Nianze kwa kukutia moyo tu kwamba, pengine mimi nilikuwa mlevi kuliko kaka yako, lakini ukiniona leo hutoamini, naichukia pombe kwa milango yangu yote ya fahamu.
Tatizo la unywaji wa pombe uliopitiliza linaweza kuwa la kiroho au la Kisaikolojia. Hivyo, tiba itategemeana na chanzo cha unywaji huo. Kwasababu hakuna sehemu ya kupigia ramli kujua chanzo cha tatizo, inabidi ujaribu njia zote.
Kwa imani yangu mimi nilianzia Kanisani na nikafunguliwa, kwa kifupi ni kwamba nilikuwa nimeshikiliwa na nguvu kali sana za giza. Tena uende Makanisa ya Kiroho (ya Kilokole) kwa Mtumishi mwenye nguvu za Mungu kweli (omba ushauri na uisikilize dhamiri yako pia), ukienda kwa makanjanja utapoteza tu muda wako.
Kama ni la Kisaikolojia, tiba yake ipo pia, akafanyiwe counselling ambayo ni church-annexed (hii ni ile counselling ya makanisani kutoka kwa Watumishi wa Mungu wabobezi wa huduma hiyo), kwa mfano mimi kabla sijaombewa na huyo Mtumishi, alini-counsel kwanza, tena kikawaida tu; bila hata kutaja kifungu cha Biblia.
Kazi kwako mkuu. Ila usikate tamaa. Kumbuka, hakuna jambo linaloshindikana kwa Mungu (Luka 1:37).