Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,398
- 14,514
Iran imerusha makombora yake ya kwanza kuelekea Israeli leo Jumatatu Machi 09, 2026 baada ya kuteuliwa kwa Kiongozi mpya mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu, Ayatollah Seyyed Mojtaba Khamenei.
Kituo cha utangazaji cha Serikali ya Iran IRIB kimesema kwenye chaneli yake ya Telegram kwamba Iran imefyatua wimbi la kwanza la makombora chini ya Ayatollah Mojtaba Khamenei kuelekea maeneo yaliyokaliwa.
Imechapisha picha ya kombora lenye kauli mbiu "Kwa Amri Yako, Sayyid Mojtaba," marejeleo ya kidini ya madhehebu ya Kishia.
Wakati haya yakijiri, Waziri Mkuu wa Qatar na Waziri wa Mambo ya nje, Mohammed bin Abdulrahman Al Thani ametoa wito wa kupunguzwa kwa kiwango cha vita vya Iran.
Akiongea na Sky News Al Thani amesema hawakutarajia mashambulizi ya jirani yao Iran dhidi ya nchi za Ghuba, akiongeza kwamba uhalali na visingizio vya Tehran wanavyotumia vimekataliwa kabisa.
Wakati huo huo shambulizi la droni lililofanywa ana Iran nchini Bahrain limewajeruhi raia 32 katika kisiwa cha Sitre.