Msaada infinix hot 6

Msaada infinix hot 6

albab

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2018
Posts
2,000
Reaction score
3,395
Hodi, heshima yenu wakuu..
Natumia infinix hot 6, betrii 4000 MAH

TATIZO.
Kwa wiki tatu sasa simu yangu imekua na tatizo la kuchaji mwanzo ilikua iko faster sana kwenye kuchaji lisaa limoja ilikua imejaa ila kwa sasa.

1. Inaweza kuchaji faster kama kawaida yake
2. Inawe kutumia masaa 8 kupeleka 4% tu
3. Inaeza isichaji kabisaa hata kwa masaa 24.

KUTATUA TATIZO.
Nilibadili chaji

Nkaipeleka kwa fundi baada ya kugoma kuchaji kwa siku mbili ilipo fika kwa fundi ikachaji kama kawaida nkarudi nayo hom

Ikachaji kwa siku mbili ikagoma tena kabisaa nkarudi kwa fundi akabadili system chaji.....

Now inapeleka moto ilaaa si kwa spidi ya mwanzo kwa sasa inaweza kupeka asilimia 10 kwa lisaa limoja so inahitaji masaa 10 kujaa tena ikiwa imezimwa ikiwa on unaweza kukesha .

MSAAA WENU.
Naomba kufahamu tatizo ni nini ili nkienda kwa fundi niwe specific.
 
Mafundi hardware huwa tunakuwa na Fast charger maalum kwa ajili ya kujaribishia simu zenye tatizo kama hilo

Nenda kwa fundi aliyekaribu nawe mwelezee hilo tatizo ataangalia namna ya kulitatua
 
Ahsante broo ngoja ntamcheki japo fundi wa kwanza ni kama kafeli mana tatizo lipo palepale na nimebadili chaji mbili yangu wakichajia wao iko fresh ila zao kwangu zinagoma ( chaji za aina kama yangu ya simu)
 
Ungeanza kwa kutujulisha kuwa hiyo simu yako ni mpya kwa maana ulii'unbox mwenyewe, au umenunua mkononi mwa mtu......?!

Kama ni mpya then itakuwa na warranty pamoja na guarantee kwa hizo wiki tatu ulizotumia utaweza irudisha dukani na kubadilishiwa.

Ila kama ni ya kununua mikononi kwa mtu then hapo umeingia choo cha kike......muuzaji kakurithisha matatizo ambayo yatakugharimu pesa ya kutengeneza mara kwa mara. Maana hizo sim bana, shikisha anza kufeli ndio basi tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nasikia case nyingi za infinix tatizo ni chaji either system charge au battery...kama unajiweza bora ubadili tu aina ya simu.

Sent using Samsung Galaxy
 
Ahsante broo ngoja ntamcheki japo fundi wa kwanza ni kama kafeli mana tatizo lipo palepale na nimebadili chaji mbili yangu wakichajia wao iko fresh ila zao kwangu zinagoma ( chaji za aina kama yangu ya simu)
Kuna OG Samsung fast charger pia kuna fake, kwa uhakika zaidi nenda Samsung Shop utajaribisha hapo hapo ukiona inaingiza kwa wakati unailipia ( kawaida dakika moja inajaza asilimia mbili hivyo dakika therathini asilimia sitini )
 
Ungeanza kwa kutujulisha kuwa hiyo simu yako ni mpya kwa maana ulii'unbox mwenyewe, au umenunua mkononi mwa mtu......?!

Kama ni mpya then itakuwa na warranty pamoja na guarantee kwa hizo wiki tatu ulizotumia utaweza irudisha dukani na kubadilishiwa.

Ila kama ni ya kununua mikononi kwa mtu then hapo umeingia choo cha kike......muuzaji kakurithisha matatizo ambayo yatakugharimu pesa ya kutengeneza mara kwa mara. Maana hizo sim bana, shikisha anza kufeli ndio basi tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawabadilishi simu kirahisi hivyo kama unavyodhani

Ataambiwa aiache kwanza wamtengenezee kwa gharama zao (bure) ikishindikana ndo watambadilishia
 
Jaribu kutumia fast charger original, pia hakikisha USB cable unayoitumia ni ya fast charge.
IMG-20190219-WA0004.jpeg
 
Ntafanyia kazi ushauri wenu ahsanteni sanaa
 
Kuna OG Samsung fast charger pia kuna fake, kwa uhakika zaidi nenda Samsung Shop utajaribisha hapo hapo ukiona inaingiza kwa wakati unailipia ( kawaida dakika moja inajaza asilimia mbili hivyo dakika therathini asilimia sitini )
Mkuu hapo hapo Kwa Samsung Nina swali............ Ukichaji simu ya Samsung Kwa kutumia Fake Charger inaweza kusababisha Simu kuishiwa chaji mara Kwa mara.
 
Fake huwa hazijazi vizuri pia unaweza kuua betri ya simu ndo maana kuna baadhi ya simu wamekuandikia, " pls use original samsung charger only"
 
Hodi, heshima yenu wakuu..
Natumia infinix hot 6, betrii 4000 MAH

TATIZO.
Kwa wiki tatu sasa simu yangu imekua na tatizo la kuchaji mwanzo ilikua iko faster sana kwenye kuchaji lisaa limoja ilikua imejaa ila kwa sasa.

1. Inaweza kuchaji faster kama kawaida yake
2. Inawe kutumia masaa 8 kupeleka 4% tu
3. Inaeza isichaji kabisaa hata kwa masaa 24.

KUTATUA TATIZO.
Nilibadili chaji

Nkaipeleka kwa fundi baada ya kugoma kuchaji kwa siku mbili ilipo fika kwa fundi ikachaji kama kawaida nkarudi nayo hom

Ikachaji kwa siku mbili ikagoma tena kabisaa nkarudi kwa fundi akabadili system chaji.....

Now inapeleka moto ilaaa si kwa spidi ya mwanzo kwa sasa inaweza kupeka asilimia 10 kwa lisaa limoja so inahitaji masaa 10 kujaa tena ikiwa imezimwa ikiwa on unaweza kukesha .

MSAAA WENU.
Naomba kufahamu tatizo ni nini ili nkienda kwa fundi niwe specific.
salaams ,
naomba msaada , nilipata system update na nika update but not its says YOUR DEVICE FAILED VERIFICATION na inaji reboot every 5 seconds nifanye nini mpaka simu irudi kwenye working condion/
 
Kuna kitu hapo cha kuangalia nacho ni "Amps(A)" ambayo ni uwezo wa chaja unayotumia. Uwezo wachaja unaisoma kwenye maandishi yalio kwenye chaja ambayo "output_ mps"ndio kitu cha kuzingatia.
Kama amps ni ndogo itachelewa kujaza au isijaze kabisa wala kupunguza. Pia ikiwa nyingi itajaa haraka ila utakuwa unapunguza maisha ya betri...
Hapo ni bora ujue cm yako inatumia chaja ya Amps ngapi ndio chaja itakayo kufaa pengine.
 
Hapo wala haikuwepo haja ya kubandua charging system. Hapo issue ni meno ya sehemu ya kuingizia charger ndiyo yamesagika kwahiyo ilitakiwa kuchomelea na siyo kubadili charging system ndiyo maana tatizo limeendelea kukusumbua.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom