Mrejesho: Nimedhalilika sana, mke wa mshkaji kaniambia nikalale nyumba ya wageni

navin dippe

Member
May 18, 2015
47
104
Wadau i hope mko poa

Kesho namaliza kazi iliyonileta hapa Mwanza, na Thursday nitakua narudi Dar

Wiki iliyopita nilileta uzi hapa unaosema Nimedhalilika sana, mke wa jamaa yangu kaniambia nikalale nyumba ya wageni
Kuhusu hii safari yangu, kwamba kuna rafiki yangu aliniomba nifikie kwake badala ya hotel, ingawa nilimkatalia lakini alisisitiza sana hivyo nikaona nikubali, matokeo yake mkewe alikataa hataki mgeni hivyo nikaenda hotel, na nikafunga mawasiliano kabisa na hiyo familia kwa udhalilishaji walionifanyia

Mrejesho wenyewe

Jumatano ndo ilikua siku ya tukio, na mm nilileta uzi hapa ijumaa, yule Rafiki yangu alikua na nia ya Kunitafuta nipo hotel gani ili aweze kuniomba msamaha kwa yaliyotokea jumatano usiku ambayo alijua wazi hayakunifurahisha, hakuweza kunipata kwa kuwa sikutaka tena unafiki, hivyo nilimblock hewani

Kumbe baada ya mimi kurusha hewani Uzi ule, some how ulifika kwenye ma group ya whatsaap na yeye kuuona, na bila shaka yoyote alijua ni mimi ndie mwandishi kutokana na kisa chenyewe, na mle kwenye Uzi nilitaja jina la hotel niliyofikia, na ndipo akaja pale na Kuniomba msamaha na kunieleza masahibu yote yanayompata kwenye familia yake.

Kwamba anashangaa mkewe kuleta usumbufu kwa wageni na ndugu Wa jamaa lakini ndugu zake yy mwanamke hawakatiki hapo kila kukicha, nyumba hufurika ndugu Wa mwanamke hadi wengine kulala sebuleni.

Akasema si kwamba hawezi kuchukua hatua Bali hapendi ugomvi au kununiwa wiki mbili na nyumba inageuka libya, au mwanamke huamua kulala na nguo wiki kadhaa, hivyo huwa anaamua kusalim amri na kumwacha mwanamke afanye anavyotaka at the expense of his friends and relatives
So akileta mgeni ikitokea mke akakubali sawa, ikitokea kamkataa ndio hivyo tena.

Nimemwelewa na tukayamaliza, kadai amekwisha kumuoa hivyo hana namna tena, Ingeruhusiwa kubadilisha angenyoosha mkono kuomba abadilishiwe, nikaona ni kweli, maana hakuna sababu ya kuanzisha vurumai na mkewe kisa Mimi Rafiki halaf baadae nasafiri kurudi namuacha na ugomvi na mkewe.

Hitimisho.

Kuna waliotoa coments wakijaribu kuonesha kwamba mimi nilitaka mteremko Wa kulala kwa Rafiki, ili ni save hela ya hotel.Hili si kweli, maana hata baada ya msala huo still nilienda hotel ya 50k niliyopewa, ningeweza kwenda hata ya 15 au 20 mitaa hii ya Uhuru ambapo kuna gesti ndogo ndogo za bei nafuu
Nilienda ya 50k. Kwa kuwa nilijua Nina pewa per diem malipo ya kuwa nje ya kazi maalum kwa siku, mbali na malazi na chakula, hivyo nilijua nitapata kwenye hiyo,

Hata hivyo si mbaya ningeshukuru pia kuipata hiyo ya hotel kwa kuwa option hiyo ilikuwepo kupitia Rafiki yangu, ndio maana wote sisi humu ndani tupo makazini lakini kuna waliojenga na wengine bado, ni kupitia kujinyima na kufunga mkanda kunaweza kukutoa kimaisha, mm kwangu Dar napokea marafiki na wadogo wa marafiki zangu wanaokuja kikazi na tunaishi na kula chochote kilichopo hadi semina inaisha na mtu anarudi na lakini tano hadi million mfukoni kwa kukwepa kulala hotel na kula hotel, akija semina kadhaa kwa mwaka au robo kama ni mtu mwenye malengo yupo mbali, na kwa kuwa mtu anaona anafadhiliwa pa kulala akitoka kwa semina anapitia butchery na kubeba kilo mbili za nyama na mchele kilo mbili tatu analeta nyumbani kama mchango wake, anatoa mule mule kwenye hela aliyopewa na kampuni, haithiri kitu Maisha yanasonga.

Kwa hiyo wewe unaedai kwamba ukisafiri huwa hutaki kusumbua watu, na ukipewa hela ya hotel unaendal kulipa yote huko ili ulale vizuri, ule vizuri, halaf back home umepanga Chumba na sebule, hata kiwanja huna endelea hivyo hivyo, maendeleo utayasikia kwenye TV

For there is no gain without pain

Good day
 
Wengine point yetu ilikuwa uhuru binafsi
ukikaa hotelini unakua huru
uhuru wa kuleta mgeni wako mliokutana nae huko semina
uhuru wa kula unachotaka
uhuru wa kutazama tv vipindi unavyotaka
uhuru wa kutoongea na mtu yeyote kama hutaki...
uhuru wa kulala mda wowote na kurudi mda wowote

kukaa kwa watu kunapunguza uhuru huo.....ingawa kweli labda ungepunguza gharama
 
My company unaambiwa utafikia hotel fulani, kwisha kazi.

Ila pole mdau, ndio maisha.
 
Duuh !! Lakini Mkuu navin dippe siku ila ya kwanza uliipata haswa, hata usingizi sidhani kama ulilala!! Lakini umeonyesha uanaume wako na heshima kwa nafsi yako, Pili umesamehe yaliotokea hapo umekamilisha uRijali wako!! unastahili kuitwa Bingwa !!
God Bless you.
 
Last edited by a moderator:
uje unisalimie basi,niko hapa New park hotel,karibu na aspen,uulizie kolokoloni wa getini Elungata utanipata....
 
You made your point mzee.

Vziuri kama umeshamalizana na rafiki yako.

Familia inafanya mambo yanakuwa complicated sana.

Afadhali huyo mwanamke alikuambia wazi, sehemu nyingine unaondoka na kuacha msala mzito nyuma.

Kufikia kwenye familia za watu wengine sio ishu, achana na mambo hayo.
 
Kma Mlishamalizana Na Jamaa Akaomba Msamaha, Sikuona Haja Ya Kuja Kumchora Tena Humu Wakat Ulishamsameh, Nilidhan Umeleta Mrejesho Wa Kisa Kingine Bhanaa!! Kwa Style Hii Ya Kuchoreshana Wakat Mmeshayamaliza, Napata Picha Auna Utu Na Inawezekana Sio Frend Yako Kwa Maana Ya Ww Ndie Yy Na Yy Ndio Ww!! Thread Ndefuuuuuuuuu Wakat Mmeshayamaliza!!! Urafik Mwingine Bwana, " Pekee Yangu....Naona Bora Pekee Yangu, Marafik Wengi Ni Wanafiki Peke Yangu, Naona Bora Pekee Yangu....""
 
Back
Top Bottom