Mrema Atoswa na Wanakamati wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mrema Atoswa na Wanakamati wake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Said Bagaile, Jul 21, 2011.

 1. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wanajukwaa nimesikia kupitia mapitio ya magazeti kupitia East African Radio kwamba Mh. Lyatonga amemwandikia Spika barua kuwashtaki Wanakamati wake kwamba toka kuanza kwa vikao vinavyoendelea vya Bunge, hajawahi kukutana na Wanakamati wake!

  Kama hivyo ni kweli, inaonekana Wanakamati hawa walitegemea kwamba Wanapoingia kwenye hizi Kamati huwa kunakuwa na Rushwa wanayopewa ya kuwaziba mdomo pindi wanapokutana na Madudu huko wanapokwenda kukagua.

  Sasa wamekuta Mzee wa Kiraracha kumbe yeye ameamua kufanya kazi na anahakikisha hakuna Rushwa inayopokelewa, sasa jamaa Wamevunjika moyo wa kufanya kazi na Mtu "Mnoko" kama Mrema ndio maana kila akiwahita wakutane hawatokei.


  CCM bila Rushwa Haiwezekani!


   
 2. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Napita tu.
   
 3. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Ataendesha vikao saa ngapi wakati muda mwingi anachapa usingizi hadi kumwaga udenda!
   
 4. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #4
  Jul 21, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  uchaguzi mdogo Vunjo lini tukachukue jimbo letu
   
 5. N

  Nangetwa Senior Member

  #5
  Jul 21, 2011
  Joined: Feb 9, 2009
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huu nafikiri ni umbea. taja hilo gazeti tukasome wote. Na hilo swala la rushwa umechomekea na sijua kuwa lina uhusiano.
   
 6. m

  marembo JF-Expert Member

  #6
  Jul 21, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mrema mpinzani tangu lini? Hivi chama chake kipo au? Tumeona vituko vyake kwenye uchaguzi kwa kuwataka wananchi wampe kura JK wakati TLP imesimamisha mgombea.

  Tufike mahali tuuchoke na kuuchukia unafiki wa wazi. Sasa ndio anaona ametoswa? Mikutano tu ya bunge inamshinda kwa kuzidiwa na usingizi sembuse muda wa vikao vya kamati.

  Kila masika na mbu wake: Mrema huyu si yule wa enzi zile za NCCR.
   
 7. n

  nyamagaro JF-Expert Member

  #7
  Jul 21, 2011
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Mkuu Nangetwa, Nadhani wewe ni mbea kuliko wote. Unawezaje kumhukumu mwenzako mbeya wakati amekupa source ya habari, shame on you lazy guy who doesn't want to make his brain work. Soma mwananchi la leo upate ghabari nasiyo unakurupuka kama kima.
   
 8. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #8
  Jul 21, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Kaka watu hukurupuka na wanataka kuongeza posts tu hapa amabazo hazina maana.JF kuna makenge kibao with no brain na hao tunawaona kwa njia hizi hizi wanakurupuka tu na madai mfu .
   
 9. dazu

  dazu JF-Expert Member

  #9
  Jul 21, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 365
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nahuzunishwa na lugha tunayoitumia kukosoana siku hizi. Najiuliza siku tukiitwa kikao tukafahamiana sijui itakuwaje!!!
   
 10. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #10
  Jul 21, 2011
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Na wewe sijui mtaangaliana vipi na mnyama wa Gombe
   
 11. F

  FJM JF-Expert Member

  #11
  Jul 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  Tuhuma za baadhi ya wabunge kujihusisha na vitendo vya rushwa zimeendelea kulitikiza bunge na sasa zinatishia kuisambaratisha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) inayoongozwa na Mbunge wa Vunjo (TLP), Augustine Mrema
  .

  LAAC ni kamati ambayo ilijizolea sifa nyingi kwa jinsi ilivyoanza kazi yake kwa kasi ambapo baadhi ya watendaji wa Halmashauri za Mkoa wa Kilimanjaro, waliamriwa kukatwa asilimia 15 ya mishahara yao baada ya kushindwa kutoa maelezo ya kuiridhisha kamati hiyo ilipofanya ukaguzi wa matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo mkoani humo.

  Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi na kuthibitishwa na Mrema mwenyewe umebaini kuwa tangu kuanza kwa mkutano wa nne wa Bunge la bajeti, Juni 5, mwaka huu, Kamati ya LAAC imeshindwa kukutana licha ya mwenyekiti, Mrema kuitisha vikao hivyo mara tatu kwa nyakati tofauti.

  Mrema aliliambia Mwananchi jana kuwa kutokana na hali hiyo ya wajumbe kutofika kwenye vikao kwa ukamilifu, anakusudia kuwasilisha taarifa hiyo kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda ili kupata mwongozo wa jinsi ya kuiwezesha kamati hiyo kufanya kazi.

  Kikao cha tatu kiliitishwa juzi Jumanne, Julai 19, ambacho kilikuwa kimepangwa kufanyika Ukumbi namba 231, lakini kilishindikana baada ya Mrema kujikuta akiwa na wajumbe wawili tu ambao ni Makamu Wake, Iddi Azzan ambaye pia ni Mbunge wa Kinondoni(CCM) na David Kafulila, Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR Mageuzi).

  Taarifa rasmi za Bunge (Hansard) zinathibitisha kuwa Mrema aliitisha kikao cha kwanza cha kamati yake Juni 16, 2011 siku tatu tu tangu mjumbe wa kamati hiyo Kafulila, awatuhumu wajumbe wenzake watatu kwa kuomba rushwa kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga.

  Juni 13, mwaka huu wakati akichangia hotuba ya mpango wa maendeleo wa miaka mitano, Kafulila aliwatuhumu wabunge wenzake ambao walikuwa katika kamati ndogo ya LAAC iliyofanya ukaguzi wa miradi katika baadhi ya Wilaya za mkoani Tanga kwamba waliomba rushwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.

  Katika maelezo yake Kafulila aliwataja wabunge wawili kati ya watatu anaowatuhumu kuwa ni Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi na Mbunge wa Bahi, Omary Badwel na kwamba taarifa za tukio hilo alikuwa amekwishaziwasilisha kwa Mrema na Spika wa Bunge, Anne Makinda.
  "Bahati mbaya sana ni kwamba, katika dhana nzima ya kusimamia hayo matumizi ambayo tunayapanga na kuyapitisha kuna tatizo kubwa sana la mfumo ambao una udhaifu wa kifisadi. Kuna Waziri, kuna Wabunge wanakula rushwa, nimekamata Mbunge anaomba rushwa kwenye Halmashauri wakati halmashauri ziko chakavu, wanalia njaa, mipango haiendi, nilikamata mbunge anaomba rushwa,"alisema Kafulila na kuongeza:

  "Wamo humu ndani, wapo humu kuna akina Zambi, Badwel,..... nimewakamata na nimechukua hatua, nchi hii haiwezi ikaendelea kwa style (mtindo) hiyo, haiwezekani".

  Tuhuma mpya
  Wakati wa ukaguzi wa miradi katika mikoa ya Tanga na Pwani uliofanyika Mei 22- 28, 2011, kamati hiyo iligawanyika katika kamati ndogo mbili ambapo kamati iliyokwenda Tanga iliongozwa na Mrema na ile iliyokwenda Pwani iliongozwa na Azzan.

  Habari zaidi zinadai kwamba hata kamati iliyokwenda Pwani baadhi ya wajumbe wake wanatuhumiwa kuomba rushwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, ambaye baada ya kumpigia simu alitoa taarifa kwa kiongozi wa timu hiyo, Azzan.

  Inadaiwa kuwa wabunge hao waliompigia simu mkurugenzi huyo wakimwambia kwamba awape hongo ili wasimchukulie hatua kali kutokana na halmashauri anayoiongoza kuvurunda katika miradi waliyoikagua.

  "Kamati hii ni kama imeoza, hali ilikuwa mbaya mkoani Pwani kwani wapo walioomba rushwa na huko hata kiongozi wao Azzan alijikuta katika wakati mgumu kwa wajumbe wake kumfokea kwamba anapoteza muda pale alipoonekana kuhoji kwa undani baadhi ya taarifa za utendaji,"alisema mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo.

  Alipotafutwa na Mwananchi, Azzan hakukubali wala kukanusha taarifa hizo zaidi ya kusema kuwa yeye si msemaji wa kamati na kutaka afuatwe Mrema ambaye ndiye mwenye uwezo wa kuzungumzia "mambo ya kamati".

  Kukwama kwa vikao
  Mrema alilithibitishia Mwananchi kwamba kikao alichokiitisha Juni16,hakikufanyika kwa madai ya kukosekana kwa baadhi ya wajumbe, akiwamo Kafulila ambaye wakati huo alikuwa amesafiri kikazi kwenda nchini Rwanda, akiambatana na ujumbe uliokuwa chini ya uongozi wa Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai.

  Sehemu ya Hansard ya Juni 16, 2011 inasomeka hivi; "Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Mheshimiwa Dk Augustine Lyatonga Mrema, anaomba niwatangazie Wajumbe wa Kamati hiyo kwamba, saa tano na nusu kutakuwa na kikao kitakachofanyika katika Ukumbi wa Msekwa C".

  Habari ambazo Mwananchi lilizipata na kuthibtishwa na Mrema jana zilisema kwamba kikao hicho hakikufanyika, hivyo mwenyekiti huyo kulazimika kuitisha kikao kingine Juni 20, 2011 baada ya Kafulila na wajumbe wengine kubainika kwamba wapo bungeni.

  Sehemu ya Hansard ya Juni 20, 2011 inathibitisha kuitishwa kwa kikao hicho na inasomeka; ".....Mheshimiwa Dk Augustine Lyatonga Mrema, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, anaomba niwatangazie Wajumbe wa Kamati yake kwamba, leo hii saa 7.00
  mchana kutakuwa na kikao cha Kamati katika Ukumbi Namba 227, katika Jengo la Utawala".

  Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba kikao hicho pia hakikufanyika kutokana na baadhi ya wajumbe kutofika bila kutoa taarifa, na kwamba mmoja wa wajumbe hao (jina tunalihifadhi kwa sasa) alitoa udhuru kwamba ana dharura ya msiba lakini alipoambiwa kwamba wajumbe wenzake wamchangie rambirambi alikataa.

  Kauli ya Mrema
  Kutokana na hali hiyo Mrema alisema; "Kamati siyo yangu, hii ni Kamati ya Bunge kwahiyo kwa hali hii mimi nitaomba mwongozo wa Spika maana yeye ndiye anayeunda kamati hizi kwa mujibu wa Kanuni za Bunge".

  "Hata nikisema nisiseme haiwezi kusaidia, ni kweli kwamba tuna tatizo hili na jana (juzi) niliitisha kikao wakaja Azzan na Kafulila tu, sasa hapo mimi siwezi kufanya zaidi ya hapo,"alisisitiza Mrema.

  Aliongeza: "Nikiitisha kikao, akaja Kafulila apo wengine hawaji kabisa, lakini Kafulila asipokuwepo, wengine utawaona wamefika na wengine hawaji, ni kama wajumbe wangu wamegawanyika, na hapo unakuwa huwezi kuwa na kikao kinachoweza kufanya uamuzi kwa manufaa ya nchi yetu".

  Habari zaidi zinadai kwamba tuhuma za Kafulila bungeni dhidi ya Zambi na Badwel zinawatisha hata baadhi ya wale waliokuwa katika kamati ya mkoani Pwani kwani wanahofu kwamba huenda nao wakaanikwa ndani ya kikao cha kamati hiyo ya LAAC.

  Source: Mwananchi
   
 12. Ba Martha

  Ba Martha JF-Expert Member

  #12
  Jul 21, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mkuu AVATAR yako balaa! hiyo Restaurant iko wap?
   
 13. Jidu

  Jidu JF-Expert Member

  #13
  Jul 21, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,167
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  hii imetulia
   
 14. p

  police Member

  #14
  Jul 24, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo watu hawapendi wengine wapate sifa. Mrema anafanya kazi nzuri bila yeye haya tusingeyasikia.

  Mbona dr. Slaa aliongoza kamati hii 2005 - 2010 hatusikia akikemea kitu au alikuwa nae anapewa rushwa, kwa kazi Mrema anayofanya JK amteue kuwa waziri..
   
 15. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #15
  Jul 24, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,486
  Likes Received: 5,721
  Trophy Points: 280
  Pengine tuumeanza kufumbuka sasa kumbe yale makofi yanayopigwa na zile sauti za kujibu wanaaopinga hakunaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa wanaosema ndiyo umati wa wabuneg wanajibu ndiyooooooooo nilijua ni hisia za siasa kumbe kuna bahasha zinakuwa zinaongea tofauti na kuhisi ni uccm na uchadema....kama vile aitoshi dhambi ya bahasha imeendelea kuzotauna zile kamati zetu bungeni na kujiuliza kuna kamati gani ambayo aipokei bahashaa jamani

  tulianza na kamati ya kakangu mh january makamba nayo kukawaka moto

  jana nimesoma mwananchi nimelalala hoi kamati ya mrema iinayoshugulika na hesabu za serikali za mitaa kumbe ile wanakula 150,000 kwa siku ni pamoja na hela za bahasha wanachofnya ni kuzunguka mikoa mingi waonekane wamefanya kazi kumbe wana ajenda zao binafsi..ukisoma gazeti la jana unaweza lia kamati hiyo iliparaganyika pale mh kafulila alipowataja jamaa waliodakishwa na mh mrema amesema tangu waanze bunge hili la sasa amekuwa akiita wakutane na akija mh kafulila wengine wanagoma na wakija wengine wanauliza kwanza kafulila anakuja ama ameshaingia...mh mrema amesema hana imani tena amechoka kabisa na hivi vituko tangu aazne kuingia bungeni ajawahi kuona vihoja kama hivi tukikipanga kukaa na kujadili hesabu tulizokuta na matatizo watu wanakimbia nimeomba mh spika kama anaweza aivunjilie mbali hii kamati na sidhan tutafika kama tutaendeleea hivi

  mh mrema anasema ni kweli amesikia kashfa za baadhi ya wabunge na hali inavyoendelea inanidhihirisha kuna mambo mengi makubwa yamefanyika bila kujua kwa kweli inasikitisha tunapochukua jukumu kukagua hesabu za serikali na mwisho kuishia kupokea bahasha...mh mrema anasema hata kamati iliokwenda pwani hivi sasa aina amani kabisa maana wajumbe wake wakiongozwa na mh iddi azan inasemekana waliomba rushwa kwa mkurugenzi mtendaji wahalmashauri ya kisarawe ambae baada ya kuanza kusumbuliwa wakati huo mh azan akiwa kwingine aliamua kumpigia iddi azan kumjulisha kundi lake wanataka nini habari zaisdi zinasema wakiwa handeniw alikuta uchafu mkubwa na kwa kuwa walijigawanya wakawaachia wenzao waandike ripoti hakika ukisoma ile ripoti na data nilizokuwa nazo na ambazo kila mmoja alisaini ni aibu walichoandika na kuamini kweli kazi kubwa iliopo mbele na soln yake si kukaa chini ni kuivunjilia mbali atiuwezi kukaa na kamati za kihuni kila sehemu alisema mh mrema

  mungu natumaini wewe ndie uliwaweka hao watu na kwa mantiki hiyo usiache kudhirisha
   
 16. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #16
  Jul 24, 2011
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,600
  Likes Received: 6,767
  Trophy Points: 280
  Bongo is a failed state?!!!!!!!!!!!!
   
Loading...