Mrejesho utakanao na mada za ubunifu

Mrejesho utakanao na mada za ubunifu

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
361,100
Reaction score
831,745
Baada ya miezi miwili na ushee ya kupost mada za ubunifu kwenye majukwaa mbalimbali hasa jukwaa la makazi na ujenzi na kidogo ujasiriamali.. Hatimaye picha zimeanza kupungua sasa

Dhima ya hizi mada ilikuwa kuamshq udadisi, kuchagiza ubunifu na kusherehesha sanaa ya ubunifu kwenye majukwaa tajwa.. Lakini zaidi ilikuwa ni kuondoa mazoea ya kupost mada zilezile wakati wote na kwa vitu vilevile... Nje ya hayo ilikuwa kutengeneza database ya bank ya picha za ubunifu kwa kutumia malighafi za kawaida ikiwemo zilizokwisha tumika na kuwekwa kwenye kundi la uchafu..

Hii haikuwa kazi ndogo bali ilikuwa kazi ngumu nzito iliyohitaji muda, utulivu na nyenzo.. Ilikuwa ni rahisi zaidi kubuni kichwa cha habari kuliko kupata maudhui yake ambayo kwa asilia miamoja yalikuwa ni picha.. Lingine ilikuwa ni uchaguzi sahihi wa picha zinazoendana na kichwa cha habari

Kuna wakati hapa na pale nilifanya makosa kwa kuchanganya picha lakini kwakuwa ufuatiliaji wa wanajukwaa ulikuwa mdogo niliweza kugundua na kurekebisha mwenyewe wakati mwingine kwa kuchelewa kidogo
Mwitikio wa wanajukwaa kwa baadhi ya post ulikuwepo lakini kadiri mapicha yalivyozidi kuporomoka weengi waliichoka mada haraka..

Hili halikuwa tatizo sana kwakuwa muktadha haukuwa uchangiaji bali kutengeneza database, hivyo ilihitajika kupost picha nyingi kwelikweli na hayo majukwaa yakaanza kupata uhai zaidi
Baada ya kuanza kupata mwitikio mzuri ndio nikaja sasa na mada ya wabunifu wa JF ..

Hii ilikuwa sasa ni kwa ajili ya kuwavuta wote kwa pamoja na kuona kama tunaweza kufanya kitu kwanza kwa nadharia na pili kwa vitendo! Hapa mwtikio ukawa ni wa kawaida hivyo nikaishia kupost mapicha randomly
Kuna feedback nilizipata lakini ni members waliotaka kuwa na baadhi ya picha kwa matumizi yao wenyewe! Mirejesho ya waliotaka kufanya ubunifu katika uhalisia wake ulikuwa ni almost sifuri!

Bado sijakata tamaa kwakuwa tayari mbegu imeshapandwa na kuanza kuchipuka! Hatua ijayo ni mada za ubunifu lakini hatua kwa hatua mpaka kitu kikamilike. Yaani kama ni kutengeneza kinyago cha mpapure ni maelezo ya hatua kwa hatua kuanzia vitendea kazi, malighafi mpaka vipimo..

Kwenye mapicha mengi ya ubunifu, baadhi ya bunifu zilikuwa za kijinga😁 kama ile ya njiti za viberiti,.. Lakini kwakuwa ubunifu hauna mipaka basi sio kesi..

Haya ndio machache na kwa ufupi yaliyotokana na mada za ubunifu... Naamini sasa mmeanza kupata picha
Asanteni sana,, siku hizi sirogi tena😁
FB_IMG_1742393385706.jpg


 
Ninatumia miwa kuzalisha mkaa, na ingawa bado sijaanza kuuza nje, ninaweza kusema kwa fahari chapa yangu inatawala masoko ya ndani na maduka makubwa yenye ubora wa mkaa.

Yote ilianza na mimi kuuza mkaa wa kawaida, lakini niliona picha kubwa zaidi. Kwa kuzingatia mahitaji makubwa na ukweli kwamba watu wengi huepuka biashara hii,
Niliamua kuchukua mambo zaidi. Niliendeleza utayarishaji wangu, nilizingatia ubora, na nikaunda kitu ninachoweza kujivunia leo.

Nataka kuwatia moyo vijana, msipuuze biashara ya mkaa. Iwe katika rejareja au uzalishaji, kuna uwezo mkubwa.
Ukijitolea kwake, utafanikiwa kwa muda mfupi. Fursa iko kila mahali; inabidi uione tu

Pesa 💵 tayari imechapishwa, nenda ukaichukue ✍️
FB_IMG_1742585201466.jpg
FB_IMG_1742585205302.jpg
 
Jinsi ya Kukuza Karanga kwenye Udongo kutoka kwa Karanga Zilizonunuliwa Dukani

1. Tayarisha Karanga: Loweka karanga mbichi kwenye maji kwa masaa 8-12.
2. Udongo: Tumia udongo unaotoa maji vizuri kwenye sufuria kubwa zenye mashimo ya kupitishia maji.
3. KuPanda: Panda karanga zilizolowekwa awali kwa kina cha inchi 1-2, zilizotenganishwa kwa inchi 6-8.
4. Mwanga wa jua: Weka vyungu mahali penye jua, ukipata jua kwa saa 6-8 kila siku.
5. Maji: Weka udongo unyevu lakini usiwe na unyevu, umwagilia mara kwa mara.
6. Mbolea: Tumia mbolea iliyosawazishwa mara kwa mara.
7. Matunzo: Tazama maua ya manjano yakigeuka kuwa vigingi, ambayo hukua na kuwa karanga.
8. Kuvuna: Chimba mimea majani yanapogeuka manjano. Acha karanga zikauke kwa wiki 1-2.
9. Hifadhi: Ondoa karanga kutoka kwenye maganda na uhifadhi mahali pa baridi na kavu. Furahia mavuno yako!
FB_IMG_1742733675852.jpg
 
Mfumo wa umwagiliaji wa Olla ni njia ya zamani, rafiki kwa mazingira kwa bustani endelevu. Hivi ndivyo inavyofanya kazi:

Faida:

  • Huokoa hadi 70% ya maji ikilinganishwa na umwagiliaji wa jadi
  • Matengenezo ya chini, kujaza tena kila siku chache
  • Hukuza mimea yenye afya na ukuaji wa mizizi ya kina
  • Hupunguza ukuaji wa magugu kwa kumwagilia mimea iliyo karibu tu
  • Imetengenezwa kwa nyenzo asilia, isiyo na maji

Utekelezaji:

1. Chagua sufuria ya udongo isiyo na mwanga au olla iliyofanywa kabla
2. Zika olla karibu na mimea, hadi shingoni
3. Jaza maji ili kunyunyiza polepole mizizi ya mmea
4. Funika kwa kifuniko au mwamba ili kuzuia uvukizi
5. Jaza tena inavyohitajika, ukiangalia kila baada ya siku chache

Matumizi bora:

  • Vitanda vilivyoinuliwa kwa bustani za mijini
  • Vitanda vya maua na mboga kwa mimea yenye afya
  • Vyombo vya vipandikizi vya kujimwagilia maji
FB_IMG_1742767278124.jpg
 
Back
Top Bottom