Mrejesho wakucomfirm vipimo vya HIV

Mrejesho wakucomfirm vipimo vya HIV

Baadhi Wahudumu wa afya ni wabaya Sana na wachache ni waaminifu,Kuna visa viwili vya Hawa watu ambavyo viliniacha hoi .

Kisa cha kwanza Ni Cha huyu mhudumu wa afya ambaye nilikutana naye mwaka 2013 kule Mkoani iringa katika harakati za kutafuta riziki ,nikiwa pale hospitali upande wamaabara nasubiri majibu ili niyapeleke kwa daktari alikuja jamaa mmoja ambaye alikuwa pale maabara sikujua alikuwa anatafuta Nini,lakini ghafula yalitokea mabishano makari Kati ya mhudumu wa maabara na yule jamaa,baadae jamaa alitoka na kutokomea na kumuacha muhudumu wa maabara akilalama,ili bidi nimuulize kulikoni ndugu yangu,yule mama wa maabara alinijibu kuwa huyu jamaa amemleta binti hapa akidai kuwa binti amebakwa ,lakini binti amepimwa hajabakwa na hakuna shida yoyote kwa binti,sasa ananilazimisha niandike kuwa binti kabakwa hakika nilibaki kinywa wazi na nikampongeza mama yule kwa kukataa rushwa ambayo baadae ingegalimu maisha ya mwanamme mwenzangu.


Kisa Cha pili kilitokea nikiwa Lindi ,Kuna jamaa tetesi zilikuwa zimesambaa kuwa ana UKIMWI, kwa kuwa utamaduni wa watu wa Lindi wengi wao wamezoea ndoa za mitala jamaa yule alikuwa na wake watatu,sasa akampata binti katika Kijiji jirani ,kwa kuwa wambeya hawana simile walienda kumtonya binti kuwa jamaa Alisha athirika, binti akawa ameshituka hivyo wakati wa kukamilisha taratibu za ndoa iliidi waende kupima,kumbe jamaa kutokana na kuwa na tupesa kidogo akawahi na kumuhonga mtu wa maabara ,majibu yakatoka Hana UKIMWI.

Kimbembe baada ya binti kubeba mimba ,Kama kawaida Wakati wa kuanza kiliniki mama mzazi lazima apimwe,binti kwa kujiamini akakubali bila hiana maana alikuwa anazijua vizuri njia zake, duh majibu kutoka binti anangoma,binti alianguka na kupoteza fahamu,na baadae mimba ya watoto wawili ikatoka.

Huyu jamaa kwa sasa nasikia Ni katibu wa CWT huko mkoani Ruvuma na anagawa Sana dozi,sijajua vizuri Yuko wilaya gani,Ila walimu wa kike huko wawe makini ataua wengi sana huyu jamaa.


Mwisho Wahudumu wa afya na watumishi wa umma kwa ujla jaribuni kuzingatia maadili ya kazi zenu.
 
Poleni sana hatakiwi kuiogopa hali yake maana ataishi kwa taabu
 
Mkuu mbona mi naona kama nyie wote wawili mmeungua?? Au mi ndio sijaelewa hizo picha za vipimo??
 
Wakuu nimeleta mrejesho wa nyuzi ya Jana ya vipimo...Kama ilivyo ada Leo asubuh mida ya SAA nne tulikubaliana tukutane tuende Sasa hospital tukahakiki vipimo vya HIV ambavyo tulikua tumeshajipima mwenyewe ambapo majibu kwa mwenzagu yaliku mistar2 mmoja umekolea ktk c na mwingine uko kwenye 1 umefifia
Sasa bas nimemkupa kashafika hospital nusu saaa kabla nkamwabia twende za serikali akagoma akasema hawez kwenda kwingne mihapo nshapata mashaka hapa Kuna kitu,bas tukaingia kwa dokta akatoa bioline kumbuka hapo minataka vipimo vyote bioline na unigold.nkawa makini kuangalia anavotoa vipimo nakuchana ...akaanza mwenzagu akachomwa akapimwa nkafuatia mim
Bas dokta akatuambia subirini nje,lakini Cha ajabu tumesubiria Zaid ya dk25 Tena nkafanya kulazimisha kumwambia dokta tunahara bas akatwita kutupa majibu... Majibu akasema mko negative wote ikabid nivichukua nishuhudie nkakuta kweli negative...Ila akili ikasita kwanin akatae kwenda serikali ang'ang'anie huku
Ikabid nimshawishi kwenda serikalini akakubali kwa mda mrefu kinyonge kwa masharti nimpe hela nkasema so kesi tukaenda kufika serikali nkaulizia nesi nkamuelezea tunataka kupima vipimo vyote unigold na bioline ..Sasa mwenzangu akawa hatulii tulii Mara katoka nje Mara amuulize nes choon wapi,Sasa akawa Kama anamwabia nesi kuwa tumetoka kupima tumekuta negative bed anamwabia haina shida tunapima Tena wasiwasi wako nin bas kupima bioline wote mim nayeye Kisha unigold..Sasa yeye kipimo Cha bioline kikaonyesha mistari2 kwenye c umekolea na kwenye 1 mstar umefifia kwa mbaali
Sasa nesi ikabid aweke damu kwenye unigold napo ikatoka mistar miwili kwenye C umekolea na kwenye T umefifia kwa mbaali,mtu wangu akawa Kama mjanjamjanja hivi nes akasema huyu huyo kwenye matazamia inaonekana anatumia dozi mda mrefu au kapata maambukizi hivi karibuni...bas tukatoka tukaondoka nkamuacha mwenzangu mahala aende kwao minkarud kwa manes kutaka kujua
Sasa manes wakanambia wakat upo ndan mwenzio anaulizia chooni babes alikua nje kafuta unigold nes akanambia mwenzagu alikua ananiita kwa ishara ya mkono kuonyesha kitu nes akakataa akasema huyo mwenzio nlikua nshamshutikia tangu anahojihoji maswali kabla yakupima kuwa Mara sjui ashapima huko tumekota
Wakuu Sasa bas huyo daktar wahospital ya private tulioenda akatoa majibu negative Tena baada yakusubiria Zaid ya dk30 kumbuka nahiyo hospital nlimkuta mwenzangu ashafika mda mrefu je hakupewa hongo kweli?naambatanisha chini majibu yake ya hospital ya pili tulikoendaView attachment 2055630

View attachment 2055628
View attachment 2055635

Huyo dem ni wa kigoma?
 
Back
Top Bottom