Naomba nikupinge mkuu.
Inategemea na aina ya matumizi ya PC yako, kumbuka kuna PC za light users, medium users na heavy users.
Light users ni kwa ajili ya kuandika documents na kuangalia muvi kwa muda mfupi tofauti na medium user ambae anaangalia muvi na kucheza game kidogo.
Heavy user ni yule anaeweza kutumia PC kwa shughuli nyingi bila kuchemka.
Mimi natumia HP 602 toka 2012 na inapiga mzigo fresh sana. Ila kuna mshikaji wangu anatumia HP ila nimeisahau model akitumia kuangalia muvi kidogo tu inachemka balaa wakati yake ni mpya hata mwaka haijamaliza.
Tunacheza game moja ila yake inachemka yangu inakuwa poa.
Nikaja kugundua baada ya kusearch mtandaoni solution, ya kwake ni kwa ajili ya matumizi madogomadogo ila yangu ni heavy user.