Msaada Betri ya simu inavimba.

Msaada Betri ya simu inavimba.

sweetlee

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2015
Posts
4,050
Reaction score
14,770
Naomba msaada. Natumia Samsung Note 4 tatizo Betri inavimba. Shida Ni nini? Nimebadili Betri mara 3 tatizo linajirudia.
 
Unanunua betri zile OG au hizi za mchina?

Kama unanunua OG achana nazo
Tafuta mchina kama vile Excellent au Concord utaenjoy simu yako ndugu
 
OG ni kama hii
Sasa hizi OG achana nazo we nunua michina tu hasa hasa excellent au Concord
IMG-20180625-WA0014.jpg
 
Pole sana kwa maswaibu yanayokupata,kama umebadili betri mara 3 na bado tatizo linaendelea nashauri jaribu kuwasiliana na dealer wa hiyo simu wenda system yake ya chaji sio nzuri.
 
Naomba msaada. Natumia Samsung Note 4 tatizo Betri inavimba. Shida Ni nini? Nimebadili Betri mara 3 tatizo linajirudia.
Naungana na wadau wanaoshauri ununue betri za Excellent, mimi nilikua na S4 betri ilikua ikikaa wiki 3 haijavimba ni bahati nikanunua excellent 15,000 tu kuanzia hapo tatizo likaisha.
 
Duuuuu Kama battery ni kubwa hvyo????Je simu yenyewe itakuaje????Yote kwa yote simu itakuwa imexpire AC
 
Duuuuu Kama battery ni kubwa hvyo????Je simu yenyewe itakuaje????Yote kwa yote simu itakuwa imexpire AC
Note 4 ni kubwa kwa size 5.7" screen
Battery 3220mAh tatizo la battery zake ni kwamba tangu zitengenezwe huko 2014 hazijawahi kua re-loaded inamaana zimekaa tu mpaka unapokuja kununua simu ndo unaanza kuitumia 2018 unakuta ishapungua ubora inaanza kusumbua.
Suluhisho ni kununua battery za kichina kama excellent hizi zinazouzwa vibandani tu
 
Subiri kulipukiwa na hiyo simu. Kumbuka, betri ya simu ina mlipuko mkali sana...
 
mi nilishawahi nunua hizo zinazoitwa og kwa elf 25 kama mara mbili lakini miezi ni 6 tu inavimba,kuna siku nikapita tandika nikanunua ya elf 10 ilidumu muda mrefu sana nilikuwa natumia samsung galaxy note 2 kwahiyo hao wauzaji sio wakuwaamini
 
Naomba msaada. Natumia Samsung Note 4 tatizo Betri inavimba. Shida Ni nini? Nimebadili Betri mara 3 tatizo linajirudia.
Chukua Sindano halaf itoboe kwa juu (sio pemben, pale battery inapolalia) Itatoa Haruf kal na gas flan.
Iache kwa muda ipoe itakua inanywea taratiibu... baada ya muda itakuwa kwenye hali yake ya kawaida. Irudishe kwenye simu endelea kutumia kama kawaida. Urudi kushukuru ukifanikiwa.
Hii njia nimesha ifanya hivyo inafanya kazi, Nilikuwa nakutana na hayo matatizo battery ikavimba mpaka mfuniko wa sim uka pasuka nilipopewa huo ujanja nikafanikiwa.
 
Unanunua betri zile OG au hizi za mchina?

Kama unanunua OG achana nazo
Tafuta mchina kama vile Excellent au Concord utaenjoy simu yako ndugu
Ya kwanza ilikuwa OG ikavimba. Nikatumia Excellent ikavimba. Concord ndio bado sijatumia.

Sent from my SM-N910T using JamiiForums mobile app
 
Naomba msaada. Natumia Samsung Note 4 tatizo Betri inavimba. Shida Ni nini? Nimebadili Betri mara 3 tatizo linajirudia.
Ushauri ni kama wadau waliopita ila jarbu kuwapigia campuni husika inawezekana aina ya betry utumiazo sio sahihi muhimu sana. Pia unaponunua betry mpya fuata maelekezo upeayo ya kuicharg betr kabla haujaitumia.kua makini kuna vifaa feki vimeenea nowdayz.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom