Mkuu JosM, hiyo msg nimuhimu sana kwako. Kutokana na watu kuwa walifungua akaunti zao na kusahau details walizoingiza, yahoo walianza kuweka hiyo page ili uweze kuwa na majibu muafaka ya "Secret questions". Hivyo jaza hiyo kitu haraka, na waweza kutumia maswali yao, ama kuweka maswali yako mwenyewe ambayo lazima uje ukumbuke majibu.
Siku ukipata tatizo utaulizwa hayo maswali ili kurudishiwa akaunti yako. Hivyo jaza wengi tutumiao yahoo tumeshajaza hilo.