Msaada jamani; Nywele kunyonyoka

mkandaboy

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
256
88
Habari zenu wana JF? Poleni kwa majukumu mbalimbali.
Tafadhali nisaidieni; Mama yangu mdogo ana tatizo la kunyonyoka nywele ambalo ameligundua miezi michache iliyopita. Zinanyonyoka zaidi anapooga ama kuzichana kwa chanio. Hazijawekwa dawa yoyote(mfano relaxer, curl etc), wala yeye hatumii dawa zozote kwa ajili ya ugonjwa wowote. Tafadhali kama kuna yeyote mwenye kufahamu tiba kwa ajili ya tatizo hili anijulishe.. Ahsanteni great thinkers..
 
Kila Tiba kati ya zifuatazo ni yenye kujitegemea.Chagua iliyo rahisi kwako. Isipokufaa ndipo uchague nyengine.

TIBA A
:Tafuta unga wa habat saudaa kachiri (komoni)-rocket,siki nyepesi na mafuta ya zeituni.
Kanda unga wa habat saudaa katika juisi ya kachiri.Changanya na kijiko kimoja cha siki pamoja na kikombe(200ml) cha mafuta ya zeituni.
Kosha kichwa kwa sabuni halafu sugua kwa dawa hiyo kila siku jioni.

TIBA B:T
afuta unga wa habat saudaa,juisi ya Jar-jiir,siki nyepesi na mafuta ya zaituni.
Changanya unga wa habat saudaa kwenye juisi ya jar-jiir pamoja na kijiko cha siki nyepesi.Koroga na kikombe kimoja cha kahawa (50ml) cha mafuta ya zaituni.
Kabla kutumia kosha kichwa kwa maji baridi na sabuni.Utasugua kichwa kwa mchanganyiko huo kila siku asubuhi na jioni.@mkandaboy Tumia ukipona nipe feedback.
 
Hali hii inaweza kusababishwa na lishe duni pia stress mbali mbali za maisha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom