Mrejesho: Naomba msaada wa ada

Mrejesho: Naomba msaada wa ada

Mpauko

R.I.P
Joined
Jan 19, 2019
Posts
2,323
Reaction score
3,451
Habari za leo.

Katika uzi uliopita nilichapisha uzi ufuatao...

Kwa lengo la kukusanya michango ya kifedha ili niweze kukomboa cheti changu cha kuhitimu Astashahada ya ualimu.

Ikumbukwe mlezi wangu alipata matatizo kwa kupoteza ajira yake,hii ilipelekea kushindwa kumudu kumaliza ada ya chuo.

Katika harakati za kutafuta shughuli za kujikimu nilibahatika kukutana na mwana-jamiiforum mmoja aliyejitolea kunisaidia kuomba ajira kutoka TSD.

Hata hivyo TSD wao huhitaji vyeti ili waweze kukuhudumia katika kusaidia watu wenye changamoto mbalimbali za Ulemavu kuweza kupata ajira.

Bahati mbaya vyeti sikuwa navyo na chuo hakikuwa tayari kunipatia bila kumaliza deni la ada kwa jumla ya tsh 1,160,000/=

KWANINI NAOMBA MSAADA.?

Mosi,Kwa sababu familia yangu haina uwezo kwa sasa baada ya mtegemezi kupoteza kibarua.

Pili,baada ya miezi tisa ya kutafuta ajira na miezi nane ya kujitolea bila malipo pamoja na kufuatilia kwa viongozi mbalimbali wa mkoa juu ya suala hili,mwisho wa siku wakanipatia kibali cha kuchangisha hivyo ndio sababu kuu ya kuja kwenu.

Tatu,kutokana na hali ya sasa ya upatikanaji wa ajira na hali ya ulemavu wa masikio imeniwia vigumu sana kupata ajira na vibarua mbalimbali hivyo kuishi katika mazingira magumu.

Nne,Hitaji la kujikwamua kimaisha na,

Tano,ukosefu wa mtaji na rasilimali katika kujiajiri.

HIVYO BASI:Kwa wana-Jamiiforum,viongozi na taasisi mbalimbali:

Ni matumaini yangu kuwa kila mmoja anaweza kuwa msaada kwangu kwa nafasi yake katika kunisaidia katika hili.

Nawasilisha kwenu kibali cha kuchangisha pamoja na orodha ya waliojitolea kunisaidia kwa chochote.

Ahsante na Mungu awabariki sana.

Kwa mawasiliano:

0677-421-378-Tigo.
0776-741-545-Zantel.

IMG_20190826_120311.jpeg
IMG_20190830_193343_976.jpeg
 
You know right now nimefikia hatua kuona Mungu hanijali.. ila haina noma mkuu yatapita
 
Naomba mkuu Maxence Melo na MOD wengine watuongoze kupata taarifa za taasisi inayoshikilia chetu cha mhusika yaani kiasi chote anachodaiwa na njia wanazopokea malipo kama hayo e.g Account halafu uongozi utusaidie kupokea michango yetu na itakapotimia waiwakilishe kwa wahusika (Taasisi husika). Nadhani hili likifanikiwa itakuwa sehemu ya mchango wa JF kwa jamii.

Ahsante
 
Naunga mkono hoja hii mkuu nipo tayari account namba ya taasisi husika wanaomdai itolewe tufanye kitu kwa mwenzetu huyu
 
@Maxence melo alikataa kufanya endosement kama inavyoonekana katika screenshot.

Taasisi niliyohitimu(ST.BENARD TEACHERS COLLEGE) mfumo wake wa malipo ni sawia na ule wa shule za sekondary (kwenda na payslip) ndiyo maana sijaweka account ya taasisi kwani nitakosa payslip kama udhibitisho wa malipo chuoni.

Naomba tusaidiane kwa kujitolea katika hili ili niweze kufikia lengo kwani hakuna mchango wowote toka kwa wanajamiiforum hadi sasa ingawaje nilitarajia kuungwa mkono zaidi na Jamiiforum lakini matarajio yamekuwa tofauti licha ya kuweka vidhibitisho vyote.
IMG_20190907_165337_572.jpeg
 
Tunaomba utaje hicho chuo kiko mkoa gani wilaya gani na kuna watu wengine watafuatilia hata mawasiliano ya mkuu wa chuo huna ?
 
Hicho chuo kifungwe hakina corporate social responsibility kwa jamii ? Watoe msaada kwa kutoa hicho cheti.Sichangii hata Mia serikali mlipieni Ada huyo mlemavu na hicho chuo kichangie.Mleta Mada weka akaunti ya chuo na namba za mkuu wa chuo for verification
 
Tunaomba utaje hicho chuo kiko mkoa gani wilaya gani na kuna watu wengine watafuatilia hata mawasiliano ya mkuu wa chuo huna ?
Kinaitwa ST.BENARD TEACHERS COLLEGE,kipo singida mjini,Misuna.

Namba ya principal ikihitajika ipo nitatoa.
 
Kinaitwa ST.BENARD TEACHERS COLLEGE,kipo singida mjini,Misuna.

Namba ya principal ikihitajika ipo nitatoa.
Ok naomba unitumie majina yako yote ambayo ni halisi kwenye cheti maana nipo Singida now j3 nifuatilie niwaletee wanajamvi mrejesho
 
Kinaitwa ST.BENARD TEACHERS COLLEGE,kipo singida mjini,Misuna.

Namba ya principal ikihitajika ipo nitatoa.
Ukiwa stand ya mabasi upande gani chuo kilipo nipe na hiyo namba ya mkuu wa chuo
 
Hicho chuo kifungwe hakina corporate social responsibility kwa jamii ? Watoe msaada kwa kutoa hicho cheti.Sichangii hata Mia serikali mlipieni Ada huyo mlemavu na hicho chuo kichangie.Mleta Mada well akaunti ya chuo na nba za mkuu wa chuo for verification
Akaunt ya chuo ipo,je mtu akilipa moja kwa moja account ya chuo mimi nitawapa udhibitisho gani wa malipo hayo.

Hii ni kwa sababu utaratibu ni ule wa kupeleka payslip pekee.

Serikali nimehangaika nao kwa muda mrefu miezi zaidi ya nane mwisho wa siku wakaniandikia tu hicho kibali.

Nimepita kwa afisa elimu,idara ya afya,mkuu wa wilaya,mkuu wa mkoa,halmashauri na mbunge kote hakuna manufaa.

Haitoshi nimejaribu kwa mh.possi na mh. Mavinde hakuna ushirikiano pia.

Halmashauri walijaribu kuwasiliana na chuo kikagoma katakata ndipo wakanirudisha kwa mkuu wa wilaya,ofisi yake ikaniandikia hocho kibali na haikichangia hata shilingi.
 
Kinaitwa ST.BENARD TEACHERS COLLEGE,kipo singida mjini,Misuna.

Namba ya principal ikihitajika ipo nitatoa.
Toa Sio Hadi uombwe watu wanatakiwa waongee naye.Mlio singida nendeni direct kwenye chuo ku confirm na ara ilipwe account ya chuo na slip iwekwe hapa ili chuo kisije pokea pesa mara mbili mbili na kujikausha.Mhusika asipewe hata Mia zilipwe direct chuoni
 
Ok naomba unitumie majina yako yote ambayo ni halisi kwenye cheti maana nipo Singida now j3 nifuatilie niwaletee wanajamvi mrejesho
Ahsante..

ROBIN EVARISTO MIHO..

ST.BENARD TEACHERS COLLEGE

Chuo kipo jirani na stendi mpya ya basi Misuna.
 
Back
Top Bottom