Mrema na Sharrif walirudisha kadi za CCM?

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,954
22,125
Jamani kuna mtu amenigusa kidogo kwa kunihakikishia
hawa mabwana apamoja na fighting yao ccm awakuwahi kurudisha
kadi za CCM walipoamua kukiama
hawa si wahaini wa kisiasa kweli???
 
mi nimechoka kabisa

sijui nkimbilie wapi jamani...yaani huy haramia alipokuwa anatunyanyasa
2005 na watu kuacha kazi zetu ,,kweli ujafa ujaumbika
 
Tokea Augustine Mrema alipopelekwa India kutibiwa kwa msaada wa Rais Kikwete,hatujui sasa Mrema yuko Chama gani,kama yupo TLP au CCM,au kama yupo katika upinzani au vipi.
Kwa hiyo,ingefaa sasa Ndugu Mrema angetuambia yupo Chama gani. Kwa sababu Mrema sasa hawezi kuvumilia kuona mtu yoyote anampinga Rais Kikwete,sasa Uchaguzi Mkuu utafanyika vipi kama watu wasipojitokeza kumpinga Rais Kikwete? Mrema anawakumbusha watu kwamba yeye aliwahi kuwa shushushu,na kwamba hata sasa labda bado ni shushushu,kwa hiyo,hataki kuwasikia watu wanampinga Kikwete. Hii ina maana gani,kwamba CCJ wawakatate watu wote wanaokuja kwenye Chama chao kutoka CCM?
Sasa hivi kuna Uchaguzi,Mrema anaweza vipi kuuliza kwa nini Butiku aliongea maneno kumpinga Rais Kikwete?Ndio maana tunasema kwamba Rais akichaguliwa,ni watu wachache tu wanafaidika,ndugu zake,rafiki zake,na watu wengine wachache. Sisi wengine,faida tunayopata ni barabara tu ambayo tunaweza kupita,kama tunayo nauli ya kupanda daladala. Sisi hatutaki mtu aliyepata msaada wa kwenda India kutibiwa,atufundishe jinsi ya kupiga kura. Sasa mtu anachaguliwa na Rais kuwa Waziri,kuwa Mkuu wa Mkoa,kuwa Mkuu wa Shirika;unategemea huyu mtu atasema nini? Atasema,''Nani mwingine zaidi ya Kikwete.'' Lalini sisi siyo lazima tumsikilize mtu kama huyo.
Kama watu watamchagua Jakaya Kikwete katika Uchaguzi ujao,sawa,lakini mimi hakufanya vema kutsahili kuchaguliwa tena. Amefanya vema,lakini siyo vema kustahili au hata kulazimisha kuchaguliwa tena.
Jambo muhimu katika Uchaguzi nadhani,mtu unatakiwa tu kumchagua yule ambaye unadhani atashinda,siyo yule unayetaka ashinde,mpiga kura anatakiwa tu kuonyesha anayoi akili ya kujua ani atashinda,na kumchagua huyo.
 
Waulizeni wenyewe live waseme wapo upande upi? Si mnafika kwenye mikutano yao au ofisi zao? na simu zao labda pia mnazo?
 
Back
Top Bottom