Mrema: CCM isilinde mawaziri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mrema: CCM isilinde mawaziri

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Jan 26, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,346
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280

  Mrema: CCM isilinde mawaziri

  Imeandikwa na Hellen Mlacky; Tarehe: 26th January 2011 @ 07:50

  Chama Cha Mapinduzi(CCM) kimetakiwa kuacha kulinda mawaziri wake wanaotoa kauli tata na kukinzana na Serikali yao.

  Mwito huo umetolewa na Mbunge wa Vunjo, Augustino Mrema (TLP), alipozungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana.

  Mrema ambaye pia ni Mwenyekiti wa TLP, alisema haiwezekani mawaziri watofautiane kauli, kisha waendelee kubaki serikalini.

  Ingawa hakuwataja mawaziri hao, lakini siku za hivi karibuni suala la Kampuni ya mitambo ya kufua umeme ya Dowans, imesababisha malumbano miongoni mwa wanasiasa wakiwamo mawaziri.

  Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kibiashara (ICC) hivi karibuni ilitoa hukumu kwa kesi ya madai iliyofunguliwa na Dowans dhidi ya Tanesco na kuamua shirika hilo la umeme nchini, liilipe kampuni hiyo Sh bilioni 94 kwa kuvunja mkataba wake.

  Suala hilo lilizua mjadala pale Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alipotangaza kuwa Serikali italipa fedha hizo baada ya kuwasiliana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

  Ndipo Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, walipompinga hadharani wakisema si vyema fedha hizo kulipwa kwani utakuwa mzigo kwa wananchi.

  Hali hiyo ilionekana kumkera Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, Mathias Chikawe, ambaye alisema viongozi hao wamekiuka maadili ya uwajibikaji wa pamoja, kwa kutoa siri za Baraza la Mawaziri na kutaka kama wanataka kuisema Serikali basi wajitoe kwanza.

  “CCM haiwezekani mawaziri watofautiane kauli katika masuala mbalimbali likiwamo la Dowans lakini wanaachwa, mimi enzi hizo nilitimuliwa mbona wao wapo wengi wenye tabia kama za Mrema, lakini hamuwaondoi?” alihoji Mrema.

  Mwaka 1995 Mrema alitimuliwa uwaziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana chini ya uongozi wa Rais Ali Hassan Mwinyi, baada ya kudai kuwa Serikali ilikuwa inamkingia kifua mfanyabiashara Chavda.

  Alisema “CCM ina upendeleo, hivyo sisi wapinzani tumepata nafasi ya kuungana sasa, tusiitane majina na wala mtu asihukumiwe kutokana na makosa yake ya nyuma, bali tuheshimu walichokichagua wananchi”.

  Aliwashauri wapinzani kuungana na kuwa kambi moja, kwa sababu wananchi watawahukumu kwa michango yao bungeni.

  Alisema kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi ambayo ina majimbo mawili ya Vunjo na Moshi Vijijini, wapinzani wameungana hivyo ni vyema pia nao wakaungana kitaifa.

  Akizungumzia matatizo yanayolikabili jimbo lake, Mrema alisema ni uvunjifu wa amani unaosababishwa na wizi na uporaji unaofanywa na vibaka, wezi na majambazi hali inayofanya watu kuvunjiwa nyumba na kuporwa fedha na mali zao na wakati mwingine kusababisha mauaji.

  Mbunge huyo alisema tatizo lingine ni hali mbaya ya kiuchumi kwa wananchi ambayo imedidimia, ikilinganishwa na miaka ya nyuma, kwani kwa sasa bei ya kahawa imeshuka na mibuni inashindwa kuzaa kwa viwango kutokana na uzee.

  Kutokana na matatizo hayo, Mrema alisema wameunda Kamati ya watu 10 ili kuratibu maendeleo ya Vunjo na kuandaa na kusimamia uanzishwaji wa miradi ya maendeleo.


   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,346
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  Tatizo la Mrema ni upeo finyu..................................ufisadi wa nchi wote hupikwa IKulu.................Mawaziri kama akina Ngeleja ni vibaraka tu wapo pale kulinda ugali wao.................hata ukiwawajibisha na kumwacha JK ni kazi bure kabisa........................
   
 3. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #3
  Jan 26, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Nini msimamo wake kuhusu DOWANS? Inaelekea yeye anaungana na Kamati Kuu ya CCM kwamba DOWANS walipwe
   
Loading...