Mrejesho: Mpenzi wangu tuliyekaa naye miaka mitatu sasa juzi tulipishana kiswahili

The Donchop

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
294
378
Habari wanajamii?

Natoa shukrani sana kwa wale waliojitoa kunishauri hili na lile juu ya mpenzi wangu tuliyegombana nae baada ya yeye kugombana na kaka yangu. Mpaka sasa hatujakaa chini kuongea ingawa alikuwa ameahidi hivyo ila kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake, hatukupata muda wa kutafuta suluhu.

Tunaongea vizuri kwa simu na kusalimiana kama tulivyokuwa zamani. Ingawa mimi nilikua na mashaka juu ya hatma yangu na nikamuuliza hivyo, hajanijibu lolote baya zaidi ya kukubali kusuluhisha.

Imani yangu juu yake imeshuka, sipo huru kama tulivyokuwa zamani na pia naona hayupo strong kiasi cha lolote litakalotokea kututingisha mwenzangu anatikisika. Ingawa tunacheka na kufurahi ila naona nimeshindwa.

Asanteni sana kwa ushauri wenu.
 
Mapenzi yenu ni ya kwenye simu tu. Ana kwa ana mmeshachokana. Kubali ukweli na uendelee na maisha yako.
 
Mapenzi yenu ni ya kwenye simu tu. Ana kwa ana mmeshachokana. Kubali ukweli na uendelee na maisha yako.
Hapana. Ukweli ni kuwa hanipendi tena lakini swala la kuonana ni yeye aliyedhamiria. Ilipotokea ya kutokea alinijulisha mwenyewe kwa simu nami nikatafuta ukweli kwa mama mkwe kujua kama ni kweli. Na niligundua hakunidanganya.
 
Habari wanajamii?
Natoa shukrani sana kwa wale waliojitoa kunishauri hili na lile juu ya mpenzi wangu tuliyegombana nae baada ya yeye kugombana na kaka yangu.
Mpaka sasa hatujakaa chini kuongea ingawa alikuwa ameahidi hivyo ila kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake, hatukupata muda wa kutafuta suluhu. Tunaongea vizuri kwa simu na kusalimiana kama tulivyokuwa zamani. Ingawa mimi nilikua na mashaka juu ya hatma yangu na nikamuuliza hivyo, hajanijibu lolote baya zaidi ya kukubali kusuluhisha.
Imani yangu juu yake imeshuka, sipo huru kama tulivyokuwa zamani na pia naona hayupo strong kiasi cha lolote litakalotokea kututingisha mwenzangu anatikisika. Ingawa tunacheka na kufurahi ila naona nimeshindwa. Asanteni sana kwa ushauri wenu.
ni vigumu sana kurudisha upendo uleule kwa mtu yuleyule
 
Never allow someone to be your
priority while allowing yourself to be
their option.The Donchop never love that which you cannot keep! there are a million ways to lose someone you love!

Move on brother
 
Hapana. Ukweli ni kuwa hanipendi tena lakini swala la kuonana ni yeye aliyedhamiria. Ilipotokea ya kutokea alinijulisha mwenyewe kwa simu nami nikatafuta ukweli kwa mama mkwe kujua kama ni kweli. Na niligundua hakunidanganya.
Hapo kesi ya nyani ilipelekwa kwa ngedere.eti ulitafuta ukweli kwa mama mkwe! kwa akili yako hata kama alikudanganya mama yake angemuumbua mwanae?

kweli mapenzi upofu.
 
Hapana. Ukweli ni kuwa hanipendi tena lakini swala la kuonana ni yeye aliyedhamiria. Ilipotokea ya kutokea alinijulisha mwenyewe kwa simu nami nikatafuta ukweli kwa mama mkwe kujua kama ni kweli. Na niligundua hakunidanganya.

Using'ang'anize mapenzi kaka utaumia! Mbona wanawake wapo wengi tu wenye heshima zao na mapenzi ya kweli?!!! Achana naye endelea na maisha yako. Wewe ni mtu mwenye hadhi, utu na heshima zako usikubali kujidhalilisha na kujishusha kwa asiye kuthamini.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom