Msaada dawa ya amoeba

angomwile

Senior Member
Sep 10, 2011
116
62
Jamani mwenzenu kwa muda mrefu nimekuwa nikisumbuliwa na tumbo na kila nikipima naambiwa nina amoeba na madawa nimetumia aina zote lakini sijapata naafuu yoyote,msaada kwa anayejua tiba kamili nawasilisha.
 
flagil z concerned, but u hv 2 stop drinks 4 a while!
 
Inawezekana kabisa huwa unapona huo ugonjwa baada ya kutumia dawa lkn baadaye unapata tena maambukizi mapya.Epuka kutumia kachumbali za kwenye bar au kwa mama ntilie kwani wao wanatumia maji yasiyo salama.Pia hakikisha kuwa unakunywa maji safi na salama sivyo utakuwa unatwanga maji kwenye kinu.Kuhusu dawa ili kukata mzizi wa fitna meza SECNIDAZOLE vidonge viwili kila siku kwa muda wa siku tatu.
 
Wakuu swali la nyongeza. Hivi dawa ya Amoeba inatibu pia minyoo Just in case nayo ipo tumboni?
 
Wakuu swali la nyongeza. Hivi dawa ya Amoeba inatibu pia minyoo Just in case nayo ipo tumboni?

Hapana mkuu...inabidi baada ya kutumia dawa za ameoba (amebicides, my preference is a single dose of tinidazole 2g tablets), utumie dawa za minyoo pia kama mebendazole au albendazole!!
 
Jamani mwenzenu kwa muda mrefu nimekuwa nikisumbuliwa na tumbo na kila nikipima naambiwa nina amoeba na madawa nimetumia aina zote lakini sijapata naafuu yoyote,msaada kwa anayejua tiba kamili nawasilisha.

Una uhakika ni amoeba? Amoeba kwa uhakika inapimwa na kipimo cha kuchukua choo kikubwa/haja/m*vi na kupima kwenye darubini (microscope), we umefanyiwa kipimo hicho amoeba wakaonekana? Kama ni kweli umefanyiwa kipimo cha choo kikubwa na amoeba wakaonekana mara kwa mara....basi naomba ujue kuwa we ni mchafu sana (samahani nakushushua lakini ndio ukweli)!

Amoeba (Amoebiasis) ni ugonjwa ambao tunaita faeco-oral...kwa maana rahisi ni kuwa 'umekula mavi'! Iwe kwenye maji, mboga za majani au matunda yasiyooshwa vizuri...lakini umekula mavi yenye wadudu wa amoeba, hiyo ndio njia kubwa ambayo unaweza pata amoeba! Na si ugonjwa mdogo mdogo kama watu wanvyodhani, kwani ukiwa sugu au kutotibiwa vyema, wadudu hao wa amoeba (hasa entamoeba histolytica) huwa wanfika mpaka kwenye ini na kusabisha jipu kwenye ini, tatizo amabalo linaweza likasababisha kifo.

Kama unapata ugonjwa huo mara kwa mara (ikithibitika na maabara kwa kupima choo), basi ni aidha dawa unayotumia haitibu amoeba kwa ufanisi, au unatmia vibaya dawa kwa kukatiza dozi au kunywa dozi isiyotosha, au unatumia vizuri tu dawa lakini unapata maambuki mapya kwa tabia yako ya uchafu.

Ushauri:
- Nenda hospitali ukapime choo kuthibitsha ni amoeba kweli. Kama kweli pata matibabu na umalize doazi husika. Dawa za familia ya Metronidazole (Flagyl) ni nzuri...lakini jaribu kutumia zile mpya zenye nguvu zaidi mfano Secnidazole au hata Tinidazole.
- Jikinge na maambukizi mapya kwa:
1. Osha mikoni kwa sabuni na maji yanayotiririka kila unapotoka chooni, na unapotaka kula
2. Osha choo na/au bafu mara kwa mara ukitumia antiseptics mfano dettol
3. Epuka kuchangia taulo za kukausha mikono utokapo kutumia choo
4. Epuka kula mboga mboga/kachumbari (salads) za mitaani au zisizooshwa vizuri, na matunda pia
5. Chemsha maji ya kunywa, na/au weka 'water guide'
6. Kama upo kijijini, tumia choo kwa haja kubwa...sio upori!
 
Inawezekana kabisa huwa unapona huo ugonjwa baada ya kutumia dawa lkn baadaye unapata tena maambukizi mapya.Epuka kutumia kachumbali za kwenye bar au kwa mama ntilie kwani wao wanatumia maji yasiyo salama.Pia hakikisha kuwa unakunywa maji safi na salama sivyo utakuwa unatwanga maji kwenye kinu.Kuhusu dawa ili kukata mzizi wa fitna meza SECNIDAZOLE vidonge viwili kila siku kwa muda wa siku tatu.
sawa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom