JembePoli
JF-Expert Member
- Jul 14, 2015
- 1,324
- 999
Habari wanajamvi pendwa MMU,
Naomba niwashukuru wote mlionichangia ushauri kwenye kisa changu cha kweli "njia panda (nimuoe yupi anaenipenda au ninaempenda?) Jana ndio ilikuwa siku ya maamuzi saa7:00 usiku nilipoamua kufanya maamuzi,Niliwashilikisha watu wazima na kuwasimulia kama nilivyoileta kwenu na wakapenda wawepo wakati wa tukio.
Kaka na mzee mmoja jirani yake pamoja na mzee Limo ambae ni jirani yangu walikuwa tayari wapo ndani ya sebule yangu kusikiliza nitakavyotoa maamuzi kuhusu yupi nimeamua nimuoe.Nakumbuka mpenzi wangu wa kwanza alifika 7:20 alishanga kuona ugeni pale kwani sio kawaida lakini nilimtoa wasi wasi na wa pili alifika 7:31 kama sijakosea,(mapigo ya moyo wangu hapa yalibadilika mno)
Lakini nilishangaa kidogo baada ya kuona hakushtuka (ikumbukwe hakuna aliekuwa akijua ameitiwa nini)
Suprise ilikuwa ikini suprise mwenyewe.Nakumbuka ni mzee Limo alieanza kuwambia wale mabinti (wapenzi wangu) kwa kuwauliza 'Nyie walembo mnajua mualiko wenu unahusu nini?
Kwa pamoja walijibu hawajui akawapa swali tena nyie huyo 'huku akininyoshea mkono' ni nani yenu? Hapo walisita na kutizamana kwa pamoja wakajibu ni rafiki yetu.Mzee akawapa tena,rafiki yenu kivipi kwani nyinyi mnajuana?
Hapo majibu ndio yalinivuruga kwani iko hivi.Wa kwanza alianza kusimulia.
Nimemjua jembepoli miaka 3 iliyopita ni mpenzi wangu tangu 2012 lakini alikuja kubadilika mwaka 2013 mwanzoni japo kila nikimuuliza sababu za kubadilika alikuwa akinijibu wasi wasi wangu tu yeye yuko sawa,lakini kwa sababu mimi namfahamu vizuri nikajua kuna tatizo nikaanza kumfuatilia kwa uchunguzi wa kimya kimya nikaja kugundua amempata msichana mwingine,'iliniumiza kwa kweli' lakini kwa kuwa nikataka kujua zaidi sikutaka kumuuliza nikapanga nimtafute msichana mwenzangu ili nae niongee nae kupata uhakika,jembepoli hakubadilika alikuwa akinipa mapenzi moto moto kila ninalotaka alinipa.
Nakumbuka ilikuwa 2014 mwezi wa 7 nilipofanikiwa kukutana na mke mwenzangu pale alipokuwa anatoka kazini kwa kweli alikuwa mstaarabu na nikamueleza kuhusu mahusiano aliyonayo kuwa tunashere mume akaniomba achunguze kama ni kweli nikampa namba yangu ya simu kwa kweli alikuwa ananipa ushilikiano kwani nilikuwa najua uko wapi nae anajua kama uko kwangu 'hapa alinitazama kwa mala ya kwanza tangia aanze kusimulia,kwa aibu mwanaume nikakwepa na kujiinamia)
Basi tukapanga mimi na (alitaja jina) mke mwezangu tukutane tuongee na ndio tukakubaliana siku moja tumuite tuongee nae na achague mmoja Kati yetu kwani mwenzangu alidai amejaribu kumkasirikia ili awe mbali nae lakini ameshindwa na kujikuta anaumia na kushindwa kufanya kazi na mambo yake na hapa naomba niwaweke wazi kuna siku waligombana mimi nikaenda kwa(akataja jina) mke mwenzangu alikuwa mnyoge na kama anaumwa hivi ikabidi tukubaliane mimi na mke mwenzangu tu.
Kuwa kwa kuwa tumegundua JembePoli Hana mtu mwingine zaidi yetu basi tuache mpaka mwenyewe atakapoamua itakavyokuwa kwani hakuna tunachokosa kwake tukawa marafiki bila mume wetu kujua kuwa tunajuana,nakumbuka kuna siku alishtuka kuona tumevaa nguo sare lakini hakujua kuwa ule ni mpango ambao sisi tuliupanga kuona nini anawaza (niliwahi kuileta mada hii hapa Jf kwa bandiko.sijui wamejuana wameshona sare)
Lakini naona mwenzetu hakugungua hivyo ndivyo ilivyo baba Angu.
Akamaliza kusimulia wa kwanza na mzee Limo akamgeukia mpenzi wangu wa pili ambae alikuwa amejiinamia na kumuuliza eti ni kweli mamaa aliinua kichwa na kuona ni jinsi gani alivyokuwa analia kimya kimya (hata mimi nilijisikia vibaya) ndio ni kweli mzee! Alijibu.Mzee Limo alitugeukia sisi na kutuuliza/kuniuliza jamani nyie mnasemaje.
Bro bila kupepesa akasema hapa hakuna cha tunasemaje aseme anamtaka yupi na tuende tukapose maana tabia wameshajuana kaka angu yupo na umri kama 40+ mjeshi kwa hiyo amri ni kawaida.Kwa upole nikajibu nawapenda wote lakini kwa kuwa ni la zima nioe mmoja basi Nikamchagua mpenzi wangu wa pili lakini nikawa nimepiga magoti kwa mpenzi wangu wa kwanza anisamehe kwa yote pamoja na uamuzi wangu.
Kabla hajasema lolote mzee Limo pamoja na mzee aliekuja na bro wakamuuliza mchumba wangu wa pili unasemaje?
Mchumba wangu aliomba apewe muda akajifikilie kwani ni kweli ananipenda sana lakini anashindwa kutoa maamuzi kwa muda ule pale.Nashukuru mpenzi wangu wa kwanza alinisamehe kwani niliomba msamaha kwa kumaanisha mzee nilipiga magoti huku mchozi ukitililika mbele ya kikao.
Leo mpaka saivi sijaamka na sijui mpenzi wangu niliemchagua kama atakuja na jibu la kukubali au kukataa lakini nimejiandaa kwa yote na pia bro kasema Mahari yote atalipa yeye(japo mimi sijashindwa)Nawashukuru sana kwa ushauri wenu ulionijenga.Ndefu lakini isome tu.