Msaada; Hii Number Plate imekaaje Wadau

Shark

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Posts
29,991
Reaction score
30,188
Wadau,

Navyofahamu Number Plate nyeupe ni kwa ajili ya magari ya Kibiashara, na ikianza na SU maana yake Gari husika linamilikiwa na Shirika la Umma.

Sasa Plate inapokua nyeupe halafu number/herufi zinaanzia na SU hapo kidogo nakua sielewi wadau, msaada tutani kwenye hili!!
Tuseme hii gari inakodishwa, ama??
 
ni ya serikali ila iko chini ya mradi flani aidha unafadhiliwa na serikali au kutoka nchi za nje
 
Labda ya Uganda au Sudan, maana hapa kwetu ingemaanisha SHIRIKA LA UMMA lkn kwenye white plate sio sahihi kwani white background ni kwa ajili ya abiria.
 
Siyo ya Sudani wala nini. Hiyo ni gari ya Steven Ulimboka (SU). Hizo ndiyo zile namba binafsi za m 5
 
Registration Number

Registration number ni zile herufi na tarakimu zinazomaanisha nambari za usajili wa gari na hata ikiandikwa ukutani, kwenye karatasi, kiganjani itaitwa registration number lakini ikiwa registration number imeandikwa kwenye kibao chake maalum kinachofungwa mbele na nyuma ya gari huitwa number plates au registration plates.
 
Yawezekana ni utaratibu mpya umeanza!
 
Shirika uma limejiongeza, limeweka kijiko. Liko kibiashara zaidi.
 
Hiyo haiwezi kuwa Sudan maana hiyo miti na greenish background huwezi kuipata Sudan.. kwani UDA number plate zake ni nyeupe au yellow..
 
Number plate ya njano ni kwa magari yote yasiyo ya kubeba abiria na number plate nyeupe ni kwa magari ya kubeba abiria kwa maana kuwa ni public service vehicles. Kwa kawaida magari yenye ante ya SU mengi yana plate ya njano . Ni magari machache sana yenye plate nyeupe kama ya TANAPA ambayo hubeba abiria au kukodishwa n.k.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…