MSAADA: BLACKBERRY VS.ipHONE VS. HTC

mkuu mbona kila mtu nnaemfahamu mimi mwenye Iphone anawezafanya hivyo, sio ishu sana ngoja nipost namna ya kujailbreak hapa..
Mkuu wacha kumpotosha mkuu issue ya kujailbreak iphone hasa iphone 4 sio rahisi kama unavyofikiria ndio maana sapna wanajailbreak simu moja kuanzia sh 60,000 hadi laki moja,simu ikiwa imelockiwa na kampuni kama Verizon sio rahisi kuijailbreak kama unavyofikiria coz hawa jamaa kuna chip huwa wanaifunga kwenye hizi iphone thats why software za kujailbreak zinakuwa ni tofauti na za mitandao mingine kama vile orange,hizo tutorial zinazotolewa kwenye google na hizo software hazijakamilika unaweza ukazidownload ukafuata kama kawaida lakini ikishamaliza lazima ije error namba 1015 inayohusika na kuganda kwa logo ya apple,so kuna program ambayo ni ndogo sana ya kumaliza hilo tatizohawa jamaa hata siku moja hawaiweki bure kwenye mtandao kama zingine bali inauzwa kuanziia dola 20 na kuendelea,ilinichukua wiki moja kujailbreak iphone 3gs na baadae ikanibidi ninunue hii software kwa dola 25 lakini nilifungulia simu tatu na ipod touch 2 na hadi leo zinafanya kazi vizuri tu.Nasema haya nikiwwa mwenye idea ya hivi vifaa vya apple na najua ubovu wake uko wapi,yaani ukikosea kidogo tu basi kama ni simu utaiweka kabatini huku unaipenda .
 
ivi,kwa hapa bongo ku jailbreak(chakachua)iphone inawezekana ili usilimitiwe kudownload only from applestore///?
Mkuu jailbreak ina maana ya kuwa hiyo simu itumie applications zingine zaidi ya apple ambayo inaitwa Cydia.
 
wamechakachua..... kitufe chs SENKYUUU.... NINGEKUGONGEA!!!!!!!!!
 
Mkuu kama uko serious ni PM
naona upo kibiashara zaidi, kama una njia yakwako mwenyewe ya kuJailbreak si upost hapa kwenye forum kila mtu aione,,angalia kichwa cha habari hapo juu mkuu amesistiza asaidiwe sio utangaze biashara yako kwenye post yake..ndio maana nikaandika kama kapata tatizo na Iphone yake baada ya kujaribu maelezo aseme asaidiwe zaidi, hapa nilipo natumia Iphone 4 na sijalipa chochote Sapna waiJailbreak!!
 
Mkuu i don do any kind of business,we si unajua jinsi ya kujailbreak hizo simu software zinapaticana JailbreakMe 3.0 hawa jamaa ni wajanja sana kwanza hauwezi kuingia kwenye members kama wewe sio mwanachama na kuwa mwanachama unatakiwa ulipa dola 25 hadi 30 na hauwezi kutumia hizo software zao kama sio mwanachama coz naweza nikaweka link ikawa kazi bure kwa sababu hawa jamaa wako makini sana sasa wewe unafikiri mimi nitamsaidia vipi huyu mkuu ndio maana nikamwambia anipm ilinijue nitamsaidia vipi kama hauniamini ingia hiyo site ujionee mwenyewe na hiyo iphone 4 yako ilikuwa iko free kwa mitandao yote,kuna iphone ambazo hata hao Sapna wenyewe wanazishindwa ambazo zillitumika na mtandao wa Verizon
 
wakuu mbona Iphone 4 inaJailbreakika kirahisi tu, yangu nimetumia greenpoison na nimeJailbreak successfully.
lakini maranyingi huwa wakitoa Firmware mpya lazima uiJailbreak tena...
 
software zipo sehem nyingi tu online tena bure kabisa ustake kutuibia sio jailbreakme pekeyake, zipo iphoneforums.net, ipmart-forums.com, noeman.org/gsm, forum.gsmhosting.com, idownloadblog.com, iphonehacks.com na zingine nyingi tu hata ukiGoogle njia rahisi zaidi. labda kama unavyosema za verizon ni ngumu kuJailbreak ila bado sijakutana na inayogoma.hivi vitu vipo bure kabisa na maelezo yake tele kwenye net pamoja na reviews za watu waliokwishajaribu.
 

Mkuu ubarikiwe! Nashukuru sana kwa kusoma hayo maelezo na kufuata procedure iliyoelezwa hapa juu nimefanikiwa kujailbreak na ku-unlock simu yangu iphone 4 32 GB iliyokuwa imefungwa na at&t japo niliazimika kununua software kutoka jailbreakme.com ya kama $20 hivi ila uanachama wa lifetime.

Nashukuru sana kwa elimu hii kwani Sapna waliniharibia wakashindwa kuirudisha ilivyokuwa na mbaya zaidi wakalamba microSIM yake inabidi nitafute nyingine

Otherwise ipo safi natumia kwa WI-fi hadi nipate line yake tena
 

sawa sawa mkuu'...:A S thumbs_up:
 
Apple leo naona wametoa ios 4.3.4 so tunasubiri jail break nyingine duh tech inakwenda fast sana wakuu!
 
Blackberry 9780/9700 wala hata wasikuangaishe na hizo hapo juu. Battery backup ipo juu (1500mAh) ni ya uhakika sana na wala hautakuwa na haja ya kuzima internet kama wenye iPhone na Android wanavyofanya kuzima internet ili wapate battery ikae kwa muda mrefu.
 
sawa sawa mkuu'...:A S thumbs_up:
Sasa mkuu niliyokua nikiyasema nadhani sasa utakuwa umeamini hauwezi kujailbreak au kuunlock for free of charge bila ya kununua baadhi ya software kutoka jailbreakme na ni vitu vidogo sana vinavyowasha simu ambavyo hizo site za free wameshindwa kuviweka,wazungu ni wajanja sana na wanajua kila wanachokifanya.
 
kwa upande wangu naona iphone is the best kwa kila kitu, swala la jailbreak ni muhimu afu kuhusu kufanya update naona ni chaguo lako mwenyewe, maana sometime update ya ios huwa inaongeza features chache ambazo mara nyingi hatuzitumii kivile na hata kama zinatumika ni asilimia chache sana,alafu pia unaweza pata hizo new feature kwenye cydia km iphone yako ipo jailbreaked, pia features nyingi ambazo hata apple wenyewe hawajaziweka hata pengine kuzifikiria zinapatikana kwa wingi cydia.
kwa hiyo upande wangu iphone is the best, na kinachoifanya iwe best ni operating system yao ipo very god and stable na application nyingi ambazo ni useful zinapatikana kwa urahisi, yani wewe ukitaka app yoyote unayofikiria, kwa asilimia kubwa lazma iphone itakuwanayo, na vilevile hata kama utaona kuna baadhi ya features ulishazoea kuzipata kwenye simu zingine(kwa watumiaji wa nokia symbian wa zamani),hapa kwenye iphone utapata almost kila kitu kinachorandana, ila ni unabidi uwe tayari kukumbana na kashikashi zake km ukiamua kuitumia.
 
hizo 'baadhi ya software' unazomaanisha ni zipi, mbona software hizi redsnow, snowbreeze, greenpoison zinaJailbreak vizuri tu na haziuzwi, kuna link hapo juu kwenye post inakupeleka kudownload snowbreeze moja kwa moja bila kununua au hujaiona!..mkuu ukingangania jailbreakme wakati sources zingine zinaprovide bure utakuwa unapoteza hela bure....:fish:
 

Acha kudanganya watu hapa. Nimechakachua Iphone yangu mwenyewe bure bila kulipa hata senti moja.

Just go to youtube and you will get very good instructions on how to do it and where to get the free software.

You have to appreciate the fact that there is no one way of doing things. Kama wewe unajua njia moja basi wenzako wanajua njia zingine.
 
Wakuu nahisi blackberry ni poa zaidi.

Wengi wa wachangiaji wameipa nyota kubwa Iphone lakini wakaja na ishu ya jailbreaking.

Poleni kwenu kwani kwenye BB hii habari haipo.

Ila kama alivosema mkuu mmoja hapo inategemea wewe katika simu ni mpz na mambo/features gani...

Otherwise michango ni mizuri na ya kuelimisha sana. Big up kwenu wote wachangiaji...
 
asante mkuu kwa kumuelimisha jamaa maana najaribu sana kumueleza kwamba sio jailbreakme pekeyake wanaoweza kujailbreak lakini hana nia ya kuelewa..:mod: :mod:
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…