Mrejesho: Ushauri katika kadhia hii ya kifamilia

biasharaTz

Senior Member
Joined
Apr 14, 2016
Posts
163
Reaction score
79
Habari zenu wana Jamii
Kama nilivyoahidi kuleta mrejesho katika suala la kuomba msaada wa mawazo na ushauri juu ya kadhia ya kifamilia iliyonikuta
Katika ushauri nilioupata na nikaona ni vema niuchukue na kuufanyia kazi ni wa suala la kwenda kupima DNA za wale watoto wawili. Japo kuna wengine walinishauri nimpotezee yeye pamoja na watoto lakini baada ya kutafakari kwa kina nikaona ni vema niendelee tu na suala la kupima DNA. Juu ya yote nasema asanteni wote kwa michango yenu wote kwani inawezekana kwangu haikufaa lakini kuna mwingine itamfaa ambaye amepitia katika mapito ya aina hii
Anyway nisirefushe sana habari. Ila ni kuwa baada ya kuamua suala la kupima DNA ilibidi niwasishirikishe mzee na mshenga wangu na kuwapa habari yote na wao wakasema hakuna taabu isipokuwa kwa kuwa tayari kulikuwa na kutokuelewana kwa kiwango kikubwa basi ni vema na yule mwanamke wataarifiwe wazazi wake na kama kuna nafasi lifanyike baraza. Nikamtaarifu mwanamke pamoja na wazazi wake na kuwakaribisha katika baraza na kwa vile hizi siku zilikuwa za mapumziko ilikuwa rahisi hivyo Jumapili baraza likafanyika. Kwa nini labda baraza lilifanyika? Mzee wangu aliona ni vema nami waniandae kisaikolojia kukubali matokeo ya aina yoyote na hasa kama ni mtoto/watoto wangu bhasi nikubali na nijue nitawapokea vipi na kufungua maisha mapya. Ila suala la kurudiana na huyu mwanamke hata mzazi na mshenga hawakuwa radhi na hilo na msimamo uliwekwa wazi mwanzo wa kikao kuwa ajenda kuu ni watoto na kama wangu nitatoa ushirikiano vipi kwa mzazi mwenzangu, ikiwa katika kuwajibika.
Bhasi kila upande ulisema ya kwake na kuona yanayofaa na hatimaye ikafikia ile ajenda kuu kuwa WATOTO NI WANGU AU SIO WANGU. Mzee wangu alimuuliza swali moja tu hawa watoto una uhakika ni wa mwanangu? Thibitisha kama ndiyo! Akaomba kadi za clinic za watoto wote wawili pale pale. Swali hili lilimchanganya sana kwani alihisi huenda sisi tulishafanya kufatilia kadi za kuzaliwa za wale watoto. Akajiumauma weee lakini mwishowe akakiri kuwa kweli hata katika kadi zile majina ya wale watoto MIMI SITAMBULIKI KAMA BABA YAO hivyo kuna majina ya huyooo kibopa aliemuwezesha kupata ajira. Huu ukawa ushahidi wa kwanza watoto sio wangu
Pili, nikamuuliza wakati nambembeleza alinipigia mwanaume mmoja simjui na kuniambia wazi kuwa yule mtoto wa kwanza ni wake na hii ilikuwa ahadi ya huyu mwanamke amzalie akishafanikisha kazi kupata. Namba ile niliisevu wakati huo na nikamkumbusha akawa anabisha. Mwenyezi Mungu hamfichi mnafiki yule bwana akawa anampigia simu naona kuna mambo yao waliyotofautiana. Sasa aliipokea simu ili kuonyesha baraza kuwa mimi sipo sahihi ili amkanushe kuwa yule mtoto sio wake, kama vile alichokoza. Yule bwana akamwaga a to z hadi mtoto wa pili na ushahidi wa vipimo vya DNA anao hao watoto wote ni wake kwani aliwahi kuwa na wasiwasi na mienendo ya yule bibie na vijana wa pale ofisini. Akasema kama nahitaji kujiridhisha atume katika whatsapp na email na yupo tayari kwenda kuthibitisha hata mahakamani kuwa hao watoto ni wake.
Ukweli ukadhihiri na akakosa la kuongea na kusababisha yeye na wazazi wake wote kuondoka katika baraza kwa aibu kuu ya kufungia mwaka
Nini nimejifunza katika hili? Kwanza kabisa kuwa na subira katika kila jambo na wakati wasubiri hakika weka matumaini na imani yako kwa yakini kwa Mwenyezi Mungu pekee. Omba na fanya visimamo vya usiku mshitakie akuonyeshe na akupe haki dhidi ya batili. Sikuwahi kuwaza kuwa nitapata majibu ya uthibitisho rahisi kiasi hiki ila kwa Idhini ya Mwenyezi Mungu kadhia imeisha saaafi kabisa kiroho safi na sasa nafurahia maisha ya raha mustarehe bila bughudha za meseji wala calls zilizokuwa zinanisumbua.
Asanteni sana
 
Nakuonea wivu sana mkuu yaani upo single kwa raha zako, duh!!!
 
Duh! We nyota yako ni ya kugongewa, watoto wote sio wako! Hata ukioa tena utagongewa tu
 
Kwa nini mkuu!!? Mbona naona nipo katika mtihani mzito wa kuwa single. Kuwa na mke ndugu yangu raha. Asiyejua raha ya mke hatatamani kuwa na mke

Dah, mkuu pamoja na mauzauza yote hayo bado unatamani ndoa? kweli binadamu tunatofautiana. Mimi kitendo cha kutokuwa huru tu ingawa wife hana matatizo. Ingekuwa mimi ningekula life kwanzaa hadi kwenye 50 hivi then nakuja oa kitoto cha 25+ hivi.
 
Daaah!!So..Sad.
Imenilazimu,niandike..licha..ya..kusumbuliwa..na..Device..yangu.

Umenigusa..Sana,Mkuu.
Una..Moyo,Una..Hekima,Una..Busara,Una..Uvumilivu.

Wewe..ni..mfano,mzuri..wa..jinsi..Mwanaume..wa..kweli,anavyopaswa..kuwa.

Niliisoma,ile..Habari..ulivyoileta..Mara..ya..kwanza.Lakini..sikutarajia..kama..matatizo...yako..yataisha..Hivi.

Umenitia..Sana..Moyo.
Umenifunza...Umenipa..Ari..ya..kutokuwa..na..papara..unapokabiliwa..na..tatizo.
Umenifanya..nitambue..kuwa,kuna..maisha...zaidi..ya..hawa..viumbe.
Ni..mwanaume..Gani..Karne..angechukua..Maamuzi..uliyochukua,kwa_yalikukuta!!
Una..busara..sana.

Nitalitumia,funzo..hili..kama..silaha..yangu,katika..Maisha..yangu..yajayo.

Bado..ni..kijana..kidogo.
Sijaoa,Sina..Mke,Wala..Familia.
Itoshe..tu,kusema..nimejifunza..mengi..kutokana..na..kushare..nasi,Tatizo..lako.

Ubarikiwe..Sana.
Mungu..Awe..Nawe.
Ahsante.
 
Mwanamke gani mdogo anakubali kuolewa na mzee asiyekuwa na hela? Kama utakuwa nazo sawa ila jiandae na moyo kurukaruka
 
Daaah!!So..Sad.
Imenilazimu,niandike..licha..ya..kusumbuliwa..na..Device..yangu.

Umenigusa..Sana,Mkuu.
Una..Moyo,Una..Hekima,Una..Busara,Una..Uvumilivu.

Wewe..ni..mfano,mzuri..wa..jinsi..Mwanaume..wa..kweli,anavyopaswa..kuwa.

Niliisoma,ile..Habari..ulivyoileta..Mara..ya..kwanza.Lakini..sikutarajia..kama..matatizo...yako..yataisha..Hivi.

Umenitia..Sana..Moyo.
Umenifunza...Umenipa..Ari..ya..kutokuwa..na..papara..unapokabiliwa..na..tatizo.
Umenifanya..nitambue..kuwa,kuna..maisha...zaidi..ya..hawa..viumbe.
Ni..mwanaume..Gani..Karne..angechukua..Maamuzi..uliyochukua,kwa_yalikukuta!!
Una..busara..sana.

Nitalitumia,funzo..hili..kama..silaha..yangu,katika..Maisha..yangu..yajayo.

Bado..ni..kijana..kidogo.
Sijaoa,Sina..Mke,Wala..Familia.
Itoshe..tu,kusema..nimejifunza..mengi..kutokana..na..kushare..nasi,Tatizo..lako.

Ubarikiwe..Sana.
Mungu..Awe..Nawe.
Ahsante.
Hii style ya uandishi kiboko!! Imenikumbusha darasani "Punctuate the following passage" haaaah haaaaaah!!!
 
Daah inauma ila weng wanachululia simple kwa kua halijakufika, mwanamke unawezaje kugawa penz had watoto ili upate kaz afu huyo ni mume Wa MTU, tena ni bosi, hivyo bora umezalishwa watoto Wa wili ,ndoa umekosa na Huyo bos c ajabu akakuachisha kaz, hii akili ni ya kuku au nn nafikir baadhi ya wanawake wamesababisha wanaume wengi kupoteza iman juu ya mabint ila kila MTU ajifunze nikusih kila kitu kinachotokea katika maisha yako mungu anampango na ww na amekuepushia kitu, mungu atakufuta machoz na atakupa MKE mwema, pole sana, its so sad
 
Dah, mkuu pamoja na mauzauza yote hayo bado unatamani ndoa? kweli binadamu tunatofautiana. Mimi kitendo cha kutokuwa huru tu ingawa wife hana matatizo. Ingekuwa mimi ningekula life kwanzaa hadi kwenye 50 hivi then nakuja oa kitoto cha 25+ hivi.
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] kaka we humwogopi Mwenyezi Mungu. Zinaa mbaya na hakika ni deni ambalo lazima atalipa yoyote ktk familia yako
 
Pole sana mkuu but pia umechukua maamuzi sahihi, ila tabia ya kuwaamin sana wake inawaumiza wanaume wengi mm mtoto akifanana na mama tu na sio mm lazima nicheki DNA kwa siri akiwa bado Mdog SIPENDANGI UBEGWE wa kulea mtoto wa mtu
 
Dah, mkuu pamoja na mauzauza yote hayo bado unatamani ndoa? kweli binadamu tunatofautiana. Mimi kitendo cha kutokuwa huru tu ingawa wife hana matatizo. Ingekuwa mimi ningekula life kwanzaa hadi kwenye 50 hivi then nakuja oa kitoto cha 25+ hivi.
Kwa Idea yako hii, watoto wako wakija kuapply (waoe wakiwa na 50) utakufa hujaona wajukuu mkuu
 
Mwenyezimungu hafanani na Kiumbe Chochote Ila ni kweli alimpa Mwanadamu Akili ya kujua Mema na mabaya
mkuu naona unawatafuta wanadini waliko, maandiko ya bibilia yanasema binadamu ameumbwa kwa mfano wa Mungu, yaani wwe unafana na Mungu
 
Daaah!!So..Sad.
Imenilazimu,niandike..licha..ya..kusumbuliwa..na..Device..yangu.

Umenigusa..Sana,Mkuu.
Una..Moyo,Una..Hekima,Una..Busara,Una..Uvumilivu.

Wewe..ni..mfano,mzuri..wa..jinsi..Mwanaume..wa..kweli,anavyopaswa..kuwa.

Niliisoma,ile..Habari..ulivyoileta..Mara..ya..kwanza.Lakini..sikutarajia..kama..matatizo...yako..yataisha..Hivi.

Umenitia..Sana..Moyo.
Umenifunza...Umenipa..Ari..ya..kutokuwa..na..papara..unapokabiliwa..na..tatizo.
Umenifanya..nitambue..kuwa,kuna..maisha...zaidi..ya..hawa..viumbe.
Ni..mwanaume..Gani..Karne..angechukua..Maamuzi..uliyochukua,kwa_yalikukuta!!
Una..busara..sana.

Nitalitumia,funzo..hili..kama..silaha..yangu,katika..Maisha..yangu..yajayo.

Bado..ni..kijana..kidogo.
Sijaoa,Sina..Mke,Wala..Familia.
Itoshe..tu,kusema..nimejifunza..mengi..kutokana..na..kushare..nasi,Tatizo..lako.

Ubarikiwe..Sana.
Mungu..Awe..Nawe.
Ahsante.
Asante mkuu
Unajua katika maisha ukitumia jazba na nguvu nyingi utajikuta unakuwa katika fungu la kukosa. Subira ibada na ina malipo ya kudumu kuliko kuwa na papara ambapo utapata majibu lakini furaha yako itadumu kwa muda mfupi tu
Wanaume tujifunze kukaza moyo na kujitahidi kudhibiti hasira na jazba.
Na wanandoa tujitahidi kuwa waaminifu ndani ya ndoa unapojaaliwa kupata mwenza.
 
Back
Top Bottom