Mrisho nyuma!

Sinai

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2011
Posts
288
Reaction score
47
Wadau, jana niliwaombeni ushauri juu ya binti ambaye alikuwa mchumba wangu, lakini hakuwa mwaminifu, alilala kwa mwanaume mwingine toka ijumaa hadi jumapili na baadae kuja kuomba msamaha!

Leo, nataka kuwapa feedback-kwanza ile jana dada wa binti alijitahidi mpaka akaonana na mimi japo nilijitahidi sana kujenga mazingira ya mimi kuto kukutana na yeye, alipo fika tukaongea kwa kirefu juu ya mdogo wake, na yeye alikiri kwamba mdogo wake hakuwa mwaminifu, lakini wamekwisha mweka chini na wamemsema sana! Nikamwambia nashukuru kwa kulitambua hilo kwani hata mimi nilienda pale hostel bila taarifa kwani nilisha pata hizo habari za yeye kutoka kila ijumaa, hivyo nikamwambia mimi basi tena! Akajitahidi sana kunishawishi nibadili msimamo, lakini nikamgomea!

Leo hii, binti amewahi ofisini kwangu kuliko hata mfagia ofisi, nakuja nimemkuta amekaa nje ananisubiri, alipo niona tu akaanza kulia na kunishika miguu eti nimsamehe, nikamtimulia mbali, akaenda kwa bosi wangu (ni mama) kumwelezea kila kitu, amemwomba eti amsaidie kunisii mimi nimsamehe, eti ni marafiki zake walimdanganya, hata kaa arudie tena! Na ameomba sana hili swala mama yake asijue, eti anapressure anaweza kupata matatizo! Sasa huyu mama amesema niende ofisini kwake saa 8, na anaonekana anataka kunishawishi nisamehe, na mimi sipo tayari kusamehe, wadau ushauri wenu please!
Binti bado yupo hapa around, yupo kama amechanganyikiwa tena sana, kiukweli nimemsaidia sana yeye na familia yake kiuchumi, tangu akiwa kidato cha tano hadi sita, then first year hadi sasa yupo third year!
 
Ushauri ulishaupata toka jana, kilichobaki ni FOLLOW YOUR HEART.
Waweza mwambia akupe a week ili u-sort mawazo yako na moyo wako vizuri; maana waweza ruka mkojo ukakanyaga mavi. lakini hakikisha anapima kwa miezi 3 mfululizo afya yake chini ya usimamizi wako.
 
bliv me wewe ni mwanaume and let ur word be definate....sasa huyo mama kamsikilize lakini msimamo ni kwamba wewe hurudi nyuma. count ur losses sasa mapema.
 
Fanya uchunguzi ujue ka ana mabwana wengine na malinda bdo yapo.
 
Ndiyo mademu wengi walivyo, kameishatumika na kupigwa chini ndo kanakukumbuka..! Wee kamwaga mavi tu hivi vitoto njaa njaa kama hivi mimi nina uzoefu navyo..!
 
::
Muda! Muda! Muda!
Muda ni silaha njema ktk maamuzi yanayohusu maisha yako yote.
::
Nenda ofisini,,then sikiliza.Omba Muda.
Ni jambo pekee litakalokupa thamani ya uamuzi utaochukua.
=
 
Msamehe!halafu waombe wakupe kama miezi mitatu utafakari cha kufanya kwenye mahusiano yenu.baada ya muda huo, follow your heart
 
Mkuu achana nae pole pole,mwambie umemsamehe lakini mfanyie vitimbi mpaka akukimbie hafai kuwa wife
 
Kuna aliyepost hapa kwamba jamaa alimsomesha hadi university na sasa hampendi tena maana kampata mwingine sharobaro. Hawa ndivyo walivyo. Mpe nafasi ya kutafakari kama wiki mbili apoe. Then usimwambie kama umemtosa. kimya kimya vile
 
Msamehe kwa usaliti wake lakini mwambie swala la kurudiana naye akupe muda mrefu halafu muda huo utumie kukata mawaasiliano naye ya simu uwe bussy na mambo mengine halafu polepole atazoea,ataona heri aendelee na anaokwenda kuwahudumia.Ni jambo hatari kama anakusaliliti kabla hamjaoana na umesema umekuwa ukiambiwa kila ijumaa huwa anakwenda kupata kitoweo,huyo ni tabia yake.

Usikutane naye kimwili hujui huko alipewa ujira gani kaswende,UKIMWI,gono,nawe kakuletea,mwanamke malaya hafai kuolewa atakutesa,au unataka mkeo awe CHAWOTE? Ndo maana kwenye torati mwanamke akizini alipigwa mawe mpaka kufa.Ila familia yake unaweza kuendelea kuwasaidia kama unavyoweza msaidia mtu mwingine.




 
Uamuzi sahihi ni wako wewe. Somewhere nyuma ya ubongo unajua jibu sahihi.

Kwa uhakika ni kuwa hutamwamini tena kama awali na hiyo itapelekea wewe kumchukulia tofauti pengine hutompenda tena kama zamani. Lakini huwa kuna kale kamsemo once a cheater always a cheater......but hey watu husameheana hasa kama kile mlichonacho kati yenu kinanguvu zaidi.
 
Lakini jamani mm sijui nikoje, hivi kweli mtu mkosaji huwa hapewi nafasi ya kujutia?? na kama akikiri kosa lake haruhusiwi kusamehewa tena bila masharti??

binti alikosea sawa tena sana, ila kama ametambua kosa lake na kukiri sion sababu ya kutomsamehe na istoshe wewe ni mwanaume nakuakikishia huwez kukutana na mwanamke malaika kwamba hatakaa akukosee.

huwa naamin zaid katika mtu kukiri kosa na kutubu na kubadilika, na bora mtu anayetubu na kuomba msamaha kwa kumaanisha kuliko mtu anayejificha kwenye kivuli cha wema ilihali ni mkosaji. nmtu anayekosa na kukiri kwa kumaanisha basi huyu yuko prone to kubadilika kuliko anayeyaficha makosa kwa kivuli cha wema.

anyways fuata myo wako kwan mm huwa nikoe mtu wa tofauti sana.
 
Dah.......ninavyodhani....... kama angekuthamini asingemfunulia mwanaume mwingine.......tena kulala huko huko...... Huyo ni changudoa........

Moyo wangu umeruka nikawaza mengine....................!
 

Dah inauma sana, embu fikiria,(Hesabu vizuri) 1. Ijumaa, 2. Jumamosi, 3. Jumapili. Yaani hajarudi anampa jamaa mambo anajipakulia tu vitu...... Bora ingekuwa siku moja tena dk kadhaa tu....................!:whoo::whoo::whoo::whoo::whoo::whoo::whoo::whoo:
 
Angalia ni mema mangapi kafanya na mabaya mangapi kafanya halafu angalia moyo wako unakwambia nini,ungekuwa unaweza kupata ruhusa kazini basi tumia wasaa huo wa kuongea ana Boss wako kuomba ruhusa na nenda mahali kapumzike bila bughudha na utakaporudi utakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuamua nini cha kufanya,kumbuka kuwa kilevi chochote kwa sasa hakina nafasi wala aina yoyote ya mwanamke wa kukufariji hana nafasi.
Pole sana kwa yaliyokukuta.
 
Kama moyo wako bado upo kwake, take time kutafakari, sali kulingana na imani yako umwombe Mungu akuoneshe uamuzi unaofaa..
Soma Yohana 8: 3-11.
 
Kwanza pole sana maana kusalitiwa kunauma kupita kiasi,kumbuka siku zote usichukue maamuzi wakati unahasira tenga muda kwanza,naamin anastahili kusamehewa na kumpa second chance.Mwambie akupe muda kama 1month hivi utulize akili na fikra halafu unaweza kumwita na kuongea naye taratibu.Jambo la msingi mpe second chance maana hebu fikilia wewe ni binadamu na unaweza kufanya kosa kubwa zaidi ya hilo,swali je usisamehewe?.Maandiko yanatukumbusha samehe saba mara sabini,pia usiacha kumshirikisha mungu na kumuuliza akujibu kama ndie aliyekuchagulia au sie,kamwe usitumie akili zako kuamau hatima ya maisha yako,kama utaweza funga na zama kwenye maombi lazima upate majibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…