Msaada: Galaxy S5 Original Tumebadilishiwa na Fake...!

Msaada: Galaxy S5 Original Tumebadilishiwa na Fake...!

KIOO

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2013
Posts
6,249
Reaction score
5,933
Habari zenu wakuu.

Hope mko salama kabisa, kuna mjanja mmoja kamuingiza mjini Bi Mkubwa wadau na ilikuwa kama ifuatavyo.

Bi Mkubwa alinunua Original Galaxy S5 akiwa MAKKAH na kurudi nayo ikiwa okay kabisa, sasa ilimshinda kufanya configuration na vitu kama playstore, whatsapp ikawa hapati and so on.

Akatokea mjanja mmoja ni katika ndugu yetu pia na kumwambia hii inabidi iflashiwe iweze kutumia net za mitandao ya hapa Tanzania ndo utaweza kutumia whatsapp n.k

Jamaa akapewa simu kwenda kui-flash kumbe akaenda kubadilisha kwa clone akamletea fake S5 na box lile lile na back cover ileile na kumpa sound kuwa fundi wake hayupo atam-check siku nyingine.

Bi Mkubwa ikabidi aitulize tu ndani coz alikuwa anatumia simu nyingine, zikapita siku kadhaa akaamua aende kwa mawakala wa samsung kuirekebisha, jamaa kui-check tu wakamwambia hii mbona sio original mama sisi tunatengeneza original tu.

Akaamua arudi home aiweke ndani tu, hivi jana nimeichukua kuiangalia wakuu dah, nimeiwasha tu nakutana na MEDIATEK ndio welcome note halaf ikaja android nikasema hapa kumebaki manyoya tu ndege keshaliwa.

Mbaya zaidi internet iko EDGE peke yake, nimejaribu kufanya configuration settings lakini wapi na cha ajabu kila nikiweka WCDMA inakataa na inarudi kwenye GSM only.

Nimejaribu ku-check kwenye settings labda nifanye factory reset hakuna hiyo option ya factory reset. Nikasema nifanye hard reset wakuu nikakutana na maandishi ya kichina tupu nikawa sina jinsi wadau ni MEDIATEK.

Naombeni msaada tu atleast ikae kwenye WCDMA/3G tu na kama ntaweza kubadili hiyo mediatek firmware au hayo maandishi ya kichina au whatever wakuu mi sio mtaalam kihivyo naombeni msaada nianzie wapi niweze kupata net au kuiflash tuone kama itakubali internet wakuu. Messages and calls zinakubali kama kawaida ila net wakuu hamna page inayofunguka wadau.

Natanguliza shukran wakuu.

THANKS A LOT.
 
Naombeni msaada tu atleast ikae kwenye WCDMA/3G
Tanzania tunatumia GSM tech mitandao yote with the negligible exception of TTCL.

Sasa wewe kwa nini unataka kutumia CDMA?

Kwa saab hakuna mtu anaethamini utu wake bado yuko TTCL, kampuni bankrupt la serikali.
 
1. Huwezi kubadili mediatek maana Ni hardware hivyo itabaki hivyo hivyo.

2. Hayo maandishi ya kichina kwenye recovery unaweza kuyatoa kwa kuroot simu na kuweka recovery nyengine ya kingereza ILA sikushauri kabisa maana wachina hawaeleweki simu inaweza kuwa mbaya zaidi uki hard reset.

3. Download CPU-Z toka play store au kwenye site Yao then fungua itakutajia Ni aina gani ya processor (soc) ya mediatek iliotumika then ilete hapa jukwaani tutajua kama inakibali 3g au haikubali.

Itakuwa mfano kama huu MT6570
 
Wcdma Ni part ya GSM, kuna utofauti Kati ya cdma na wcdma
 
nenda play store download mtk engeneering then ingia option ya mediatek then nenda network selection weka iwe wcdma au 3g only, ushauri wa kupata hio og yenu mwambie huyo ndugu arudishe simu yenye imei(*#06#) sawa na zile zilizoandikwa kwenye box/risiti
 
Tandika makofi huyo ndugu yenu arudishe haraka hiyo simu.hakuna kuangahika
 
Aisee watu wabaya sana duuh ndugu kwa ndugu mnachakachuana aisee pole mkuu anunue tu nyengine
 
Sasa jamaa,kwani huyo ndugu yenu kahama nchi???,kwanini usimfuate umtoe kamasi arudishe simu ya maza!!!
 
We mleta mada labda nikuite "Boya" Kabisa...
Reason: Ulivyoandika hii mada yako naweza kukuita ni "advance user" wa hizi simu. Kwanini ulishindwa kumsaidia mama yako just kuinstall whatsapp na internet ambayo hata "mtoto mdogo" anaweza kufanya, mpaka ukaruhusu ulaghai wa huyo ndugu yako?...Shame on You "Hapa Kazi tu"
 
Right on point.
Mleta mada ni mjinga sana.
Hiyo kazi alitakiwa aifanye yeye.
 
Haina haja ya kuangaika,nenda kariakoo kanunue techno m3 mpe bimkubwa maisha yaendelee
 
Duuhhh sasa simu mmeshajua mmebadirishiwa, bado mnaangaika na hiyo clone ya nini, fanya mchakato original phone irudi
 
Tanzania tunatumia GSM tech mitandao yote with the negligible exception of TTCL.

Sasa wewe kwa nini unataka kutumia CDMA?

Kwa saab hakuna mtu anaethamini utu wake bado yuko TTCL, kampuni bankrupt la serikali.

Ooh okay, ndo mana nikasema si mtaalam sana wa haya mambo that's why nikasema nionbe msaada kwenu wakuu.

Well, ninachomaanisha ni kwamba kwenye settings za network kuna options za kuweka either GSM au CDMA or both at once, na mara nyingi nikiweka hapo kwenye GSM huwa naona alama ya E zedge pale kwenye bar ya network kwa juu, ila nikiweka hiyo CDMA naona 3G au H+ and so on, ndio sababu ya kutaka kutumia hiyo CDMA nikiwa na maana hiyo mkuu ili kuondoa hiyo E coz haifungui hata page ya web yani net iko down kabisa ila kukiwa na 3G au H+ huwa inachukua sekunde tu kufungua ndio mana nikataka kuweka hiyo CDMA sjui ntakuwa nimekosea kiongozi, labda ungenielewesha juu ya hilo mkuu.

Natanguliza shukran.
 
1. Huwezi kubadili mediatek maana Ni hardware hivyo itabaki hivyo hivyo.

2. Hayo maandishi ya kichina kwenye recovery unaweza kuyatoa kwa kuroot simu na kuweka recovery nyengine ya kingereza ILA sikushauri kabisa maana wachina hawaeleweki simu inaweza kuwa mbaya zaidi uki hard reset.

3. Download CPU-Z toka play store au kwenye site Yao then fungua itakutajia Ni aina gani ya processor (soc) ya mediatek iliotumika then ilete hapa jukwaani tutajua kama inakibali 3g au haikubali.

Itakuwa mfano kama huu MT6570

Ooh okay, ngoja nifanye mkuu japo ni masaa mpaka iweze kufungua playstore kiongozi.

Ila ngoja nifanye mchakato huo then will give you feedback kiongozi.

Thanks a lot brother.
 
nenda play store download mtk engeneering then ingia option ya mediatek then nenda network selection weka iwe wcdma au 3g only, ushauri wa kupata hio og yenu mwambie huyo ndugu arudishe simu yenye imei(*#06#) sawa na zile zilizoandikwa kwenye box/risiti

Thanks a lot mkuu kwa ushauri ulio mzuri kabisa itanilazimu kuufanyia kazi mpaka pale ntakapofkia the will let you know kiongozi.

Thank you so much mkuu.
 
Sasa jamaa,kwani huyo ndugu yenu kahama nchi???,kwanini usimfuate umtoe kamasi arudishe simu ya maza!!!

Aisee watu wabaya sana duuh ndugu kwa ndugu mnachakachuana aisee pole mkuu anunue tu nyengine

Tandika makofi huyo ndugu yenu arudishe haraka hiyo simu.hakuna kuangahika

Tatizo jamaa hayupo dar kwa sasa ila muda wowote atakaporudi tutafanya kumuuliza tujue atatujibu nini wakuu na hatimaye tutazame uwezekano wa kuipata simu ambayo ameibadilisha wadau.

Nawashkuru kwa ushauri wenu.
 
We mleta mada labda nikuite "Boya" Kabisa...
Reason: Ulivyoandika hii mada yako naweza kukuita ni "advance user" wa hizi simu. Kwanini ulishindwa kumsaidia mama yako just kuinstall whatsapp na internet ambayo hata "mtoto mdogo" anaweza kufanya, mpaka ukaruhusu ulaghai wa huyo ndugu yako?...Shame on You "Hapa Kazi tu"

Right on point.
Mleta mada ni mjinga sana.
Hiyo kazi alitakiwa aifanye yeye.

Nashkuru kwa kauli zenu wakuu, ila labda mfaham kitu kimoja kuwa Bi Mkubwa yupo Upanga mi nipo Kinyerezi, na pili wakati amerudi hakuniambia suala hilo kuwa ana simu anataka kufanya configuration settings sidhani kama ningeweza kuota au sijui ningejuaje labda kama ingekuwa ni nyinyi. By the time jamaa anapewa simu mimi sina taarifa kama Bi Mkubwa alikuja na nini toka safari yake ilipaswa aniambie kuwa kuna kitu flani nahitaji kufanya jambo flani ili niweze kukitumia ila hakunijuza ingekuwa nyinyi mngefanyaje wakuu au mngejuaje labda...?.

Mi nimekuja kujua na kuiona simu juzi wakuu kosa langu liko wapi hapo ilhali sikuambiwa kuwa kuna simu inatakiwa kufanyiwa vitu kadha wa kadha wadau...?.

Ila najua binadam tunatofautiana kwa UTASHI na pia ningependa tu kuwashauri kuwa msipende kumnyooshea mtu kidole kimoja wakati kuna vidole vinne vinaangalia kwako, mngeuliza kwanza kabla ya kuanza kuongea kauli ambazo mmeziongea.

By the way, nawashkuru sana.
 
1. Huwezi kubadili mediatek maana Ni hardware hivyo itabaki hivyo hivyo.

2. Hayo maandishi ya kichina kwenye recovery unaweza kuyatoa kwa kuroot simu na kuweka recovery nyengine ya kingereza ILA sikushauri kabisa maana wachina hawaeleweki simu inaweza kuwa mbaya zaidi uki hard reset.

3. Download CPU-Z toka play store au kwenye site Yao then fungua itakutajia Ni aina gani ya processor (soc) ya mediatek iliotumika then ilete hapa jukwaani tutajua kama inakibali 3g au haikubali.

Itakuwa mfano kama huu MT6570

Mkuu hii simu net inagoma inaingia playstore ila ku-download kwake kiongozi ni kukesha, ila nimetumia es file explore kuituma kwa bluetooth hiyo CPU-Z na imeleta hizi info hapa chini mkuu...

Screenshot_2012-01-02-04-50-21.png
 
Hio soc Ina 3g hivyo simu yako pia inayo 3g jaribu ushauri WA shiny-c hapo juu kama utaweza kui enable
 
Back
Top Bottom