenda update software na anza ku update software mpya kwenye simu yako....wala haina madhara yoyote sababu hiyo njia sio short cut kama hizi zingine za mpaka kuroot simu
 
Back
Top Bottom