Msaada jamani miaka26 sina nachomiliki na sina muelekeo

Status
Not open for further replies.

Kamwene kamwene

JF-Expert Member
Jul 7, 2019
1,159
2,585
Hali ni mbaya jamani member mwenzenu naomba msaada wenu
Elimu yangu ni kidato cha nne
Sina muelekeo wa maisha yani asubuhi naamka kama mbuzi,natamani sana navyoona watu wanaamka wanaelekea kwenye majukumu mbalimbali..

Yeyote mwenye kibarau naomba
Yeyote mwenye ushauri naomba
Yeyote mwenye mchango iwe mtaji naomba

Naweza kufanya kazi mkoa wowote
Nimepata wazo la kutembeza viatu vya mtumba na kwenda navyo mnadani,
Mtaji ni laki moja na kuendelea
Naomba Mwenye chochote anisaidie namba yangu 0755293337
 
Last edited:
Ushauri wangu soma Veta chukua fani ya ujenzi watu wana jenga everyday Dar Dodoma na Zanzibar Kasome
Veta kibaha
Shirika la elimu kibaha
Shirika la elimu kisarawe
kazi zipo za kutosha huo ndio msaada wangu kwako sina kingine

Asante sana kwa ushauri,natamani sana ningepata elimu ya ufundi tatizo pesa,na hata ndugu wa kunisaidia sina
 
Relax
Kwanza nimefurahi kuwa uko tayari kufanya kazi.
Hata hivyo, kwa umri wako maana yake una chini ya miaka 10 tu ukiwa umeingia rasmi kwenye working class. So, una mengi ya kujiandaa na kujifunza.
Maisha ni hatua, chukua hatua
Jenga uwezo katika jambo unalopenda na kisha jiendeleze
nakutakia kila lililo jema kwako
 
usijali.... ushauri wangu kwanza achana na kitu kinaitwa "MUNGU YUPO"
Fanya kazi kwa kujiamini na kwa uaminifu hata kama ni kulima mchicha.....
JIAMINI WEWE NA USIWE MUONGEAJI SANA KUSEMA UNAWEZA KUJIFUNZA JAMBO KWA HARAKA SANA WAKATI UMESHINDWA KUJIFUNZA NAMNA YA KUFANYA KAZI KWA WATU WANAOFANYA KAZI.......
Fanya kazi acha uduwanzi.
 
Hali ni mbaya jamani member mwenzenu naomba msaada wenu
Elimu yangu ni kidato cha nne
Sina muelekeo wa maisha yani asubuhi naamka kama mbuzi,natamani sana navyoona watu wanaamka wanaelekea kwenye majukumu mbalimbali..

Yeyote mwenye kibarau naomba
Yeyote mwenye ushauri naomba
Yeyote mwenye mchango iwe mtaji naomba

Naweza kufanya kazi mkoa wowote
Naweza kujifunza jambo jipya kwa haraka sana
HAPO KWENYE RANGI NYEKUNDU UMENISTAAJABISHA SANA NA NIMEKASIRIKA SANA BAADA YA KUSTAAJABU.
 
Asante sana kwa ushauri,natamani sana ningepata elimu ya ufundi tatizo pesa,na hata ndugu wa kunisaidia sina
KIJANA CHACHARIKA.... usitegemee sana elimu na kusaidiwa kijana..... NAONA UNAJIITA KAMWENE LABDA NI MZALIWA WA IRINGA...... mimi kwetu moshi lakini huko iringa nimenunua mashamba na kupanda miti mafinga huko tena yanauzwa bei ya biskuti........ HUKO IRINGA NA NJOMBE UNAFANYA KAZI UNAPATA HELA NA KAMA NI KWENU HUKO MASHAMBA UNAPATA BURE NA UNAWEKA MITI....

jaribu kwanza kuacha akili za kipuuzi kudhani elimu na ndugu vitakusaidia maana lazima UFE MASIKINI NA HAKIKA UTAKUFA MASIKINI.... fanya kazi utafanikiwa. AU KAA UIMBE MUZIKI UWE KAMA CHIDI BENZI,TID,NA HATA NGWEA NA LANGA KILEO.
 
Utakubali kuuza bites? Yaani mi na tengeneza bites tambi, crips, vileja etc then unauza... Ila sijajua unakaa wapi,
Kama upo mkoani ebu jaribu hii biashara mtaji anza hata na elfu kumi huo ndio ushauri wangu
 
Tafuta kikundi chochote hapo ulipo kama ni cha vijana wenzako boda boda au bajaji wakufundishe kidogo halafu utapata mchongo Wa kuendesha boda au bajaji ...unachokipata wekeza kama mtaji Wa biashara nyingine ya kufanya kama ni kibanda cha chips au mgahawa italipa.
Pia uwe na malengo ya muda mfupi na muda mrefu usifanye kazi tu ili mradi mkono unaingia kinywani .wek a pesa kwa ajili ya kufanya kitu Fulani pia usiache kufanya kazi za deiwaka kama utazipata hizi pia zinaboost kipato. Kwa hali uliyofikia miaka 26 aisee jitoe aibu na usharobaro ishi kama vile unadaiwa million nyingi tu mwarabu alieshikiria uhai wako
UKUMBUKE KUNA VIJANA AMBAO NI KAMA WADOGO ZAKO WANAMILIKI VITU VIKUBWA TU SO UKIJIFANYA TOZI ...!!!
ALL THE BEST.
 
Hapo ulipo unamiliki utajiri mkubwa sana kupita vitu vyote duniani.
AFYA YA MWILI PAMOJA NA AFYA YA AKILI.
Vitumie vizuri nishukuru mwakani
 
Anza na umachinga mkuu nunua gazeti jumla na mifuko unakuwa unawasambazia wamama wauza maandazi asubuhi mbona unatoboa 20k pa day haukosi mfano mimi natafuta sana mtu anayeuza magazeti aniconnect kwa sasa ni dili
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom