Msaada: Asili yangu inanishangaza

Hapo kwenye big five nigusie na mm

Iko hivi, BIG FIVE PERSONALITY MODEL ilitokana na maboresho ya PSYCHOLOGICAL TYPOLOGY ya CARL .G. JUNG ambae ndo aliewabainisha watu katika makundi makuu mawili INTROVERTS na EXTROVERTS.

Hivyo basi katika BIG 5 kuna traits 5 zinazounda personality nzima ya mtu na kila trait inaanzia upande mmoja mpaka wa pili ambao ni kinyume kabisa na ule wa mwanzo.

mfano rahisi usio halisi ni kuwa rangi ya ngozi ya binadamu( hapa nitaichukulia kama trait) ni mojawapo ya sifa ya mwonekano wake wa nje( hii ndo mfano wa hainba au personality) na kila mtu anaangukia katika rangi flani kuaanzia mweupe mpaka mweusi na hakuna rangi mbaya au nzuri kuliko nyingine sema tu binadamu wakiamua kuvumisha jambo (kwa kukosa maarifa sahihi) kuwa mtu mweupe ni mbaya au mweusi ni mzuri linapitishwa na hapo ndo ubaguzi wa rangi na matatizo yote yanapoanzia . Kwa hiyo usipokuwa mwelewa wa mambo kama wao unaweza kuambiwa unaumwa au wewe kichaa au ukashindwa hata kufanikisha malengo yako kwa kukosa ushirikiano au kushindwa kwendana nao.Japo ni kweli kuna faida na hasara za kila upande.

Hivyo ni muhimu sana kujua faida na hasara traits zako zote ili uweze kuishi kwa amani na kila mtu na kufanikisha malengo yako. Hapa chini nitajaribu kuelezea kwa kifupi traits 2 kati ya 5 nlizoziona kwa mtoa mada hapo juu na faida na hasara zake.

Hizo traits 5 ni

1.OPENNESS
2.CONSCIENTIOUSNESS
3.EXTROVERSION-ni hali ya mtu kupenda kuongea , kutoka out, shangwe, marafiki wengi, story nyingi, party sana, harusi , shughuli na mambo kama hayo kiufupi ni watu wa mizuka na wanajiamini
4.AGREEABLENESS- ni hali ya mtu kukubaliana na wengine, kusaidia, kukubali mawazo ya wengine, huruma kwa wengine na kutopenda kuwakwaza wengine.
5.NEUROTICISM

Sasa mtoa mada yeye hapo kwenye 3 ana LOW EXTROVERSION kwa maana ya kuwa yeye ni kinyume chake i.e ni INTROVERT faida yake kubwa ni huwa wana uwezo zaidi wa kufikiri na kuchambua mambo kabla ya kuropoka au kukurupuka. Hasara kubwa ni kukosa connections za kufanikisha mambo na kuchelewa kufanya mambo kwa kukalia kufikiria na kuchambua au kutokujiamini haswa mbele za watu.

Tukija kwenye 4 mtoa mada ana LOW AGREEABLENESS kwa maana akishikilia jambo hataki kupingwa kirahisi, hana huruma za ovyo ovyo, anapenda kusimamia ukweli hata kama utamuumiza mtu. Faida yake ni kuwa ni ngumu kupelekeshwa katika maisha yake , na wanakuwaga wazuri kwenye sehemu zinazohitaji maamuzi magumu, hasara ni kuwa wanachukiwa na watu wengi kwa kuwa hawakubaliani kizembe na mawazo yao au wanajiona kuwa wao wako sawa kila muda na hawana huruma za ovyoovyo kwenye kusimamia ukweli au haki.

Kiufupi haiwezekani kuelezea kila kitu hapa na ngumu kuelewa hivi vitu kwa watu wengi
 
Stay blessed watu kama nyinyi yawezekana mmebaki wachache sana
 
Katikq utulivu wako jaribu kuspend muda mrefu bafuni kwako ukimwditate bila nguo.

Kuna majibu utayapata yafanyie kazi
 
Kama maisha hayo yanakupa furaha endelea kuishi hivyo,maisha ni furaha achana na wapiga domo ambao muda wote wanapenda wawe wanasikilizwa wao tu na ndio faraja yao ilipo,usikubali wakutoe kwenye ulimwengu wako wakupeleke kwenye ulimwengu wao ili wakupe huzuni.Mimi mwenyewe ni kama wewe tu naweza shinda ndani siku hata tatu bila kuonana na mtu yeyote na hakuna shida na ninayafurahia maisha.Achana na hao wanasaikolojiia wa mitandaoni wanaosema “eti dalili za ugonjwa wa kichaa”
 
Utaanza kukimbia uchi ukidhani uko pekeyako (simaanishi dishi limeyumba)
 
Tuliosoma Cuba tumekuelewa

Waliosoma Urusi muda huu wamejazana huko PM.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…