Msaada: Idadi ya Wajumbe wa NEC ya CCM na majina yao

Msaada: Idadi ya Wajumbe wa NEC ya CCM na majina yao

Labda kwa kukuraisishia tu ni kwamba jumla kuna wajumbe 360 na kati ya hao Lowassa anaungwa mkono na wajumbe 286....

Mkuu asante kwa takwimu, tafadhali hebu tueleze kuhusu kamati kuu pia ina wajumbe wangapi na wanaomuunga mkono EL ni wangapi? Nadhani huko ndiko ambako hali sio nzuri kiasi..
 
Mkuu asante kwa takwimu, tafadhali hebu tueleze kuhusu kamati kuu pia ina wajumbe wangapi na wanaomuunga mkono EL ni wangapi? Nadhani huko ndiko ambako hali sio nzuri kiasi..

hilo ndilo la Muimu zaidi.
 
Nguvu ya Lowassa ni nchi nzima.... Hiyo idadi niliyokupa ndio real na ipo katika data base.... Kuna wengine kama 12 wanatarajiwa kuungana na kambi ya ushindi mwezi wa 3 katikati....
unamoyo kweli. ila jiandae kasaikolojia. maana..........
 
Muda uende ili tukate vilimilimi vya watu humu lo!. Mara sijui nani mara vile aaaargh!
 
Ninachokielewa, Mtihani mkubwa wa Lowassa kupitishwa kama mgombea wa kiti cha Urais kwa tiketi ya ccm ipo CC (kamati kuuw) ya ccm ambayo wajumbe wengi hawamuungi mkono ikiwa ni pamoja na Nape,Kinana,Kikwete ambao kwa ushawishi wa kiccm hao ndio waweza sema kama wananguvu ya kumpitisha Mgombea yeyote.

Kumbuka kauli ya Kinana aliposema "Hatakama kura zao (Kina Lowassa) zitakuwa nyingi mpaka kufika mbinguni tutakata jina lake" ( Usiniulize alitolea wapi kauli hiyo) Huo ndo msaada pekee naoweza kukupa.

Nb, Kuparurana kwa ccm kwa maslahi ya UKAWA kudumu...!!!!!!

BACK TANGANYIKA

Na hiyo Kauli kama ni kweli na EDO akawa pale magogoni jamaa lazima atakuwa mkimbizi maeneo ya Nairobi.
 
Lawassa namfahamu sana, alikuibia watanzania kupitia kampuni feki ya RICHIMONDI so ajiandae kujibu jukwaani. Mwaka huu kutakuwa na mdahalo so tutataka ajieleze maana hatutakubali kuuziwa mbuzi kwenye gunia kama 2005
 
Kama mna ushaidi nendeni mahakamani,Lowassa kawashika tako gambaz
 
Hata mimi nipo hapo. tutamchagua Lowasa kwa kishindo
 
Watu 8 Kila wilaya! Kuna wilaya 136 hivi! Kundi la Zbar!!!Na kundi la kifo
 
"Lowassa ukitaka kuwa mrithi wa Jk kwa hali halisi na kwa jinsi ccm ilivyochokwa igizeni kukinzana..igizeni kuwa hauelewani na baadhi ya viongozi wa ccm..kinzana nao..watanzania walioichoka ccm watakuona wewe ndo mkombozi wao..utapata huruma ya watanzania"
 
Wajumbe wa NEC hawahongeki

Sikweli kabisa. Wabunge wa NEC ndani ya CCM wanahongeka tena kirahisi kabisa. Kwa mfano mwaka 2005 kulikuwa na mashindano ya wagombea wa urais wa CCM Kuhonga wajumbe wa NEC, na mtandao wa Kikwete ndio ulikuwa kinara.
Hata sasa viongozi wakuu wa CCM(Kikwete,Kinana, Mangula, Nape) wanalia wakisema wagombea urais wa CCM wako busy kuhonga wajumbe wa NEC.
 
Back
Top Bottom