pakaywatek
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 4,710
- 6,372
Nilileta thread ya mke ninaeishi nae niliemkuta anadokoa pesa, watu wali changia nashukuru kwa baadhi yenu kutoa ushauri.
Kilichofwata: baada ya kumkuta anaiba pesa, nilitoka nikaenda zangu bar nikiwa na mawazo nimfanyie nini, nilikaa bar hadi mida ya sa sita ingawa situmii pombe, nilitumia maji karibia lita tatu kupoza hasira.
Baada ya kurudi nyumbani nilimkuta amekaa anaendelea kuchati na simu kama kawaida yake, aliponiona akawa na wasiwasi, tangu tuishi nae sijawahi kushika simu yake zaidi ya Mara tatu! kwa nini? Kwa sababu nilishawahi kupata shida na mwanamke ambae tulizaa nae hivyo nilihapa kutokushika simu ya mwanamke.
Nilipomkuta nikamwambia anipe simu nikamuamrisha atoe password akiwa anatetemeka akaanza kuniomba msamaha, nikachukua simu nikaingia bedroom nikaweka lock akabaki sitting room, nikaenda moja kwa moja kwenye SMS lengo langu nilitaka kuona SMS alizo kuwa anatumiana na wazazi wake kama ndo alikua anawatumia pesa.
Lakini nilicho kutana nacho yaani mi natafuta SMS za mamake zingine ndo zinaingia ambazo ni za mapenzi, ilibidi nisitishe zoezi nililokusudia na kuanza kusoma SMS zilizoingia kabla sijamaliza nilianza kutetemeka kwa hasira, lakini nilijizuia nikatulia.
Nilichukua simu yangu nikazipiga picha SMS zote, baada ya kumaliza nikafungua mlango nikamkuta analia nikampa simu yake akaichukua kwa uoga ikiwa bado haijaji lock na SMS ya mwisho kuisoma bado ipo hewani.
Nilirudi chumbani nikaoga siku hiyo sikulala hadi asubuhi yaani nililala macho, sikumuuliza tena chochote na siku zote hizo alikua akilala chumba cha mdogo wangu ambae yupo shule mda huu.
Leo sasa; nimerudi kutoka kwenye mizunguko yangu nimekuta barua kitandani, kuwa, KAMA UNANIPENDA njoo kwetu tuongee.
Na siku zote hizo wazazi wake wamekua wakinipigia simu kuomba msamaha, ninachofanya yeyote akipiga simu napokea naacha anaongea hadi basi Mimi sijibu chochote na sikati simu hadi akate mwenyewe.
MWISHO: namshukuru mungu kwa kuniondolea huu mzigo bila kumwaga damu.