ngosha2011
JF-Expert Member
- Aug 20, 2011
- 681
- 87
toa pesa upate pesa.
amalize mwaka? Sijui....
yuko kada ipi?kama ni mwl hadi mwka mmoja au apate tsd namba
rules toa pesa upate pesa... Muhimu sana mwambie aende kuongea na huyo ambae anasubiria sahihi yake kwamba mkopo ukitoka atampa kiasi fulani simple like that... La sivyo mwakani tena atasubiri sana...
mbona ishu ipo rahisi namna hiyo...mwenye njaa aambiwi kula akunyue mkono tu asiwe na mkono wa birika
ntafanyia kazi thanx sana,kwa hiyo kwa sasa bado hayupo kwenye haki?
tatizo sio mkono wa birika,kwanza ajue kuwa ana haki ya kupata mkopo ndipo atoe chochote
haki inatafutwa...
Kuna rafiki yangu kapata
kazi mwaka huu mwezi wa pili serikalini,na barua ya ajira anayo,alikuwa
anaomba mkopo benk ya nmb akajaza form na kuweka viambatanisho vyote
vinavyotakiwa na benk,ishu ikaja kwenye kupata sahihi huko
halimashauri,DT amesaini ,mkubwa wake wa idara amesaini,bado sahihi moja
ya mkurugenzi wamemzungusha kama mwezi hivi,bila kusainiwa huku akipewa
majibu ya kuwa unaruhusiwa kupata mkopo mpaka ifike mwezi kama ule
uliyo ajiriwa,mwenye kujua ukweli wa hili! Maana anaona kuna kila dalili
za rushwa au ndio ndivyo ilivyo?
Nawasilisha kwa mawazo zaidi
ni mwal wa kike au wa kiume? Labda papuchu inatakiwa.......otherwise nadhani hapa siyo mkurugenzi, ni wale wa mapokezi. Issue ya mkopo wa ticha haizidi hata 8m, mkurugenzi ana mafungu hawezi kunyemelea kamkopo cha mwl.
akaongee na afisa utumishi wa manispaa yao amwelekeze utaratibu ili ajue kama anastahili au laa
ngosha2011, msipende kulalamika sana jaribuni kufanya utafiti kidogo vijana. Hilo moja, pili tumia neno saini na siyo sahihi kama ulivyoandika. Tatu na hii nadhani itakuwa point muhimu kwako ni kwamba huenda inatakiwa huyo rafiki yako athibitishwe kwanza kazini ndiyo awe na stahili ya kupata mkopo. Na kwa hiyo amethibitishwa kazini? Barua ya kuthibitishwa kazini anayo?