Msaada: amenunua simu ya wizi na yupo kituo siku ya nne

Ndilla

Member
Dec 22, 2012
42
7
Tukio limetokea mkoani Kigoma, ameuziwa Samsung galaxy toka 15.03.2017 na kijana aliyetokea Dar-es-salaam na baada akarudi lakini ni naye mzaliwa wa eneo hili pia. Baadae mtuhumiwa alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha anashida naye kumbe alikuwa POLISI, tatizo tulilonalo ni jinsi ya kumpa dhamana kwa sababu POLISI wamekataa kwa kusema kuwa RB ya kesi yake ipo kituo cha polisi cha Ostabei. Je kisheria ipo sawa?
 
Kama jalada lake lipo Oysterbay, kwa nini wasimsafirishe sasa mpaka huko ili apate kupatiwa maelezo?
 
Jaribu kupanda ngazi ikiwezekana hata kwa kamanda wa polisi mkoa.
Ndugu yangu alishawai kipata tatizo kama hilo. Tulipambana ngazi kwa ngazi ikabidi wampeleke kwenye mahakama iliyo karibu ili apewe dhamana . Wakati anasubiri taratibu za kusafirishwa.
 
Back
Top Bottom