Wakuu tafadhali naomba ushauri wenu, kuna mdada nlikuwa na mahusiano lakini tukaachana miaka saba iliopita baada ya kugundua kuna njemba nyingine inashiriki( ndio anaishi naye sasa hivi). kipindi naachana nae alikuwa mjamzito na alinieleza ni yangu. Lakini kila kitu kilibalika baada ya ishu zake kuvuja. kutokana na hasira nlizokuwa nazo nikamchana na sikutaka kujua chochote kuhusu hiyo mimba. Ingawa baadaye aliniomba radhi yakaisha, akajifungua salama na baadae akaniletea mtoto nikamuona, na nikamchukulia poa. lakini baada miaka mitatu nikapata ham ya kutaka kujua kama ni mtoto wangu ila njia ndio siioni. kuna mambo kadhaa ambayo yanasababisha nihisi akawa wangu. 1.Alipopata ujauzito alitaka autoe akidai kuwa haukupangwa tena huku akinililia, nilimgomea na kumwambia kuwa kama akitoa basi ndo ameuwa uhusiano wetu. 2. Ujauzito alinihakikishia kuwa ni wangu kabla hatujagombana. 3. mtoto alipokuwa mdogo alikua akiniletea kwa siri kama nikimwambia. 4. Wambea nao wamezidi maneno, "eti nimekataa mtoto." Huyo mtoto sijaonana naye miaka mitano, ila habari ninazopewa juu yake zinanipa kizunguzungu. Kwahiyo wakuu msaada wenu, nifanyeje nijue kwa uhakika kama nna changu ama la, sina shida ya kumchukua ila naogopa isije ikajulikana wakati nshaoa mwakani Mungu akipenda akaniharibia hali ya hewa kwenye familia yangu. NB:Jamaa aliyekua anagegedana naye alikuwa anajua kuwa mimi ndio mkuu wa kaya "nlikuwa naibiwa." Nawasilisha wakuu.