Abuu Said
JF-Expert Member
- Jul 5, 2015
- 4,010
- 4,761
Habari zenu wadau wa MMU,
Jana nilileta mada ya
Nitamtokeaje huyu Msichana?
kutaka ushauri jinsi ya kumtokea mtoto mmoja hivi aliekuwa anauumiza mtima wangu baada ya kusoma ushauri wa wachangiaji waliotoa mawazo yao sasa huu ndio mrejesho niliowaahidi kuuleta baada ya kukamilisha zoezi.
Baada ya kusoma maoni mbalimbali ya wadau nikachukua uamuzi wa kumuandikia kimemo ambacho nimeambatanisha na namba yangu ya simu. Mwanaume baada kumaliza shughuli zangu za kila siku nikashika njia kurejea home huku nikiwa na kimemo changu mfukoni nikafika maeneo ya yule binti anapoishi daah! bahati mbaya nikakuta shari nje kwao na yeye akiwepo watu kama wanne hivi akiwemo dada yake pamoja na mzee mmoja wa makamo basi ikabidi nipitilize nikaishia kutoa salamu tu.
Moyo ukaniuma sana nikasema haiwezekani hata njia hii inishinde kama vipi subiri nikajilipue kama mbwai mbwai tu, nikaenda kwanza mpaka home nikachange nguo nikasema subiri nirudi hata kama akiwa na ndugu zake nitamuita pembeni nimkabidhi alafu nisepe, nikaanza safari ya mafanikio moyo wa uwoga nikautoa nikafika eneo la tukio Mungu si athumani nikakuta shari limepungua akawa amebaki yeye na binti mmoja mdogo nadhani ni mtoto wa dada yake mwanaume kufika pale nikamsalimu nikamwambia dada samahani nina ujumbe wako, binti akashtuka mimi?
Nikamwambia ndio huku natoa kimemo changu mfukoni nikamkabidhi akapokea, kidume huyo sikutaka hata kusubiri nikasepa huku nikiwa najiona nimetua bonge la mzigo kichwani kweli mapenzi balaa. Sasa basi wadau kufika mida flani hivi naiti napiga story na wanafamilia wangu home mara sms inaingia kuangalia namba ngeni.
Mambo...
nikajibu Poa....
Ujumbe wako nimeupata...nikamwambia fresh hii ndio namba yako? Kanijibu ndio basi baada ya hapo story nyingine ziliendelea kidogo tukaagana. Kwa hiyo mazee mdau wenu sijawaangusha nimetekeleza jambo mtoto sasa yupo kiganjani hapa sasa mimi tu kama samaki ndo nishamvua chaguo langu nimkaange, nimbanike, nimuunge supu au mchuzi wa chukuchuku.