Zeddicus Zu'l Zorander
JF-Expert Member
- Aug 25, 2011
- 797
- 929
Mke wangu alichukua mkopo crdb bank mwaka 2014 mwezi 11,ambao anatakiwa kukatwa mpaka mwezi wa 11 2019.
Kuna siku niliskia analalamika kwamba kuna wakati bank wanakata hela lakin salary slip haionyeshi,nikanusa hali ya hatari, tukapiga toka aanze kukatwa mpaka leo tukapata jumla.
Baada ya hapo nikamwambia aende benki aulize bado anadaiwa kiasi gani, juzi kaenda benki lakini loan officer kampa majibu ya kumchanganya zaidi, na alikuwa kama ana wasiwasi,anamuuliza kwani ulirenew mkopo lini?
Wakat hajawahi kurenew.Mara anamwambwia siku hizi hazina wanakata hela ukouko alafu ndio wanatuma benki.
Mwisho akaprinti fomu imeandikwa loan enquiry...
Naomba ufafanunuzi wa sentensi hizi
1.Principal amount
2.Total facility(kuna kiasi mbele yake)
3.first drawdown date
4.Final maturity date
Pia naomba ushauri atau gani tuchukue sababu loan officer anaonesha kama kuna kitu anaficha.
Mkuu sijui kama umeelewa,deni linalipwa, kinachotokea ni kwamba fedha inakatwa lakin salary slip haionyeshi kama imekatwa, na ndio hapo shida inapoanzia.Kukopa harusi, kulipa matanga, "mwambie dawa ya deni ni kulipa tu"
Loan officer hakukopeshi unakopeshwa na bank "crdb plc"
Huyo officer awepo asiwepo mtadaiwa deni hadi mlipe lote.
Kopi ya kitu gani unataka niweke?Sema alikopa sh.ngapi na weka copy siyo maneno Tu hatukuelewi
Kwani we hii taarifa umeitoa wapi?Kwani huyo mkeo alichukua fedha za kigeni hata useme hakuna mtu aliyewahi kukopa fedha za aina hiyo?
Kwani we hii taarifa umeitoa wapi?
Haaaahh haya mzee.Mkuu;
Nimeipata humu humu JF kwamba mkeo kakopa na mna hofu kuliwa zaidi
Mkuu sijui kama umeelewa,deni linalipwa, kinachotokea ni kwamba fedha inakatwa lakin salary slip haionyeshi kama imekatwa, na ndio hapo shida inapoanzia.
Thanks, ila nadhani kuna shida mahali flani, maana kuna baadhi ya slip zinaonesha nyingingine hazioneshi.Kwa kawaida, mwajiri anakuwa "garanter" -mdhamini wa mkopp. Na anacho wa gurantee bank ni kuwa salary ya mkopaji atatumbukiza kwa bank anakodaiwa, mwajiriwa.
Salary ikingia kwa account bank wanachukua chao .
Hakati mwajiri mshahara wa mdaiwa kwenda kulipa bank, hence ndio maana haionyeshi kwa salary slip
Kweli kuna usanii sana, walimwambia riba ya chini( kati ya 20-30) hakumbuki, akakopa 15,000,000 atalipa 22,000,000.Kimsingi sio wakweli.mikopo ya bank za bongo ni majanga.
bank zinafaidika mara mbili ya unavyofaidika mkopaji...
riba wanaongeza anytime
Thanks, itabidi akaombe bank statement,kama watakuwa wanatoa mpaka ya miaka 2 itakuwa vizuri.Kama benk wanakata na salary slip haionyeshi labda tatizo la muajiri huko upande wa hizo salary slip... dawa ni kucalculate jumla ya pesa mlizolipa ambazo hazikuonyeshwa. Kuwa na copy ya bank statement na kuwasiliana na muajiri na benki ili kufanya reconciliation ya hiko deni...