Msaada-files na folders sizion japo flash inaonekana imejaa

kvelia

JF-Expert Member
Jun 24, 2009
246
44
Wakuu naombeni msaada, nina flashi yangu ndani ina mambo mengi ila nikitaka kuyafungua hayaonekani ila yanaonekana ktk computer moja tu, nifanyeje ili niweze kuyaona (Hidden files and folders)
 
Dah, sina jibu kwani hata mm hili tatizo huwa naliface sana....Labda kama kuna mdau alishalipatia ufumbuzi atuelekeze..
 
Wakuu naombeni msaada, nina flashi yangu ndani ina mambo mengi ila nikitaka kuyafungua hayaonekani ila yanaonekana ktk computer moja tu, nifanyeje ili niweze kuyaona (Hidden files and folders)

Haya hii hapa solution!

Hili tatizo ni 'common' sana kwa computer hususan zile ambazo zinatumia Windows XP na Vista. Hao no virusi wameingia kwenye kompyuta mojawapo katika ulizoiweka hiyo flashi. Cha kufanya hapo ni rahisi. Kama kuna mtu anatumia Ubuntu ama Mac nenda kwenye kompyuta yake weka hiyo flashi yako itakuonesha hayo mafaili yote. namna nyingine rahisi ni kutumia hiki kidude unachoweza kudownload hapa USB Show - Download kinaitwa USB Show na ni kama KB 500 hivi kwa hiyo ni rahisi tu ku-download.

Ukishaidownload hiyo USB-Show iweke kwenye flash disk yako iliyoathirika kisha uki double click kikifunguka kitakupa dialogue ya ku-show files, chagua flash drive yako kwa hiyo dialogue kisha useme Show files. Yatarudi mafaili yote. Ni rahisi zaidi ya hivi nilivyoandika sema mimi sina namna ya kuandika kirahisi kama yenyewe ilivyo. Ichukue uone na usiisahau kuwaambia watu hapa kama imefaa ili waitumie siku nyingine.

Belle epoque connaisseur!
 
Wakuu naombeni msaada, nina flashi yangu ndani ina mambo mengi ila nikitaka kuyafungua hayaonekani ila yanaonekana ktk computer moja tu, nifanyeje ili niweze kuyaona (Hidden files and folders)

Okay fanya hivi.
>weka flash yako kwenye moja ya USB port,
>Angalia flash yako imepewa jina (drive) gani, kama ni G au H etc,
>kabla hujaifungua, bofya start , type cmd halafu bonyeza enter (kwa ufupi fungua command prompt)
>Angalia flash yako imepewa jina (drive) gani, kama ni G au H etc,
> Katika command, type jina la flash likifuatiwa na alama : bila kuacha nafasi,
mfano jina la flashi ni H, sasa andika H:
Kisha enter,
Baada ya hapo chapa herufi zifuatazo

attrib -s -h -r /s /d

Kisha bofya enter

Fungua flash yako na files zote zitakua zimerudi.
Exclusively 2zone computers support
2zone & company - Home
Kwa msaada zaidi pigia sisi
+255719792703
Ni tech kidogo tu ila kuna kampuni inachaji hadi laki nne kusolve kijitatizo hicho
Enjoy,
Ushauri, tumia antivirus inayoeleweka na uiupdate mara kwa mara
Mfano
2zone & company - Blog: Kaspersky Antivirus 2012
 
Wakuu nashukuruni sana kwani nimeyaona mafolder yote, atakaeandika attrib -s -h -r /s /d azingatie space. Sijafanikiwa kudownload hiyo software lakini nitafanya hivyo nione pia. Shukrani sana tena G-Thinkers.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom