MREJESHO: Renata Mapunda amepatikana

NUHWAHI

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
304
464
Ama hakika mitandao ya kijamii ina nguvu.. ni masaa 24 tu toka niombe msaada wa kumpata huyu mtu.. ni tayari nimesaidiwa kumpata kwa nguvu za JamiiForum, FaceBook.

ASANTENI WADAU..ASANTENI SANA..kila wazo nililitumia ipasavyo... Na nimempata bila kusafiri. Ni miaka 40+ toka tupotezane na huyo mtu...MUNGU NI MKUBWA JAMANI. Ukoo mzima wamejawa na furaha. Ukoo ulipanga kuzika mgomba tu kama utamaduni kwa mwili ulopotea pasipo onekana.

Karibuni.. hivi sasa pana Ngelenge, mbege, kwa kuku choma wa kienyeji wazee wanafurahi...karibuni Mpapa Mbinga.

Pia Soma:
- Msaada: Namtafuta Renata Mapunda
 
Labda hujanielewa mkuu...niliupitia Uzi wako tangu siku ya Kwanza na nakumbuka Kuna mtu alikusaidia kupata mwanga Sasa baada ya hapo Nini kiliendelea?
Sawa,, tangazo lile nilituma inbox kwa kila mwenye surname ya motta facebook na marafiki zake angalau 5
Hatimaye mmoja toka mwanza akanipigia na kunipa details za hao walipo na namba zao
 
Ni kawaida sana tu hapa Tanzania sema nawashangaa sana Kwa nini iwe mwaka huu na si mingine na wakati Facebook ipo toka 2008 huko, na RFA Redio ilikuwa na Satellite kipindi Cha kuwatafuta ndugu, rafii na jamaa kitambo chini Rahabu Fungo au Rahabu Freddy. Kuna mambo ya ajabu sana kwa nini iwe sasa. In fact Facebook would have been enough without all these lousy noise as if kawakosea chochote
 
KWA UPANDE WANGU.. kakaza mlengwa ni wazee wapo vijijini ambao ni baba zangu... Nami sikuchulia kiumakini... Sasa wiki hii wakawa wanaitana kujadili mambo fulani na hiyo ikawa ajenda lengo wanitume mie kwenda vituo vya kazi alivyowahi fanya mumewe... Nikawaomba wanipe wiki moja nitumie plan hii...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom