Msaada: Gari yangu inameza oil

Abramovic

JF-Expert Member
Sep 6, 2013
324
597
Habari ya jioni wanabodi? Ni matumaini yangu nyote mu wazima wa afya njema.

Naombeni msaada, tatizo langu gari yangu inameza oil isivyo kawaida.

Yani kwa mfano nimeweka oil jumanne ya wiki iliyopita, lakini leo taa ya oil inawaka nikiangalia stick ya Oil inaonyesha engine haina oil kabisa. Hii ni mara ya tatu hali hii inajitokeza.

Kuhusu hali ya gari, gari bado mpya kabisa maana niliinunua mwaka jana February ni namba DJW, Oil nayotumia ni Castrol GTX 20W-50. Gari yangu ni kwa matumizi binafsi tu sio biashara, yani kwenda ofisini na kurudi na mizunguko ya kawaida ya mjini.

Nilijaribu kuwasiliana na mafundi kadhaa, fundi mmoja alinishauri kubadilisha mswaki (nusu engine), mwingine akashauri kufanya overwhole service ili kutatua tatizo. Sasa hivyo vyote ni gharama kubwa kiasi kwamba naona bado mapema sana kwa gari kama hii kufanyiwa service ya hivyo.

NB: Gari natumia mwenyewe sichangii na mtu pia wakati wa kubadilisha Oil hua nakuwepo nashuhudia fundi akibadilisha. Aina ya gari ni Toyota IST 2005

Tafadhari naombeni msaada wadau nini cha kufanya, niwaombe radhi kwa maelezo marefu.
Natanguliza Shukrani.
 
Omba Mods waihamishie jukwaa la ..JF Garage (Magari na Vyombo vya Usafiri) huku sio mahala pake mkuu.
 
Habari ya jioni wanabodi? Ni matumaini yangu nyote mu wazima wa afya njema.

Naombeni msaada, tatizo langu gari yangu inameza oil isivyo kawaida. Yani kwa mfano nimeweka oil Jnne ya wiki iliyopita, lakini leo taa ya oil inawaka nikiangalia stick ya Oil inaonyesha engine haina oil kabisa. Hii ni mara ya tatu hali hii inajitokeza.

Kuhusu hali ya gari, gari bado mpya kabisa maana niliinunua mwaka jana February ni namba DJW, Oil nayotumia ni Castrol GTX 20W-50. Gari yangu ni kwa matumizi binafsi tu sio biashara, yani kwenda ofisini na kurudi na mizunguko ya kawaida ya mjini.

Nilijaribu kuwasiliana na mafundi kadhaa, fundi mmoja alinishauri kubadilisha mswaki (nusu engine), mwingine akashauri kufanya overwhole service ili kutatua tatizo. Sasa hivyo vyote ni gharama kubwa kiasi kwamba naona bado mapema sana kwa gari kama hii kufanyiwa service ya hivyo.

NB : Gari natumia mwenyewe sichangii na mtu pia wakati wa kubadilisha Oil hua nakuwepo nashuhudia fundi akibadilisha. Aina ya gari ni Toyota IST 2005

Tafadhari naombeni msaada wadau nini cha kufanya, niwaombe radhi kwa maelezo marefu.
Natanguliza Shukrani.

Kuvuja oil kunahusianaje na umeme wa gari?
 
Pole sana kiongozi...
Gari kula oil inachangiwa na mambo makuu mawili.
1-Oil ina penya kwenye piston rings.
2-Kuna leakage kwenye valve seals.

Mengine ya kawaida angalia oil filter kama ipo vizuri imelegea au imekwisha muda wake.
Ni lini mara ya mwisho umefanya service!!!

Pia inawezekana sump ina shida either ina tundu mahala linalo pelekea oil Kupotea.

Wahi gereji utakaanga engine hiyo.

NB
Hiyo gari sio mpya imeisha tumika, inawezekana kabisa vipuli hasa nilivyo taja vimechoka.

All the best.
 
Pole Sana Kiongozi
Naamini Shida Yako Inaweza Kupata Ufumbuzi Haraka Sana Kubwa Waone Mafundi Pia Uwe Mtulivu Yaani Mpelekee Fundi Afanye Ukaguzi Kupitia Dondoo Unazopata Hapa Jamiiforums
 
Kuhusu hali ya gari, gari
bado mpya kabisa maana
niliinunua mwaka jana
February ni namba DJW, Oil
nayotumia ni Castrol GTX

gari mpya kivp ?? 0km ilikuwa au ni ugeni wake kwa hapa bongo??
 
Hiyo gari sio mpya ni used. Ungewtuwekea imetembea kilomita ngapi sio namba za gari. Mie nina gari imetembea kilomita laki mbili na kadhaa nchi za wenyewe ila kwa bongo ina namba DMD
 
Habari ya jioni wanabodi? Ni matumaini yangu nyote mu wazima wa afya njema.

Naombeni msaada, tatizo langu gari yangu inameza oil isivyo kawaida.

Yani kwa mfano nimeweka oil jumanne ya wiki iliyopita, lakini leo taa ya oil inawaka nikiangalia stick ya Oil inaonyesha engine haina oil kabisa. Hii ni mara ya tatu hali hii inajitokeza.

Kuhusu hali ya gari, gari bado mpya kabisa maana niliinunua mwaka jana February ni namba DJW, Oil nayotumia ni Castrol GTX 20W-50. Gari yangu ni kwa matumizi binafsi tu sio biashara, yani kwenda ofisini na kurudi na mizunguko ya kawaida ya mjini.

Nilijaribu kuwasiliana na mafundi kadhaa, fundi mmoja alinishauri kubadilisha mswaki (nusu engine), mwingine akashauri kufanya overwhole service ili kutatua tatizo. Sasa hivyo vyote ni gharama kubwa kiasi kwamba naona bado mapema sana kwa gari kama hii kufanyiwa service ya hivyo.

NB: Gari natumia mwenyewe sichangii na mtu pia wakati wa kubadilisha Oil hua nakuwepo nashuhudia fundi akibadilisha. Aina ya gari ni Toyota IST 2005

Tafadhari naombeni msaada wadau nini cha kufanya, niwaombe radhi kwa maelezo marefu.
Natanguliza Shukrani.
IST 2005 Afu unatuaminisha ni gari jipya?
 
Yangu ilianza kupoteza oil kidogo kidogo. Baada ya mwaka, ika fail kabisa ikawa inatoa moshi mweupe. Ilibidi kufanya overhaul. Hiyo oil 20w-50 si sahihi kwa hiyo injini, ni ni nzito sana. Tumia 5w-30 au 10w-30, ndio specifications sahihi za hiyo injini.
 
washa gari yako, wacha ipate moto kidogo, fundu dip stick ukiona inatoa mvuke kabisa uwe unauona kwa macho sio kuweka mkono, ujue hio engine inaunguza oil. apo lazima ifunguliwe ndani itizamwe tu. na ikifunguliwa hakuna dogo tena mkuu. hio namba kuwa DJW isikushughulishe kabisa. Nawaambia kila siku, uzima na upya wa gari ni mashine sio namba za usajili!
 
Yangu ilianza kupoteza oil kidogo kidogo. Baada ya mwaka, ika fail kabisa ikawa inatoa moshi mweupe. Ilibidi kufanya overhaul. Hiyo oil 20w-50 si sahihi kwa hiyo injini, ni ni nzito sana. Tumia 5w-30 au 10w-30, ndio specifications sahihi za hiyo injini.
Sijaelwa mkuu, mimi nimekuwa natumia 20w-50 mara zote...gari ni IST.
 
Back
Top Bottom