Mrembo hataki kulea mimba

Mrembo hataki kulea mimba

Mtonyi

Member
Joined
Feb 28, 2013
Posts
11
Reaction score
4
Helo wana jamii amani iwe nanyi,mimi ni mwanaume ambaye nimekuwa katika mahusiano ya kimapenzi na binti mmoja kwa muda wa miaka 2, nampenda sana na December mwaka huu nilitaka kumwoa.Wiki tatu zilizopita alinieleza kuwa ni mjamzito na haikunipa shida maana niliona ni jambo la kheri.Lakini cha ajabu alinieleza msimamo wake kuwa anataka kutoa hiyo mimba na nilikataa kukubaliana nae na kumwambia kuwa akitoa asahau kuwa na mimi.Baada ya hapo alikubaliana nami kuilea,lakini baadae akawa hataki kuzungumzia chochote juu ya ujauzito wake pindi nilipotaka kujua maendeleo yake na ukafika wakati akawa hapokei simu yangu na akawa hapatikani na hata akipokea simu hunijibu kauli mbaya jambo lililonipa wasiwasi wa kuwa huenda ametoa.Wiki iliyopita alikuwa anakata simu na wakati wote simu ilikuwa inaita tuu jambo lililonipa hasira ya mimi kutomtafuta tena mpaka sasa ni siku ya 3 sijaongea naye na yeye hajanitafuta.Naomba ushauri wenu ili nijue kama bado au ametoa hiyo mimba maana mimi nipo Dar na yeye yupo Mwanza likizo.
 
Mimba zinakuja kwa style mbalimbali. Kuna nyingine mke akiwa na mimba anapenda sana kuwa na mme wake na nyingine hataki kumuaon kabisa. La muhimu ni kujaribu kuongea naye kwa hekima sana. Kuhusu kujua kama katoa au la inabidi umtafute mtu aliyeko karibu yake ahakikishe.
 
mbona kila kitu kipo wazi?hivi mtu ana mimba yako anaweza kukata mawasiliano bila sababu?
 
Mmmh... Kwanza unahakika hiyo mimba ilikuwa yako?
 
Mkuu hapo inabidi uwe makini kidogo...hiyo mimba inawezekana siyo ya kwako, ndiyo maana kakomaa kuitoa..aiseee!!
 
Nenda Sumbawanga wakaihamishie mimba kwako akikaribia kuzaa inarudi kwako.
 
Pole sana Mkuu kwa kumpoteza mwanao kwa mazingira yanavyoonesha.

Kwa nini baadhi ya wadada wana roho katili kiasi hicho lakini? Bahati mbaya wanatafsiri mtu ni aliyezaliwa tu. Wamepotoka akili na ufahamu wao. Mtu ni Nafsi na sio mwili, Mimba ikishatungwa tayari ni Mtu hai awe na wiki mbili au miaka 100 tofauti yao ni maumbile tu na akili, ila ana nafsi hai kabisa. Huo ni uuaji mbaya zaidi kuwahi fanywa na mwanadamu aliye na akili na ufahamu.

Kweli inaingia akilini kuua mwenzako(mimba) ili jamii ikuone decent? Kwani hiyo jamii ni safi kiasi gani bandugu? mbona hao mnaotaka wawaone decent nao ni wachafu kuliko wewe?? endeleeni tu kutoa, lakini ipo siku mtatoa hesabu ya hao watu/nafsi hai mlizoua. a

Hivi ingekuwaje mama yako angefanya hivyo, sio ndio wewe ungekufa? then mbona mwasema mimba changa sio mtu kamili? Kwani hiyo nafsi yako ambayo ndio wewe ilikuingia baada ya kuzaliwa? kwani kuua si kutenganisha mwili na nafsi??? Tafadhalini sana dada zetu, Hakuna uasi mkubwa kwa Mungu kama kutoa Mimba!!
 
mbona kila kitu kipo wazi?hivi mtu ana mimba yako anaweza kukata mawasiliano bila sababu?

Well said.. Coz kama anamalengo mazuri na mhusika, sion sababu ya kumfanya huyo dada kufanya hivyo...

There is something fish going on.. Hawezi kung'ang'ania kutoa bila sababu za msingi. Watch out gentlemen!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
kungekuwa na uwezekano wa kuuziana, ningemuomba aniuzie mie hiyo mimba maana nahitaji sana mtoto.
 
yaani sie tukushauri kama keshatoa mimba ama bado? tutajuaje sasa? Kongosho, njoo utabiri hapa nakuja na jogoo
 
Last edited by a moderator:
Hashuo tuu alitaka kukujaribu,sasa kakuona umeshikilia Kama ruba ndio hana jinsi zaidi ya vituko,angekua na mimba kweli ungetia akili kwa style hiyo yako, jenginee punguza speed kidogo umchunguze huyo binti usije chamba -----....
 
Back
Top Bottom