Mrembo aikosoa Serikali ya Awamu ya Tano

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,769
Reaction score
288,284
Mrembo aikosoa Serikali ya Awamu ya Tano

20374680_10155600890359339_2535330084660106730_n.jpg

By Mwandishi Wetu, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Mwanamitindo wa kimataifa, Tausi Likokola ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kufanya vizuri katika mapambano dhidi ya rushwa, lakini ameikosoa kwa kuzuia uhuru wa kujieleza.

Likokola, ambaye ni mwanamitindo aliyewahi kushiriki maonyesho makubwa ya mavazi duniani kama Gucci, Escada, Tommy Hilfiger na Christian Dior, amesema anasikitishwa na hali ilivyo nchini, akitoa mfano wa tukio la hivi karibuni la mwanasheria Fatma Karume kuzuiwa kuzungumza na waandishi wa habari.

Katika taarifa aliyoitoa jana, Likokola amesema Tanzania inasifika kwa amani duniani, lakini matukio kama hayo yanaitia doa na kwamba, anatamani kuona demokrasia ikichanua.

“Natambua kazi inayofanywa na Serikali ya kusafisha rushwa na kuwapa Watanzania maisha bora, lakini hayawezi kuwa bora kama watu hawatapewa uhuru wa kujieleza,” anasema Likokola ambaye ni Mtanzania anayefanya kazi zake nchini Marekani.

Tukio jingine alilolitolea mfano katika maelezo yake ni la aliyekuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye ambaye Machi 23 alitishiwa bastola na askari kanzu waliotaka kumzuia kufanya mkutano na waandishi wa habari baada ya kuvuliwa uwaziri.

“Nilikuwa Tanzania wakati aliyekuwa Waziri wa Habari, Nape Nnauye aliposhurutishwa kurudi ndani ya gari wakati akijaribu kuzungumza na waandishi wa habari. Tukio hilo lilikuwa baya zaidi niliposhuhudia akionyeshwa bastola. Nini kinatokea kwa Tanzania yangu, amani imeenda wapi?” anahoji Likokola katika taarifa hiyo.

Anasema tukio jingine lililomshtua ni la wakili Karume aliyekuwa akimtetea mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu. Anasema alishuhudia Karume akishurutishwa kuondoka akizuiwa kuzungumza na waandishi wa habari waliokuwa wamemzingira.

Likokola alisema anasikitishwa na magereza kutumika kuwatisha watu badala ya kuwahifadhi wafungwa.

“Nadhani uelekeo wetu si mzuri. Yapo mengi ninayoweza kueleza ambayo yamenisukuma kutoa msimamo wangu huu. Tanzania inahitaji shule bora, huduma bora za afya na miundombinu. Dunia inaona kinachoendelea, tusiende huko,” anasema.

Likokola, ambaye taasisi yake ya Tausi Aids Fund inasaidia watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi, pia anasikitishwa na taarifa kuwa wanafunzi wanaopata ujauzito, hawataruhusiwa kuendelea na masomo.

“Watoto hawa wanahitaji msaada na mapenzi yetu wazazi. Mwaka 2010 nilifanya kazi nchini Marekani ya kuwasaidia mabinti kama hao waliopewa ujauzito shuleni. Sasa wanaendelea vizuri. Tanzania tunahitaji kupendana na kufarijiana,” anasema Likokola ambaye pia ni mwandishi wa vitabu.
 
Hata rushwa bado hakuna mapambano yoyote yale ni usanii tu hasa ukitilia maanani Wabunge wa MACCM walihongwa milioni 10 kila mmoja pale Lumumba October 2016 ili wapitishe muswaada wa kuminya uhuru wa habari nchini. Na juhudi za upinzani kutaka kujua KULIKONI kuhusu hiyo rushwa imepotezewa Bungeni.

Mtaangaika sana lakini kipindi iki hakuna kukodishiwa
Nyumba au kuongwa magari na fedha za kifisadi!

Mrembo aikosoa Serikali ya Awamu ya Tano

20374680_10155600890359339_2535330084660106730_n.jpg

By Mwandishi Wetu, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Mwanamitindo wa kimataifa, Tausi Likokola ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kufanya vizuri katika mapambano dhidi ya rushwa, lakini ameikosoa kwa kuzuia uhuru wa kujieleza.

Likokola, ambaye ni mwanamitindo aliyewahi kushiriki maonyesho makubwa ya mavazi duniani kama Gucci, Escada, Tommy Hilfiger na Christian Dior, amesema anasikitishwa na hali ilivyo nchini, akitoa mfano wa tukio la hivi karibuni la mwanasheria Fatma Karume kuzuiwa kuzungumza na waandishi wa habari.

Katika taarifa aliyoitoa jana, Likokola amesema Tanzania inasifika kwa amani duniani, lakini matukio kama hayo yanaitia doa na kwamba, anatamani kuona demokrasia ikichanua.

“Natambua kazi inayofanywa na Serikali ya kusafisha rushwa na kuwapa Watanzania maisha bora, lakini hayawezi kuwa bora kama watu hawatapewa uhuru wa kujieleza,” anasema Likokola ambaye ni Mtanzania anayefanya kazi zake nchini Marekani.

Tukio jingine alilolitolea mfano katika maelezo yake ni la aliyekuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye ambaye Machi 23 alitishiwa bastola na askari kanzu waliotaka kumzuia kufanya mkutano na waandishi wa habari baada ya kuvuliwa uwaziri.

“Nilikuwa Tanzania wakati aliyekuwa Waziri wa Habari, Nape Nnauye aliposhurutishwa kurudi ndani ya gari wakati akijaribu kuzungumza na waandishi wa habari. Tukio hilo lilikuwa baya zaidi niliposhuhudia akionyeshwa bastola. Nini kinatokea kwa Tanzania yangu, amani imeenda wapi?” anahoji Likokola katika taarifa hiyo.

Anasema tukio jingine lililomshtua ni la wakili Karume aliyekuwa akimtetea mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu. Anasema alishuhudia Karume akishurutishwa kuondoka akizuiwa kuzungumza na waandishi wa habari waliokuwa wamemzingira.

Likokola alisema anasikitishwa na magereza kutumika kuwatisha watu badala ya kuwahifadhi wafungwa.

“Nadhani uelekeo wetu si mzuri. Yapo mengi ninayoweza kueleza ambayo yamenisukuma kutoa msimamo wangu huu. Tanzania inahitaji shule bora, huduma bora za afya na miundombinu. Dunia inaona kinachoendelea, tusiende huko,” anasema.

Likokola, ambaye taasisi yake ya Tausi Aids Fund inasaidia watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi, pia anasikitishwa na taarifa kuwa wanafunzi wanaopata ujauzito, hawataruhusiwa kuendelea na masomo.

“Watoto hawa wanahitaji msaada na mapenzi yetu wazazi. Mwaka 2010 nilifanya kazi nchini Marekani ya kuwasaidia mabinti kama hao waliopewa ujauzito shuleni. Sasa wanaendelea vizuri. Tanzania tunahitaji kupendana na kufarijiana,” anasema Likokola ambaye pia ni mwandishi wa vitabu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nani anamjua Tausi Likololo Tz au na yeye ndio anatafuta kiki ?
Ah! Man, usiniambie na wewe umekuja juzi kutoka Kolomije manake vijana wa mjini, husuani wapenda mambo ya mjini na walimbwende, sote wanamfahamu Tausi!!! Au unajifanya humjui kwa vile amepiga Magogoni?!

Sema dah, kitambo sana...
 
Huyu ana pesa yake ndefu wewe, hahitaji kuhongwa na yoyote yule wala kukodishiwa gari. KAMWE usimfananishe na Warembo uchwara.

Mtaangaika sana lakini kipindi iki hakuna kukodishiwa
Nyumba au kuongwa magari na fedha za kifisadi!
 
Hili linaweza lisiwapendeze watu lakini ukweli ni kwamba idadi kubwa ya diaspora inakubali kazi ya Magufuli kunyoosha nchi, tatizo ni economic na social policy. Ata ivyo wengi wanaamini hayo yatafuata muhimu ni watu wanyooke.

Sasa uelewi kwanini polisi wanatumia nguvu nyingi penye mapungufu akosolewe ndio demokrasia.
 
Huu utafiti uliufanya lini na katika nchi zipi duniani ambapo kuna Watanzania? Hebu tuwekee na ukubwa wa sample yako ukilinganisha na idadi ya Watanzania waishio nchi za nje?

Hebu tuambie na nchi inanyooshwaje? Au ni kupitia huu udikteta uchwara ndiyo wewe unaona nchi inanyooshwa!?

Hili linaweza lisiwapendeze watu lakini ukweli ni kwamba idadi kubwa ya diaspora inakubali kazi ya Magufuli kunyoosha nchi, tatizo ni economic na social policy. Ata ivyo wengi wanaamini hayo yatafuata muhimu ni watu wanyooke.

Sasa uelewi kwanini polisi wanatumia nguvu nyingi penur mapungufu akosolewe ndio demokrasia.
 
Back
Top Bottom