lup
JF-Expert Member
- Apr 23, 2015
- 2,514
- 2,743
Za wakati huu wana GT, naamini kama ilivyokawaida yetu kwa vile leo mkuu alivyowatunuku vyeti hao waliofanikisha zoezi la kupata japo 300m USD, kwani hata hizo hatukuwa nazo na akaendelea kuthibitisha hao ni wezi. Kwa hiyo naamini wana great thinker bado mnatafakari kwa kina hutoba yake ya shukrani, sasa niende kwenye mada moja kwa moja.
Nimekuwa nikipost hapa kuwa sasa nahitaji kuoa, ingawa maisha yangu bado ni ya kawaida sana lakini lazima nioe ili nipate kibali zaidi kwa Mungu kama yasemavyo maandiko matakatifu, lakini kuondokana na ushauri na Sunna ya Mtume Paulo ya kusema kuwa kama tunaweza tuishi kama yeye kwa maana muda ule hakuwa na mke wala mpango wa kuoa.
Kitu nilichokigundua kutokana na wengi kupinigia simu lakini hata ku- PM, ingawa mimi nilikuwa namaanisha lakini wengi walikuwa wanajaribu na walikuwa hawamaanishi hata kidogo. Ingawa kweli nilipata mmoja alionesha kumaanisha lakini tatizo alikuwa mbali, na mimi sera ya kutuma nauli ukweli sina (kwa maana mimi naishi kanda ya ziwa na yeye yuko kada ya bahari).
Wengine nilingudua walifungua au wana akaunt isiyo na avata pia haina taarifa sahihi na kazi yake ni hiyo ya kujaribu watu.
Kingine niligudua ukweli kuna wanawake ambao wanachagua mtu wa hali fulani ya maisha, nahisi lengo lao ni kuchuna na kukaa juu ya mawe, wanapenda kazi yako au kipato lakini sio mtu.
Wengine niligundua ni mabigwa wa kupinga mizinga, yaani ukisha onesha nia ya dhati hata kabla ya kuonana huku anaishi sio mbali na ulipo lakini hachelewi mzinga na ukimshtukia tayari mawasiliano yanakufa hapo.
Wengine niligundua hawana lugha za kawaida zaidi ametawaliwa na lugha za vijiwemi mfano nirushie buku tano fasta kama vipi, hadi unawaza hii lugha kweli naielewa lakini sio ya kutumia!
Wengine niligundua hawachelewi kukwambia amepata dharula hivyo nimrushie pesa kwani mama yake ameugua ghafla, sasa unawaza yaani kuchati kama masaa mawili tayari na mama anaumwa na mimi ndio suluhisho na kama tusingewasilina angefanyaje!
Wengine wanaomba nauli kubwa kuliko inavyohitajika, hata kama akikodi tax bado hiyo nauli ni kubwa .
Kuna sababu nyingi sana lakini bado naamini wapo wanaomaanisha hivyo kijana mwezangu usikate tamaa utapata, ingawa Mimi sijapata lakini bado natafuta.