Mrema atua Loliondo kuimarisha afya yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mrema atua Loliondo kuimarisha afya yake

Discussion in 'Celebrities Forum' started by fangfangjt, Mar 14, 2011.

 1. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  Adai amekunza dawa kupata nguvu ya kupambana na mafisadi - source Mwananchi


  UPDATE


  MWENYEKITI wa TLP, Augustine Mrema, ametinga Loliondo kwa Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Ambilikile Mwasapile kunywa dawa na kutamba ni kwa ajili ya kuongeza nguvu ya mwili kupambana na ufisadi.


  Mrema, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), alisema jukumu alilokabidhiwa kuzunguka nchi nzima ni kubwa linalohitaji kuimarisha afya yake.

  "Kazi niliyokabidhiwa ni kubwa, kuzunguka nchi nzima kupambana na ufisadi kunahitaji kuimarisha afya yangu," alisema Mrema na kuongeza:

  "Bila kuimarisha afya huwezi kufanya kazi hii niliyokabidhiwa, waeleze Watanzania kuwa nimeimarisha afya sasa nikupambana na mafisadi kwenye halmashauri nchini kwa kwenda mbele."

  Alisema Watanzania wanatakiwa kumshukuru Mungu kwa ‘kuwashushia' Mchungaji mstaafu Ambilikile Mwasapile (76), kwa sababu hawatumii gharama kubwa zaidi ya 500.

  "Kama angekuwa Marekani tungeenda kwa Sh500? dawa yake haina kuchakachua unakunywa. Dawa nimekunywa na nimerudi na picha nimepiga naye " alisema Mrema kwa kujiamini.

  Hata hivyo, Mrema hakubainisha magonjwa yanayomsumbua hadi kwenda kwa Mchungaji Mwasapile, ingawa anasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari kwa muda mrefu. Siku za hivi karibuni vigogo wengi wa Serikali na CCM wamekuwa wakienda Loliondo kwa ajili ya tiba.

  Serikali itegemee maajabu
  Profesa Ibrahim Lipumba, amesema Serikali itegemee maajabu zaidi ya tiba za asili kuliko ya Loliondo, kwa kuwa wananchi wamechoka na ubabaishaji wa sekta ya afya.Profesa Lipumba alisema hayo juzi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

  Kwa mujibu wa Profesa Lipumba, umati unaoendelea kufurika kwa Mchungaji Mwasapile ni kiashiria kwamba Watanzania wamekata tamaa na huduma za afya zinazotolewa na Serikali.

  "Ikiwa Serikali haitajali huduma muhimu za afya kwa wananchi wake, tutarajie mengi zaidi ya haya ya Loliondo," alisema Lipumba.

  Alisema wananchi wakichoka na kukata tamaa na chombo chenye dhamana ya kuwahudumia, watatafuta njia mbadala ya kujikwamua na tatizo kama ilivyokuwa Loliondo.

  Profesa Lipumba alieleza kuwa kasi ya watu kwenda kutafuta tiba mbadala kwa mchungaji, inaonyesha kuwa Watanzania wameshakata tamaa na huduma za afya zinazotolewa hospitalini.

  "Kimsingi hii ni dalili ya wazi kuwa, sekta ya afya imeshindwa kazi. vinginevyo isingewezekana watu watoroke hospitalini kwenda Loliondo," alisema.

  Profesa Lipumba alisisitiza kuwa watu kukimbia tiba za hospitali na kwenda kutafuta tiba mbadala ni aibu kwa taifa hasa kwa sekta ya afya ambayo imeajiri watu na kuwalipa mishahara kwa kazi hiyo.

  "Ni kiashirio kibaya sana kwa taifa kuona watu wakiwa wanatorosha wagonjwa wao hospitalini kutafuta tiba mbadala," alisema.

  Profesa Lipumba aliongoza kuwa umati uliojaa Loliondo unaonyesha picha halisi kuwa, Watanzania wengi ni wagonjwa, lakini sekta ya afya haina uwezo wa kuwahudumia.

  Profesa Lipumba ametoa kauli hiyo huku maelfu ya watu yakiendelea kumiminika Loliondo kupata tiba ya mchungaji huyo aliyoeleza kuwa aliigundua kwa njia ya maono.

  Ongezeko la watu wanaoelekea Loliondo limezidi hasa baada ya Serikali kubariki tiba hiyo inayotolewa katika kijiji cha Samunge wilayani Ngorongoro.

  Mchungaji, Mwasapila juzi alipongeza uamuzi wa Serikali kuondoa tishio la kuzuia kutoa dawa kwani watu wengi wamekuwa wakinufaika na dawa na mahitaji yanaendelea kuwa makubwa.

  "Tunamshukuru Waziri William Lukuvi kwa kuruhusu dawa iendelee kutolewa na kutoa ahadi ya kuleta huduma mbalimbali muhimu katika kijiji hiki," alisema Mchungaji Mwasapile.

  Chakula, malazi
  Mmoja wa wasaidizi wa mchungaji huyo, Peter Dudui alisema jana kuwa kuanza kupatikana hudumu muhimu katika eneo hilo kama chakula, vyoo na mahala pa kulala kumechangia kupunguza wimbi la vifo vya wagonjwa.

  "Sasa vifo hakuna, wagonjwa wanaokuja wanapata huduma kama chakula na maji na pia wanapata mahali pa kulala. Ingawa sehemu za kulala ni chache zinasaidia sana," alisema Dudui.

  Ijumaa wiki iliyopita, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alitangaza kuwa Serikali imeruhusu Mchungaji Mwasapile kuendelea na huduma zake za tiba na kwamba itatoa ushirikiano wa kusimamia na kujenga mazingira mazuri ya kuendelea kutoa huduma.

  Tamko hilo lilitolewa wakati ambapo tayari kulikuwepo na tetetsi kwamba Serikali imekusudia kumsimamisha Mchungaji huyo hadi hapo uchunguzi maalumu wa kitaalamu utakapofanywa kwa dawa yake.

  Tangazo hilo la Serikali ambalo limetolewa wakati bado wataalamu wa afya wanachunguza dawa hiyo, limehamasisha maelfu kwa maelfu kumiminika kupata tiba.

  Msururu mirefu ya magari yanayotoka Arusha mjini kuelekea katika kijiji hicho ambacho sasa kinaiitwa 'Kijiji cha Babu', jana ilionekana katika barabara ya Arusha hadi Ngorongoro.

  Walioshuhudia msafara huo mrefu walisema kitu kibaya walichoshuhudia kwenye msafara huo ni madereva walombele kutoruhusu wenzao wanaookuja nyuma yao kwa kasi kutokana na kila mmoja kujaribu kuwahi kufika kabla ya mwingine kunywa dawa.

  Baadhi ya watu walioshuhudia misafara hiyo, walisema ni vigumu madereva kuwaruhusu wenzao wanaokuja nyuma kwa hofu ya kuchelewa kwenye foleni ya dawa.


  Mrema atua Loliondo kuimarisha afya yake
   
 2. Mbeu

  Mbeu Member

  #2
  Mar 14, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Glory to God,kwa kumleta Babu, mzee wa Kiraracha alikuwa ana chungulia Kaburi sasa atapata nafuu ila anatakiwa aache UNAFIKI otherwise HATA PONA, anatakiwa awe na common stand, maana MUGARIGA is all about FAITH, it does not need people who SIT ON THE FENCE.
   
 3. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Shehe yahya hajaenda?!:focus:
   
 4. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  atashuka tu utamuona
   
 5. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Madai ya Lipumba kwamba umati wa watu unaofulika Loliondo kwaajili ya tiba ya Babu unatokana na kukatishwa tamaa na huduma mbovu za tiba hapa nchini siyo ya kweli; kwani baadhi ya watu ambao wameenda huko kufuata tiba hiyo, ni wale wenye fursa ya kwenda kutibiwa nje ya nchi kwa gharama ya serikali, hata kwa ugonjwa mdogo. Aidha kutokana na hadha ya usafiri iliyopo, ni watu wenye uwezo kifedha ndio ambao wameweza kufika huko na wala siyo hoi hae.
   
 6. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  kwa hiyo ina maana hata huduma za kutibiwa huko nje ya nchi hawaziamini?ee bwana hapa nimejifunza kitu kimoja kwamba imani ni jambo moja gumu sana mtu akishaamini basi kumbadilisha ni kazi sana halafu matatizo mengi ndiyo yanayotufanya tupoteze imani ila pia namsifia babu kwa kua anatoa tiba kwa gharama nafuu sana kuliko hata hospitali za serikali maana serikalini hiyo 500 haya cheti tu hupati!
   
 7. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  angalau aonyeshe hizo jitihada za kupambana na hao mafisadi basi!
   
 8. Jitihada

  Jitihada Senior Member

  #8
  Mar 14, 2011
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ila naona hii tiba ya loliondo ingemfaa sana JK, na tatizo lake la kudondokadondoka pindi awapo jukwaani,
   
 9. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #9
  Mar 14, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  umeambiwa ameshapitia huko alipoenda kutembelea nyayo za mtu wa kale wasiwasi wangu kwamba asije akawa alikunywa vikombe viwili maana babu anasema ukigonga viwili huponi!pia hawa wote wanatakiwa wauthibitishie umma kama wamepona!
   
 10. N

  Nanu JF-Expert Member

  #10
  Mar 14, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kweli Imani inaponya! Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika!
   
 11. Jitihada

  Jitihada Senior Member

  #11
  Mar 14, 2011
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Du, kama JK kanywa mbona amekunywa kisiri sana? haoni wapinzani wenzake akina mrema wanavyoutangazia umma baada ya kunywa! mi sikusikia kama mkwere nae kanywa! Anyway kutakuwa na agenda ya siri hapa juu ya unywaji wake
   
 12. k

  kisukari JF-Expert Member

  #12
  Mar 14, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,753
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  kuna mtu namfahamu ameenda huko,sijui ni kweli maana huyo mtu ni msemaji,anasema kuna watu wana confess sasa sijui ni akili zao,wanasema wao wameua,au wamefanya mambo ya kichawi
   
 13. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #13
  Mar 14, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ni imani au dawa??
   
 14. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #14
  Mar 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,274
  Likes Received: 19,420
  Trophy Points: 280
  Mwenyekiti wa TLP na mbunge ametia timu Loliondo kwa babu kunywa dawa. Amedai anakunywa dawa kuimarishwa afya yake kuongeza nguvu ya na kupambana na ufisadi.
  "Kazi niliyopewa ni kubwa kuzunguka nchi nzima na kupambana na ufisadi na kunahitajika kuimarisha afya yangu" alisema Mrema.
  Alisema na kuongeza
  Waambie watanzania sasa nimeimarisha afya kwa hiyo kilichobaki ni kupambana na mafisadi kwenye halmashauri kwa kwenda mbele .
  source : mwananchi.co.tz
   
 15. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #15
  Mar 14, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Si ajabu kwa nchi kama yetu, ambapo serikali haijifunzi kutokana na makosa ya nyuma, ndani ya nchi au nje, Kadhalika wananchi hawajifunzi kutokana na makosa ya nyuma! DECI (Ponzi scheme) bado iko mahakamani, tumejifunza nini?, Sheikh Yahya na utabiri usio na miguu, n.k! nchi imekuwa ya maruhani na miujiza ambayo hazihojiwi! Tukiishi bila ya kufikiri na kuhoji, we are doomed to fail in the road ahead.
   
 16. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #16
  Mar 15, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mabaka yake sasa yatakwisha! Mzee amekua km chatu! Duh!
   
 17. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #17
  Mar 15, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,022
  Likes Received: 8,504
  Trophy Points: 280
  Hiyo dawa expire date yake mwilini dakika ngapi?alafu huo mmea ziko hekari ngapi za kutosha kuchemshia dawa watu?
   
 18. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #18
  Mar 15, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mrema nanashuhudia tbc, miujiza ya babu, eti anashauri serikali ianze kutoza kodi kwa watu toka nje ya nchi, na kutoa mfano wa biligate, mchango wake ni vituko tupo plz watch
   
 19. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #19
  Mar 15, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,274
  Likes Received: 19,420
  Trophy Points: 280
  kwanza kapona?? Na huyu si kesho anaongoza maandamano ya ccm?
   
 20. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #20
  Mar 15, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  anataka roliondo kwa babu pafanywe kituo cha utalii ili wageni wanaotoka nje walipe ili serikali ipate kipato.
   
Loading...