Msaada & Elimu

gwahe

Senior Member
Joined
Nov 24, 2014
Posts
147
Reaction score
84
Heri ya mwaka 2015 wana MMU.

Naombeni ushauri na elimu...
Babu na bibi yangu!! Walinieleza na kunishauri. Kuwa kuna mambo muhimu, makubwa na kuzingatia wkt wa kuchagua mchumba. Wakanieleza kuwa upendo (Love) pekee siyo kigezo cha mwisho cha kuoa au kuolewa .

Mwaka jana nilipokuwa angalia tamthilia ya Merlin season 5. Pia nikakutana na ujumbe km huo, ukisema. There's things morely important to consider and more importantly than love when comes to marry.

Je kuna ukweli wowote??? au upendo (Love) ndo kila kitu???
 
Kwenye Merlin hiyo statement itakuwa ilitolewa kwasababu za kisiasa zaidi. Hapo na-assume aliyesema alikuwa anaongelea mapenzi ya Athur na yule binti mweusi. And ofcourse kwenye haya maisha kuna watu ambao wanatakiwa wazingatie sana 'social standard' linapokuja swala la ndoa kuliko mapenzi . Yani kuna watu wanatakiwa kuoa/kuolewa na JINA au PESA wala sio mapenzi kwasababu ya nafasi zao na ambitions.

Pili kwenye maisha ya kawaida kuna hii style ambayo ndo fashion ya siku hizi ya watu kuona ili kuinuka kiuchumi bila kupenda/kupendana. Kote huko hiyo statement ina-apply kwa kiasi kikubwa sana. Ila kwa baadhi ya watu mapenzi bado yana uzito wake yakifuatiwa na mambo mengine ambayo hatafanya mapenzi + ndoa inoge zaidi.
 
Vijana mko makini na ndoa kuliko hata investment na liability balance!

Ndo mijiafrika tulivyo.
 
Merlin mbona haina siasa, ila naamini kwa maadili ya uwepo family imara na bora, upendo hautoshi. Wandoa wanafunga pingu maisha huwa wanapendana. Je kinasabisha upendo kupotea???
 
Vijana muhimu kuchukua hatua ktk maamuzi ya mwenza wa maisha.

Mila na tamaduni za kiafrika, zinaamini uwepo wa magonjwa ya kurithi. Magonjwa hayo km kifafa, ukoma,asthma na n.k. pia na family za koo zingine wanawake wana mikosi na wanaume ni majambazi na n.k.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…