Mrusi aliyetengeneza Ak-47

Mrusi aliyetengeneza Ak-47

Big Phil

Member
Joined
Nov 20, 2019
Posts
50
Reaction score
339
Tarehe 06 August Ya Mwaka 1945, Ndege iitwayo USAAF B-29 bomber, iliyokuwa inamilikiwa na Jeshi la Anga la Marekani, ilikua chini ya uongozi wa Watu wawili waliokua wakiiongoza ndege hio kukatiza katika anga la Mitaa fulani ya Japan.

Ukiwatoa Colonel Paul Tibbets, Jr (Rubani wa Ndege hio) na Enola Gay (Bomber). Ndege hio ilikua na mzigo uitwao “Little boy”. Mzigo ambao ulikuja kuleta habari nyingine kabisa katika histori ya vita ya pili ya dunia
Si unakumbuka Habari ya bomu la Hiroshima?

Sasa katika wingu hilo hilo la vita ya pili ya dunia, niruhusu na Mimi nikiwa kama Rubani wa uzi huu nikuchukue nikupeleke mpaka Urusi, ila nikuhakikishie ndege yangu haina mzigo wowote wenye madhara Kwa binadamu, Ndege Yangu ina Mzigo uitwao “Ugunduzi wa Bunduki ya Ak-47”.

Jina “AK-47” ni Kifupi cha Neno “Avtomat Kalashnikov-47”.
Neno “Avtomat” ni Neno la Kirusi lenye maana ya “Automatic
Hio namba “47” imetokana na Mwaka ambao Bunduki hio iligunduliwa, yaani Mwaka 1947.

Na Hilo neno “Kalashnikov” limewekwa hapo kwasababu ye Heshima Ya Mgunduzi wa Bunduki hio bwana “Mikhail Kalashnikov”.
Mikhail Kalashnikov aliyekuwa askari wa Kirusi, katika kitengo cha vifaru, alipata majeraha kadhaa mwilini mwake na Kuvunjika mkono akiwa vitani (WWII).

Hivyo wakuu wake wa kazi walimpa likizo ili akajiuguze.
Kwa kipindi chote alichokuwa vitani aligundua Mapungufu Makubwa yaliyokuwa kwenye bunduki zilizokuwa zikitumika na Jeshi lao. Baadhi ya mapungufu yake ilikua ni bunduki ku-Jam pale maji yanapoingia kwenye bunduki hizo.

Kwaio kipindi Mwana Anajiuguza, alijiiba Chemba Kidogo, na kuanza harakati za kusuka bunduki ambazo hazitakuwa na Mapungufu Kama Yale aliyoyaona kwa zile za kwanza.

Hizo bunduki ambazo zilikua Miyeyusho zilikua zikifahamika kama Sturmgewehr 44 (StG 44) assault rifle.

Akiwa na Cheo cha Chini sana Jeshini, ilikua ngumu kuamini kama Mikhail anaweza kutengeneza chochote lakini mwisho wa siku uwezo wa AK-47, uliwashangaza wengi.
Mikhail Alifariki 23 December 2013 (aged 94) na baadhi ya makala zinamtaja kama “The World’s deadliest inventor”.

Anaitwa hivo kutokana na Ubora wa Kile alichokigundua na Kukitengeneza, Muite Mikhail Kalashnikov.

Oya Skia, Me sifundishi watu kutengeneza bunduki na sijui kutengeneza bunduki,sasa asije mtu aka comment hapa chini,like
Mbona hujatuambia alitengenezaje tengenezaje!!?.
 
Alfa Blond ameiimba hiyo bunduki. Kwenye kibao chke cha Khalashnikov. Hiko kifaa akikishika msomali pale mogadishu basi anaona kama dunia ioo kiganjani kwake.
Kifupi madhara ya hii bunduki ni makubwa sana. Osama bi Laden alikuwa haiachi hata kidogo.
Imeleta madhara huko somalia, liberia Seara Leoni, Afganistan nk.

Afu Mikhaily mwenyewe kafa masikini.
 
Mwisho wa yote hiyo 'Little boy' , 'fat man' , 'thin man' zilibadilisha kabisa vita duniani
 
AKA 47 ni mali ya soviet si Urusi kama jamaa anavyodai. Urusi si Soviet.
Baba successor pekee was Soviet Russia Ni Russian Federation. Kwahiyo Ni urusi pekee ambao kiukweli vumbuzi nyingi zimefanyika kwao ( mikoani) hata kabla ya anguko la Soviet Russia.
Russia ndo imebeba kila baya na zuri la Soviet Russia baada ya anguko Lile.
 
Baba successor pekee was Soviet Russia Ni Russian Federation. Kwahiyo Ni urusi pekee ambao kiukweli vumbuzi nyingi zimefanyika kwao ( mikoani) hata kabla ya anguko la Soviet Russia.
Russia ndo imebeba kila baya na zuri la Soviet Russia baada ya anguko Lile.
Bwashee ni hivi, Ukawa wangelijenga ofisi then ikasambalatika kama ilivyo sasa hiyo ofisi isingelikuwa Mali ya Chedema et kwasababu Chedema a
Ilikuwa na mtaji wa mkubwa na webunge wengi.
Back to the Topic.
Hadi leo kila Nchi mwanachama wa Soviet ana Akilimiliki ya kufyatua hayo mabunduki bila kuhojiwa na mwenzeka.
 
AK ni noma chukua chimbia ardhini kavu kavu fukua test mtambo. Ngoma jino moja. Ni bunduki imara mno ambayo inahimili mazingira magumu. Kuna aina nyingi za AK 47 kutokana na maendeleo ya teknolojia.
Mkuu ulishawahi kuifukia then ukafukua kufanya jaribio?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu ulishawahi kuifukia then ukafukua kufanya jaribio?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Nenda you tube utaona majaribio yote ya ak kuna kutupwa kwenye tope zito na ikagonga kazi kama kawa,kuna kuchimbiwa,kuna kulowekwa kwenye maji zote hizo na walifanya hivyo kuilinganish na ile sijui inaitwa m16 carbine ya marekani
 
Back
Top Bottom