Mrejesho: MwanaJF aliyeomba mtaji

Mkuu, halafu niligundua kuwa wanaume anaweza kukuambia kuwa anashida ya msingi sana, ukimuhurumia ukimsaidia, badala ya kwenda kufanya kilichokusudiwa anahonga warembo angalau apate hata kimoko[emoji14] [emoji14] [emoji14]

Nikafikiri wanawake wana afadhali labda wako serious kumbe nao sometimes!!!!!!!!!!!!!!!!!?
 
Sawa leta uzi wa kuomba msaada kwa rejea
Sijakuelewa mkuu
 
Mkuu, kwanza nakupongeza sana kwa ulichokifanya. Mimi sioni cha kukupa pole. Hujaliwa wala kutapeliwa bali kajitapeli mwenyewe, ulionesha nia ya kumsaidia lakini kakuangusha. Kajipotezea bahati.

Hiyo pesa itamtafuna na siku moja atajutia uamuzi wake.

Usikate tamaa katika kuwasaidia wengine. Ndivyo hivyo Mungu huendelea kukubariki.
 
Hongera mkuu kwa moyo wako mzuri wa kusaidia, hakika Mungu atakuongezea ulipopunguza insha allah
 
Ahaaaaa, sawa mkuu nimekuelewa ila sio huyo, tumuache tu tusimdhalilishe kwa sababu huenda akajirekebisha na siku moja akawa mtu mzuri sana na akaisaidia jamii. Nikimtaja ataona kama nimeamua kutumia msaada niliompa kumdhalilisha na hiyo haitampa nafasi nzuri ya kujirekebisha kama tusipomtaja.
 
Kuna baadhi ya binaadamu hawana ubinaadamu, nyoyo zao zimejaa unyama. Kuna mtu nilitaka kumpa biashara kama ya million13, jamaa akataka kunifanyia zulma hapo ndio ilikuwa mwisho wa biashara yetu. Na urafiki wetu mpaka leo sijaongea nae mwaka wa 5 huu.
 
Huo ni uamzi wa busara ila ingesaidia ukiweka bila kutaja jina jinsi alivyoomba msaada
 
Kuna jamaa nilimkuta mashambani huko iringa wakati natafuta mali ya shamba, akawa anajaza mazao kwenye magunia na kupakia kwa gari kama kibarua, jamaa alikuwa na hali ngumi sana, nikamuhuhurumia nikamleta dar, tukawa tunafanya naye biashara, nilipo mzoea zoea, nikamtuma shambani sasa aende mwenyewe akachukue mzigo maana mimi ratiba zangu zilikuwa zinabana, akaenda alipofika shambani akaniambia mazao yamepanfa bei kwa hiyo nimtumie hela ya nyongeza, nikamuongezea hela, akatoroka na hela yangu nyingi tu, mpaka wa leo hajarudi, nyumbani kwao napajua, nikiamua naenda kumkamata, lakini kila nikijiuliza nimfanye nini bado sijajua cha kumfanya, hela alihonga wanawake zikaisha, mali anayo miliki ni shati na jinsi mbili zilizotoboka.

Naomba kuwasilisha.
 
Mkuu huyu mtu kajilaani mwenyewe maisha yake yote hatokuja fanikiwa. Lakini cha msingi fuatilia hii falsafa ya "Give it as a charity hope nothing by"
 
Mkuu huyu mtu kajilaani mwenyewe maisha yake yote hatokuja fanikiwa. Lakini cha msingi fuatilia hii falsafa ya "Give it as a charity hope nothing by"
Yeah, hiyo ni falsafa ambayo tukiishika itatuweka huru na kutufanya tuwe na furaha wakati wote.
 
duuuh jamani!!!!!!
huyo ajielewi.
mm naomba mwenye moyo kama huyu kaka alietoa msaada wake bila mafanikio.
mm sina mtaji.
naomba tu mtu anisaidie kiasi kitakacho nisaidia kufungia kijiwe cha kahawa hapa mjini, hii ni moja ya njia ambayo huwa naamini nikiitumia ntarise mtaji ndani ya miezi mitano mpaka nane the nafungua biashara nyingine.
ni hayo tu. asanteni sana
 
If you are serious ni pm, ukieleza uko wapi, unafanya nini, unapokwama ni wapi, kwa nini unakwama, ungependa usaidiwe nini, mchanganuo wa unachotaka kufanya n.k.

Lakini badala ya ku pm, unaweza pia kuchanganua hapa anaweza akajitokeza mdau akakuunga mkono.
 
Reactions: PNC
Si vizuri kuanzisha mada ndanibya mada ila nikipata nafasi nitawapa ushuhuda wangu jinsi nilivyowainua akina mama watatu wa Dar es salaam kutoka katika kutembeza mboga za majani hadi kuwa na biashara inayoingiza hadi laki 6 kwa mwezi. Hata baada kuona matunda wale akina mama wakavamia upatu kwa nguvu na sasa hivi hata ule mtaji wa mbogamboga hawana!
UMASKINI WA WATANZANIA TULIOWENGI HAUTOKANI NA KUKOSA MITAJI, AKILI ZETU HAZINA AKILI!
 
natamani kufanya hichi kibiashara lenfo kbwa ni kupandish mtaji.
kwa mtu atayekuwa tayari anisupport kupata hivi.
bench mbili ndefu, mbili fupi kiasi
meza moja ndefu futi nne na nusu na upana wake futi mbili.
kitivi kidogo kwa ajili ya wateja
mabirika manne. makubwa mawili na madogo mawili
kahawa na tangawizi
karanga mbichi na za kukaangwa
kashata
themosi nne zote mdogo
vikombe vidogo pic20
vikubwa pic 20
vikombe vya plastic saiz ya kati pic20.
asante sana
 
Swadakta! Mkuu nafikiri fikra zetu zinakaribiana sana katika hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…