Msaada hauna risiti

Kanungila Karim

Verified Member
Apr 29, 2016
17,216
2,000
couple-shoot-mallorca-32.jpg
Shoga wakati mwingine huwa naongea sana hadi koo lanikauka, naomba kwa leo niishie hapa! Kwa wewe ambaye upo kwenye uhusiano nikutakie Valentine’s Day njema! Kaa na mchumba…


WEREEE reeee kama hujapendwa mwaka huu basi subiri huenda mwakani ikawa bahati yako! Wanakwambia heri kulala juu ya dari kuliko kuishi na mwanaume mgomvi, upo?


Waringia mguu wa bia unasahau kama wa soda nao ni mguu, hee eheeeeiyaaa! Shoga wakati mwingine ni bora ule mboga za majani kuliko nyama iliyokolea chumvi! Nashanga kubwa zima unauliza vumbi stoo!

Tena shoga usinione nacheka ukajua leo Anti Naa amekuja na vitu vizuri, tusikaushane uzazi ati! Mume wako mlioana kwa raha na shida leo hii unakuja kunililia inahu?


Leo mwenzako nipo na waleeee kina mama, kina dada tena nawakumbusha maana hii mada nilishawahi kuigusia lakini kwa kuwa kesho ni sikukuu ya wapendanao acha niwape vichambo mchambike, haloooo eeeeeh! Kutapika atapike mgonjwa akitapika mlevi ujue kalewa huyooo!

Hakuna kitu kinanikaa kwenye koo kama kumuona mwanamke mwenzangu akikimbilia ofa za bure, najua hili hata wewe litakugusa tena sana tu! Wanaume wakati mwingine sijui wamerogwa na nani! Ikifika kipindi cha sikukuu kama hizi za wapendanao ndiyo huwa mstari wa mbele katika kubomoa ndoa za wenzao na wakati mwingine kumharibia mwanamke ‘future’, mtanisamehe nimeongea na Kizungu.


Siku ya Wapendanao wao huona ndiyo sehemu ya kutoka na mwanamke kwenda kupata dina na hukohuko anahakikisha anakupa vibia kadhaa hadi ulainike akuingize gesti! Shuuuutuuuu!

Tena wengine watakuja na vizawadi vya uongo na kweli ili mradi mwanamke aingie kwenye mtego wake na hivi wengi wetu hatujielewi tunajikuta tukiingia mkumbo, leo anakuchezea kesho huyo anakutema!


Shoga nikisemaga huwa namaanisha ati! Kwa uzoefu wangu ikifika kipindi hichi cha wapendanao huwa napata malalamiko mengi kutoka kwa wanawake, wengine ooh nilimuomba lifti nikampa na namba yangu ya simu, baada ya kunichezea nimejua kuwa ana mke na watoto juu!

Kama ulikuwa hujui jua sasa, shoga msaada hauna risiti! Umefika wakati wa kujanjaruka ati! Akikuomba namba za simu mpe hata za gari au mpe za hausigeli wako kwa kumkomoa kwani amelazimishwa kukupa lifti? Amelazimishwa kukupa zawadi au ndiyo akikutoa ‘auti’ mpaka akuleweshe na kukupeleka kitandani?

Shoga wakati mwingine huwa naongea sana hadi koo lanikauka, naomba kwa leo niishie hapa! Kwa wewe ambaye upo kwenye uhusiano nikutakie Valentine’s Day njema! Kaa na mchumba/mumeo umweleze mipango yenu mbele kiuchumi na hata uzazi wa mpango siyo umekalia ngono tu! Shuuuutuuu!
 

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,756
2,000
Hata vote 20 haina risti ndiyo maana wanaiba kodi zetu kupitia matumizi ya usalama wa taifa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom