Msaaada jamani ndoa iko hatarini kuvunjika

Msaaada jamani ndoa iko hatarini kuvunjika

Mimi ni mwanamke kaka.

Okay, jivalishe viatu vya huyo mke, mume wako kila siku anaongea na mwanamke anayemwita rafiki (sio mfanyakazi mwenake, of course hata kwa mfanyakazi mwenzake kuna limit), ungefanyaje? Manongezi yenyewe dk 5 kwenda juu.
 
Habari wana wakubwa

Kwa kweni nakuja mbele yenu kutaka msaada niko na mke wangu mwaka wa 8 sasa na tumebahatika kupata watoto 2 wa kike na wa kiume.

Kwa hakika nampenda sana mke wangu kwani tumetoka mbali alinivumilia kuishi na mm kipindi kigumu cha kipato changu kua pia kwa kunizalia watoto.

Shida ni kua mke wangu kila siku tunakwaruzana kisa simu akiona simu inapigwa yeye ataikimbilia akiona jina la mwanamke basi anaweza kuipokea ili ajuwe ni nani au anataka musikilize shirika ukimalize aanze kuhoji huyo ni nani na anatala nn? Ukimiambia kua ni rafiki hakuelewi hapo ataanza oooo unawana wake kwa kua siku hizi una kazi kila nikijitahidi kumuelewesha basi hakubali ananiona kicheche

Hadi naiona ndoa haina amani mpaka natamani hata kutoa maamuzi mabaya ila tatizo watoto wangu bado wadogo nimekua namchoka kwa kutokuniamini hadi maneno machafu yanamyoka hutamani kumpiga ila najihisi nitamuonea.

Mimi simu yake sishiki wala sifuatiliii maana sioni sababu na nimemnunulia simu mbili ila anaweza akazifungia hata wiki eti hazina chaji wakati nyumbani pana umeme namtilia salio kwa mwezi basi unaweza kuisha mwezi bila ya yeye kutumia hilo salio.

Kwa kweli nampenda sana ila kuacha kutumia simu kwa ajili yake siko tayari kwani kazini kwangu kia na simu ni jamabo la lazima .

Hamna watu nawachukia kama wanaodai eti wanalinda ndoa kwa ajili ya watoto wao huo ni upuuzi na uwongo uliopitiliza. Upo hapo kwasababu bado unampenda jaribu kumbadilisha, ikishindikana basi kubaliana na ukweli ndio tabia ya mwenzi wako na maisha ya endelee.
 
Huyo MKEO anakupenda saana na analinda maisha yako. Shukuru Mungu kwa kukupa mke mwema kama huyo. Ingekuwa huyo mke si mwema kwako, angekuwa akiona unaongea na mwanamke nayeye anatafuta kidumu pembeni. Kwa mtazamo wangu kaa na mkeo muzungumze na kama haitoshi jaribu kushirikisha wakubwa wenu wamkalishe mkeo nazani atakuelewa na atabadilika. Hilo wazo lako la kumwacha sikushauri tena never usijaribu hicho kitu ni hibilisi hilo, utatesa watoto.

Hongera kwa kupata mke mwema tena MWAMBIE MUNGU ASANTE KWA KUKUPA MKE MWEMA.
 
Inawezekana wewe ulikuwa mtu wa kuchepuka hapo awali ndio maana hana imani na wewe tena

Wanasema ukiumwa mara moja na nyoka ......
 
Hao 'marafiki' na Wife,kipi bora?...........Acha kabisa kuwasiliana nao bila sababu za msingi.
 
Back
Top Bottom