Msaaada jamani ndoa iko hatarini kuvunjika

mkuu kama umeweza kukaa nae miaka 8 bila tatizo im sure mnajuana vyema in and out unajua weakness zake na strength zake tumia hizohizo kumueleweshaa na mrudishke mambo kwenye mstari by the way wewe ndo kiongozi wa famiia kila kitu kiko chini yako
 
Dah... Pole sana mtoa mada, inawezekana kuna kitu ambacho mkeo alikiona kikahashiria wewe kutokuwa mwaminifu....

Hawezi kutoka from nowhere akaanza kuyafanya hayo.Jiangalie upya. Na simu isiwe chanzo cha kuvunja ndoa ambapo wahanga watakuwa ni watoto wasio na hatia

#ThinkTwice
 
Hajiamini mkeo,inawezekana ulimpa sababu kwa matendo au kauli zako!
Kama ni simu tu unaweza ukamrekebisha kwa kumueleza madhara ya afanyayo ila kama hapendi hata uchanganyike na ndugu na jamaa basi huyo ni possessive na anahitaji msaada.
 
Hatuwezi kukusaidia kwa maelezo yako ya upande mmoja. Tungepata ya upande wa pili tungejua kisa haswa kilianzia wapi, lazima kuna sababu sio bure mke wako hawezi kukuhisi vibaya from no where.
 
Nakataa nasema nakataa kumuachia mwenza apokee simu au kuweka loud speaker eti kwa sababu hakuamini ndo unataka akuamini. Huo ni utumwa, si mahusiano yenye afya. Haya, simu unampa, siku akikwambia "leo tunaenda wote huko kazini au kwenye hicho kikao". Au kila muda wa lunch ofisini ukifika yuko reception au mlangoni kwako anakusubiri. Au anakupigia kwa land line ya ofisi. Utamweleza ulikuwa chooni au kwenye kikao akuelewe? Utayaweza?

Mwenza anayekufanya ukose uhuru wa ku-interact na wenzio na wakati mwingine kukulazimisha hata useme uongo ili tu kuepusha shari si mwema - anatakiwa kuachwa ila kwa kuwa huyu ni mwanandoa anahitaji kurekebishwa. Wapo wenza wanaopokeleana simu - ndo jinsi walivyojizoeza na haikutokana na ukosefu wa imani na si kila simu wanapokea na si kila wakati. Wapo wenza hawachungulii simu za wenzi wao hata iite mara 100, si kwa sababu wanaaminiana sana ila kwa sababu hawaaminiani na hivyo wanajiepusha na maradhi ya moyo. Imani manake ni kuwa "hata kama haupo naye, mwenza wako hafanyi uzinzi". Kama humuamini mwenzio basi ingia kwenye pichu yake uende nae kila anakoenda. Ya nini kusubiria simu? na kama huwezi kuvumilia usaliti na unajua hata ukigundua huwezi kumuacha unamfata fata nini mwenzio kwenye simu yake?

Halafu hivi ukishajua rafiki yako au ndugu yako simu yake inapokelewa kwanza na mwenza wake utakuwa na uhuru wa kupiga kweli? Mara nyingi utasubiri mpaka muonane live. Sasa huko si kumuweka mtu kwenye kisiwa? Kuna wenza tu wana tabia hizi za wivu wa kijinga: simu anataka achunge: nani kapiga, saa ngapi, mara ngapi, alisema nini, kwa muda gani; marafiki akuchagulie tena ikiwezekana usiwe nao kabisa, kila kona uipitayo anataka aijue, kila ufanyalo anataka alijue, anataka ukae nae yeye tu hata kwa ndugu usiende, kama ana hela ataweka hata watu wa siri wa kukufatilia! Na kwa taarifa hawa ukiwaendekeza hawakawii kukupa limbwata kama ni wanawake, hawakawii kuanza kukupa vipigo kutokana na hisia za kuibiwa, hawakawii kukwambia acha kazi ukae nyumbani, hamna kuona ndugu wala marafiki. Kiwango cha juu kabisa cha hii tabia ni kudhuru wenzi wao au wao wenyewe ikiwa ni pamoja na kuua au kujiua. Hili naliongea kwa hakika - nina uzoefu nalo. Tusichukulie tabia za binadamu kirahisirahisi.
 
na simu yenyewe mwachie akae nayo yeye km jioni tu hajakurudishia na misamaha kibao..
 
jitahidi uwe muwazi, ishu si tu kumpenda na kumuamini bali mfanye yeye aone kua unampenda na atajifunza kukuamini taratibu
 
Shida ni kua mke wangu kila siku tunakwaruzana kisa simu akiona simu inapigwa yeye ataikimbilia akiona jina la mwanamke basi anaweza kuipokea ili ajuwe ni nani au anataka musikilize shirika ukimalize aanze kuhoji huyo ni nani na anatala nn? Ukimiambia kua ni rafiki hakuelewi hapo ataanza oooo unawana wake kwa kua siku hizi una kazi kila nikijitahidi kumuelewesha basi hakubali ananiona kicheche

Rafiki wa kike! No, bora ungesema ni mfanyakazi mwenzio na kweli iwe simu ya kikazi. Hizi habari za kupigiana pigiana simu weekend au usiku (masaa ambayo siyo ya kazi) na kuanza kupiga piga story ambazo sio za msingi ni tatizo kwenye mahusiano.

Ukitaka kuweza ni wewe kwanza kucontrol hizo calls za opposite sex, call ziwe za kikazi, au kuulizana vitu vya kawaida lakini sio mambo ya kuanza kupiga story, story huko huko kazini ila ukirudi home story ni wewe na mke wako tu.

Hizi ni baadhi ya changamoto ndogo sana, ambazo hata hutakiwi kuwaza kuachana, unaweza kuzifutilia mbali kwa kuacha habari za kuwa na marafiki wa jinsia tofauti, marafiki wenyewe hawaaminiki, ukute mtu anakupigia pigia ili mzoeane akuchukue.

Chunga sana, hata mimi siwezi kumwelewa wife eti ana marafiki wa kiume ambao anaongea ongea nao mida ambayo niko naye, sitaki. Kama wanaulizana kitu sawa, ila sio mambo ya story za kijinga jinga. Asubiri akiwa kazini watapiga story huko, akija nyumbani ni mimi na yeye.
 
Ukweli hakuna cha ziada ila mwanzo hakua na hio tabia ingawa kwa sababu ya watu wa mtaani kupeleka umbeya usio na ukweli kwa hio miaka hio aliami kua ni ukweli hadi sasa haniamini ananiona msaliti
 
Nakataa nasema nakataa kumuachia mwenza apokee simu au kuweka loud speaker eti kwa sababu hakuamini ndo unataka akuamini. Huo ni utumwa, si mahusiano yenye afya. Haya, simu unampa, siku akikwambia "leo tunaenda wote huko kazini au kwenye hicho kikao". Au kila muda wa lunch ofisini ukifika yuko reception au mlangoni kwako anakusubiri. Au anakupigia kwa land line ya ofisi. Utamweleza ulikuwa chooni au kwenye kikao akuelewe? Utayaweza?

Mwenza anayekufanya ukose uhuru wa ku-interact na wenzio na wakati mwingine kukulazimisha hata useme uongo ili tu kuepusha shari si mwema - anatakiwa kuachwa ila kwa kuwa huyu ni mwanandoa anahitaji kurekebishwa. Wapo wenza wanaopokeleana simu - ndo jinsi walivyojizoeza na haikutokana na ukosefu wa imani na si kila simu wanapokea na si kila wakati. Wapo wenza hawachungulii simu za wenzi wao hata iite mara 100, si kwa sababu wanaaminiana sana ila kwa sababu hawaaminiani na hivyo wanajiepusha na maradhi ya moyo. Imani manake ni kuwa "hata kama haupo naye, mwenza wako hafanyi uzinzi". Kama humuamini mwenzio basi ingia kwenye pichu yake uende nae kila anakoenda. Ya nini kusubiria simu? na kama huwezi kuvumilia usaliti na unajua hata ukigundua huwezi kumuacha unamfata fata nini mwenzio kwenye simu yake?

Halafu hivi ukishajua rafiki yako au ndugu yako simu yake inapokelewa kwanza na mwenza wake utakuwa na uhuru wa kupiga kweli? Mara nyingi utasubiri mpaka muonane live. Sasa huko si kumuweka mtu kwenye kisiwa? Kuna wenza tu wana tabia hizi za wivu wa kijinga: simu anataka achunge: nani kapiga, saa ngapi, mara ngapi, alisema nini, kwa muda gani; marafiki akuchagulie tena ikiwezekana usiwe nao kabisa, kila kona uipitayo anataka aijue, kila ufanyalo anataka alijue, anataka ukae nae yeye tu hata kwa ndugu usiende, kama ana hela ataweka hata watu wa siri wa kukufatilia! Na kwa taarifa hawa ukiwaendekeza hawakawii kukupa limbwata kama ni wanawake, hawakawii kuanza kukupa vipigo kutokana na hisia za kuibiwa, hawakawii kukwambia acha kazi ukae nyumbani, hamna kuona ndugu wala marafiki. Kiwango cha juu kabisa cha hii tabia ni kudhuru wenzi wao au wao wenyewe ikiwa ni pamoja na kuua au kujiua. Hili naliongea kwa hakika - nina uzoefu nalo. Tusichukulie tabia za binadamu kirahisirahisi.

Una point, lakini fikiria situation ambayo mwanaume anampigia simu mke wako (assuming wewe ni mwanaume) wanaongea umbea umbea tu, wanachekeshana story nyiiingi halafu iwe mara kwa mara, ukiulizwa unaambiwa ni rafiki yangu.

Kwa mfano tukiwa hatujaoa tunakuwa na story story za hapa na pale na watu wa jinsia zote bial kujali, lakini ikishatokea mtu akaoa, lazima story ziwe na mipaka, hata kama ni jinsia moja.
 
Inategemea labda ulishampa reason ya kuku doubt, kuna wanawake tuko hivyo yani nikikumaini nakuamini kweli ila ukinipa sababu ya kutokukuamini kweli utajuta, haiwezekani ndani ya miaka 8 muishi vzr bila hizo kelele leo from no where aanze visa, ingekuwa umesema kwamba ulipomuoa ulikuwa na pesa lakini kwasasa hali mbaya ningeweza sema anatafuta sababu baada ya kuonamambo yamekuwa magumu lakini kama alionyesha upendo wa kweli kipindi cha dhiki iweje kwenye neema ndo aanze visa? hapana bwana kuna namna, tuelezee vzr

Nimekupenda bure shost kuanzia leo nitakuwa nakuita shost yangu eeeh, well said kabisa, mtoa mada naona urudie kumsoma mrsleo hapo utapata majibu ya chanzo cha tatizo la wife, mie mwenyewe nikikutrust utapenda 100% amani lakini nikikustukia tu na kausaliti aisee nina gubu utakimbia ndani lakini wakati yote hayo umeyasababisha mwenyewe
 
Habari wana wakubwa

Kwa kweni nakuja mbele yenu kutaka msaada niko na mke wangu mwaka wa 8 sasa na tumebahatika kupata watoto 2 wa kike na wa kiume.

Kwa hakika nampenda sana mke wangu kwani tumetoka mbali alinivumilia kuishi na mm kipindi kigumu cha kipato changu kua pia kwa kunizalia watoto.

Shida ni kua mke wangu kila siku tunakwaruzana kisa simu akiona simu inapigwa yeye ataikimbilia akiona jina la mwanamke basi anaweza kuipokea ili ajuwe ni nani au anataka musikilize shirika ukimalize aanze kuhoji huyo ni nani na anatala nn? Ukimiambia kua ni rafiki hakuelewi hapo ataanza oooo unawana wake kwa kua siku hizi una kazi kila nikijitahidi kumuelewesha basi hakubali ananiona kicheche

Hadi naiona ndoa haina amani mpaka natamani hata kutoa maamuzi mabaya ila tatizo watoto wangu bado wadogo nimekua namchoka kwa kutokuniamini hadi maneno machafu yanamyoka hutamani kumpiga ila najihisi nitamuonea.

Mimi simu yake sishiki wala sifuatiliii maana sioni sababu na nimemnunulia simu mbili ila anaweza akazifungia hata wiki eti hazina chaji wakati nyumbani pana umeme namtilia salio kwa mwezi basi unaweza kuisha mwezi bila ya yeye kutumia hilo salio.

Kwa kweli nampenda sana ila kuacha kutumia simu kwa ajili yake siko tayari kwani kazini kwangu kia na simu ni jamabo la lazima .

Wew ni mpuuzi, Mume wa mtu unaendekeza mawasiliano ya kipuuzi na wanawake wengine ili nin? Mume wa mtu utakuwaje na utafiki na mwanamke hadi wa kupigiana simu ili nin? Hapo wew hako kakazi na visent unavyopata ndo vinakupa jeuri hata ya kufikiria uachane na mkeo kisa kuendekeza mawasiliano yasiyo na ulazma na watu wengne.... Kuwa kam mwanaume bhana.
 
Ushauri wa bure; unapoingia katika mahusiano rasmi aidha uchumba au ndoa unatakiwa upunguze ukaribu wako na jinsia nyingine. punguza huo urafiki na jinsia ya kike, mkeo anatosha kuwa rafiki yako
Kama lazima kuwa karibu na hao marafiki wa kike labda kutokana na uhusiano wa kikazi basi jenga mipaka ya mawasiliano kati yenu. sio muda wote ni wa kuwasiliana. Tena muwasiliane kwa mambo muhimu tu, sio porojo.
Naamini hata wewe hutokuwa tayari kuona mkeo ana marafiki wa kiume wasio na umuhimu wowote.
Halafu waswahili wanasema 'Mume anauma'.
 
1. Ishi naye kwa akili sana anakupenda sana lakini hakuamini wewe.
2. Toka naye mara kwa mara ili ahisi mabadiliko hayo mapya ya kimahaba.
3. Siku nyingine kama unayo nafasi hama nyumbani kwa muda hamia hotelini aone mabadiliko. Hakika penzi atakalo kupa huko hotelini utakuja kuni PM hapa JF
 
Nimekupenda bure shost kuanzia leo nitakuwa nakuita shost yangu eeeh, well said kabisa, mtoa mada naona urudie kumsoma mrsleo hapo utapata majibu ya chanzo cha tatizo la wife, mie mwenyewe nikikutrust utapenda 100% amani lakini nikikustukia tu na kausaliti aisee nina gubu utakimbia ndani lakini wakati yote hayo umeyasababisha mwenyewe

Powa shost angu tehe
 
Rafiki wa kike! No, bora ungesema ni mfanyakazi mwenzio na kweli iwe simu ya kikazi. Hizi habari za kupigiana pigiana simu weekend au usiku (masaa ambayo siyo ya kazi) na kuanza kupiga piga story ambazo sio za msingi ni tatizo kwenye mahusiano.

Ukitaka kuweza ni wewe kwanza kucontrol hizo calls za opposite sex, call ziwe za kikazi, au kuulizana vitu vya kawaida lakini sio mambo ya kuanza kupiga story, story huko huko kazini ila ukirudi home story ni wewe na mke wako tu.

Hizi ni baadhi ya changamoto ndogo sana, ambazo hata hutakiwi kuwaza kuachana, unaweza kuzifutilia mbali kwa kuacha habari za kuwa na marafiki wa jinsia tofauti, marafiki wenyewe hawaaminiki, ukute mtu anakupigia pigia ili mzoeane akuchukue.

Chunga sana, hata mimi siwezi kumwelewa wife eti ana marafiki wa kiume ambao anaongea ongea nao mida ambayo niko naye, sitaki. Kama wanaulizana kitu sawa, ila sio mambo ya story za kijinga jinga. Asubiri akiwa kazini watapiga story huko, akija nyumbani ni mimi na yeye.

Well said, hapo umemaliza kila kitu na asipokuelewa basi tena. Yaani jianaume zima linafanya upuuzi mwenyew anakuja kulalamika huku, Inaboa sana na kusikitisha. Halafu kuachana anaona ndo solution kisa kapata vischana vya kuongea nae.. Wanawake tunatakiwa tuwe makini sana na hawa watu.
 
Una point, lakini fikiria situation ambayo mwanaume anampigia simu mke wako (assuming wewe ni mwanaume) wanaongea umbea umbea tu, wanachekeshana story nyiiingi halafu iwe mara kwa mara, ukiulizwa unaambiwa ni rafiki yangu.

Kwa mfano tukiwa hatujaoa tunakuwa na story story za hapa na pale na watu wa jinsia zote bial kujali, lakini ikishatokea mtu akaoa, lazima story ziwe na mipaka, hata kama ni jinsia moja.
Mimi ni mwanamke kaka.
 
Back
Top Bottom